Rais wa Tanzania sio rais wa Tanganyika (Wazanzibar hamjui hili?)

Wasichokijua Wazanzibari kwa sasa ni kuwa wana serikali ambayo haitambuliwi na KATIBA ya JMT. Kama ni halali au sio hilo nawaachia akina Lissu.

Ndugu yangu una uhakika kuwa SMZ haijatajwa katika katiba ya JMT? Tunaomba utujuze au kama hujui tuambia tukujuze SMZ imetajwa wapi na hadhi yake ndani ya muungano?
 
We tunalia kuwa na serikali kubwa ambayo haiendani na maisha ya wengi, af unataka tuongeze nyingine! YOU MUST BE THINKING MASABURIKALY.
 
Trust me, its just 50 years of Tanganyika (which is the real TANZANIA). others are just blackmails
 
Naikubali sana sera ya Chadema kuhusu Muungano, Serikali tatu. Demokrasia ni gharama, ccm wasituambie kuwa serikali tatu ni gharama. Ni suala la kupunguza watendaji wa hizo serikali 3 ili waendane na uwezo wetu. Sera ya serikali 2 ya ccm imekwama jumla. period
 
Nimesikitishwa na kauli za wazanzibari (kupitia kwa wabunge wao) na wengine humu JF wanaolazimisha kuwa rais wa Zanzibar na rais wa Tanzania wawe na mamlaka sawa katika suala la katiba na mustakabali wa nchi yetu.

Urais wa Tanzania sio Jakaya Kikwete. Leo hii JK akifa, ni wazi kuwa Mohamed Gharib Bilal atapishwa kuwa rais wa Tanzania. Kwa hiyo, itawezekanaje Bilal na Shein wakae kuzungumzia mustabali wa Kigoma, Mwanza, Mbeya, Bukoba, Mtwara, Tanga, nk? Kauli za wabunge hawa zinamfanya JK kuonekana kuwa ni rais wa Tanganyika na si rais wa Muungano.

Ni ‘ujuha’ kwa rais wa Tanzania kutembelea Zanzibar kama mgeni wa kitaifa wakati yupo katika nchi anayoitawala! Rais huyo huyo anapokwenda Dodoma haendi kama mgeni bali mkuu wan chi yake. RAIS WA TANZANIA SIO RAIS WA TANGANYIKA. Kwa kuongezea tu, sasa ifikie wakati kwa wabunge kukaa kama ‘bunge la Tanganyika’ na kuwatoa nje wabunge wa Zanzibar pale yanapojadiliwa mambo yasiyowahusu wa-zenji.

Kama watawaonea aibu wabunge wa Zanzibar pale Dodoma, basi wafufue bunge la Tanganyika pale Karimjee (kwa masaburi) ili Tanganyika iweze kuongea kama Tanganyika bila mwangwi wa visiwa vya Unguja na Pemba. Mungu ibariki Tanganyika

Mkuu mimi huwa sielewi wala sijielewi inapokuja kwamba wazanzibar wanashiriki kujadili mambo ambayo si ya muungano na kushiriki kupiga kula. Unakuta ati ndani ya Bunge kuna wabunge ambao wanawakilisha baraza la wawakilishi; sijui hii ni nini? Achilia mbali wabunge ambao ni kama wabunge wa kata huku Bara (Yaani mbunge anyetoka zanzibar anawakilisha watu ambao huku ni watu ambao wako katani)!! Wakati sisi watu wa Mrima hatuwezi kuwa japo Masheha huko kwao. Hii ni CHANGU CHANGU, CHAKO CHETU.
 
WaDanganyika acheni kulala mnapaswa kudai Utaifa wenu na Rais wenu kama Zanzibar.<br />
<br />
Laini naona ipo namna kwanini waTanganika hawaitaki Serikali na nchi yao ya Tanganyika kama ilivyo Zanzibar? WaZnz wanawabembeleza sana waanzisha serikali ya Tanganyika ndani a muungano lakini hawataki ndipo tunapojiuliza kuna nini hapo? Je kuna manufaa gani kwa TNG?
<br />
<br />
wadangayika ni kina nani?..
 
Naikubali sana sera ya Chadema kuhusu Muungano, Serikali tatu. Demokrasia ni gharama, ccm wasituambie kuwa serikali tatu ni gharama. Ni suala la kupunguza watendaji wa hizo serikali 3 ili waendane na uwezo wetu. Sera ya serikali 2 ya ccm imekwama jumla. period

Mkuu serikali tatu ya nini na huku CHADEMA ina sera ya Majimbo? Hapa dawa ni serikali moja kisha majimbo; Pemba jimbo na Unguja Jimbo na majimbo mengine yanatoka bara. Tumeishi takribani miaka hamsini tukiwa na serikali mbili sasa ni wakati muafaka tuwe na moja badala ya kurudi nyuma na kuwa na tatu!!
 
Tulipoteza jina letu mwaka 1964, wazanzibar mpaka leo wanalo. Muungano huu ulilenga kupoteza identity yetu?
 
Ndugu yangu una uhakika kuwa SMZ haijatajwa katika katiba ya JMT? Tunaomba utujuze au kama hujui tuambia tukujuze SMZ imetajwa wapi na hadhi yake ndani ya muungano?

Kama una hakika kuwa SMZ imetajwa katika katiba ya JMT, je una hakika pia kuwa katiba hiyo imempa rais wa SMZ nguvu sawa na za rais wa JMT?
 
Umeuliza vema, japo jibu walijua. Kwahiyo si sahihi kwa mtu na bosi wake kuwekwa level moja inapokuja katika suala la katiba. Mwinyi na Salmin wasingeweza kukaa kujadili mambo yanayohusu Biharamulo. Kwa hiyo JK hawezi kukaa na Shein wakiwa ktk level moja, huyu ni rais wa Tz na mwingine ni rais wa znz (iliyomo ndani ya tz).

Swadakta, hapo umenena lakini hujaandika ilivyo, Tanganyika hakuna. Kikwete ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dr. Shein ni Rais wa Zanzibar, vitu viwli tofauti kabisa. Na Kikwete akienda Zanzibar anakwenda ama kama Rais wa Tanzania na si Rais wa Zanzibar ama Mwenyekiti wa CCM na si Rais wa Tanzania.

Siku ukiujuwa Muungano huu ulivyo ndio siku utaujuwa Utatu ulivyo. Mungu kwa Mungu sio Mungu< Mungu duniani ni Mungu na Mungu Mwingine sijui alipo maana Mungu Watatu Kwa Mungu Mmoja wanafanya kazi zao pamoja lakini duhhhh, Hayo ndio ya Tanzania. Rais wa Tanzania si Rais wa Zanzibar lakini Rais wa Zanzibar ni Rais wa Zanznibar na Rais wa Tanzania hana mamlaka Zanzibar na Rais wa Zanzibar hana mamlaka Tanzania na Tanzania ni muungano wa Nchi zilizokuwa na Marais wawili tofauti duhhhh. Ipo kazi.

Naikumbuka Tanganyika yangu.
 
Huu muungano! Magumashi tu. Mambo ya kulazimisha tu. Wazenji wenyewe hawautaki!
 
Rais wa Tanzania ni rais wa Jamhuri ya muungano na kwa hivi ni rais wa Zanzibar vile vile. Hili alilidhihirisha Nyerere wakati alipompiga Jumbe stop 1984. Shein kama rais wa Zanzibar hana kauli katika masuala ya Morogoro na Tanga lakini kama rais wa Zanzibar akiamua kuwanyanyasa wakazi wa Bububu, rais wa Jamhuri ya Muungano anayo haki ya kupeleka geshi liwalinde wakazi wa Bububu. Upo hapo?
 
Jumbe alikuwa Makamu wa Rais wa Tanzania, usichanganye madawa.

Rais wa Tanzania hata Comoro walipokuwa wanabughudhiwa kapeleka jeshi wacha kuweza kupeleka bububu.

Nnarudia tena, siku ukiujuwa Utatu unavyofanya kazi ndio utaujuwa Muungano wa Tanzania unavyofanya kazi. Kama hujapitia kanisani kuujuwa utatu Muungano wa Tanzania uukubali tu kama ulivyo lakini kuujuwa huwezi kuujuwa. Nakiri kuwa mimi sijapitia kanisani kuujuwa utatu na kwa hilo hata Muungano wa Tanzania siujuwi ulivyo. Nipo nipo tu. Hata unieleze vipi siwezi kukuelewa, mimi najuwa zikiungana zinakuwa nchi mbili zenye muungano au inabaki kuwa moja tu. Leo tuna nchi mbili ambayo ni moja Tanzania halafu tuna nchi nyingine ambayo ni Zanzibar. Sasa Zanzibar iliungana na nani, utaniambia Tanganyika, Tanganyika iko wapi, utaniambia haipo. Sasa vipi Zanzibar iwepo? utaniambia hujui, aahhh. Msiniumize kichwa.

Naikumbuka Tanganyika yangu.
 
Mwaka huu tunasherekea miaka hamsini ya Uhuru wa nchi gani?
Tanganyika huru (1961-1964) age 2yrs 4months
Tanzania (URT) (1964- to date) age 47 years
sasa hii miaka hamsini ya kitu gani? I stand to be corrected!

Utata huu usingekuwepo tukiweka haya mambo sawa

Sherehe hizi zifutwe, au Tanganyika irudi ili ziendelee. Hivi nchi haina wanasheria, ili waweke pingamizi.
 
Habari zilizoandikwa na baadhi ya vyombo vya habari vikimnukuu Katibu mkuu wa CUF Maalim Seif Hamad kuwa sio haki kwa urais wa jamhuri ya muungano kuendelea kuwa na rais anayetoka upande mmoja wa muungano zimenishtusha.
Mimi naomba kusema kama mtu akizungumzia haki kwa njia ya haki basi ni muhimu kwa haki tukasema kama ifuatavyo.

1. Ni vizuri akasema SIO HAKI KWA ZANZIBAR KUWA NA BARAZA LA WAWAKILISHI (BUNGE) na RAIS na mawaziri wanaotoka ZANZIBAR huku bara wakishirikiana maeneo mengine yote na Zanzibar ambayo kiidadi wananchi wake hawafikii idadi ya wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam.

2. SIO HAKI RAISI WA ZANZIBAR AWEPO WAKATI TANGANYIKA HAINA RAIS WALA MAWAZIRI WALA BARAZA LA WAWAKILISHI.

3. SIO HAKI KUWA NA UTAMBULISHO WA UPANDE MMOJA WAKATI UPANDE MWINGINE UTAMBULISHO WAKE UKIFA NA KUZIKWA.

4. SIO HAKI KWA UPANDE MMOJA WA MUUNGANO KUWA NA KATIBA YAKE WAKATI UPANDE WA PILI HAUNA.

5. SIO HAKI KWA UPANDE MMOJA (ZANZIBAR) KULINDA JINA LAKE WAKATI UPANDE WA PILI ( TANGANYIKA) JINA LAKE LIKIFA.

6. SIO HAKI KWA WATU WA ZANZIBAR KUEGEMEA DINI MOJA HUKU WAKIJUA DINI NYINGINE ZILIZOKO BARA WATU WAKE WANAPASWA KUPEWA HAKI YA KUENDELEZA DINI YAO ZANZIBAR

7. SIO HAKI KUZUNGUMZIA HAKI YA UPANDE WAKO TU WAKATI UKIJUA WAZI KUWA KUNA HAKI NYINGI ZA UPANDE WA PILI AMBAZO HAZIJAPEWA UZITO KATIKA KUZUNGUMZIWA. NI KAMA KUZUNGUMZIA HAKI YA ASIYE NA MIGUU ALIYEPAKIWA KWENYE BAISKELI KUENDESHA KWA ZAMU HUKU UKIJUA MATOKEO YAKE
 
Hapa juu yako mengi ambayo hata siwezi kumaliza kuyaweka hapa, Ukifuatia haki ya makazi, ardhi nk basi utagundua kuwa suala la haki katika muungano wetu ni haki zaidi kwa upande mmoja tu.
 
Ndugu zangu mm nimezaliwa nimeikuta tanzania ambayo ni nchi iliyoungana kati ya tanganyika na zanzibar.Kila mwaka kuna sherehe za kitaifa za kusheherekea Kuzaliwa kwa nchi hizo kule zanzibar kuna raisi anayesimamia kazi za kila siku na sherehe lakini huku tanganyika raisi wetu nani?nani anasimamia kazi za kila siku za tanganyika?naombeni mnisaidie jee mambo yetu ya tanganyika yanajadiliwa katka bunge gani?nisaidieni watanzania
 
Tanganyika haipo ndio maana haina rais. Lakini mambo yasiyo ya muungano yanashughulikiwa na JK+ ya muungano.
 
Back
Top Bottom