Crucifix,Pasco siafikiani na wewe. Ninaangazia 'angles' zote mkuu. Ni kwa kujiamini huko ndio maana tumejiachia bila tahadhari kwa kudhani kuwa siku zote rais wa muungano hatatoka znz kupitia uchaguzi na eti bara tutatawala siku zote kwa uwingi wetu. Vipi rais akifa akiwa madarakani na katiba inatamka makamu ndiye anachua urais? Bado utasema tena kuwa chance ya mwisho ilikuwa kwa Dr Salim? Au kuna mkakati wa rais na makamu wote kutoka Tanganyika?
Rais akifa katiba inaitisha makamu rais ashike madaraka nadhani kwa siku tisini. Baada ya hapo uchaguzi unafanyika. Na uwezekano unaweza kuwa mkubwa kwamba makamu rais (Mzanzibari) hatapata kura za Busegwe.