goldensylva
Member
- Sep 29, 2010
- 35
- 14
Inashangaza na kusikitisha Raisi wa nchi anaposifia faida kubwa wanayopata Makampuni ya Simu Binafsi. Ningeweza kuelewa kama ingekua ni TTCL, shirika la serikali ambalo limeshindwa ubunifu na makampuni binafsi na sasa lipo kihasara hasara. Watumiaji wameongezeka kwa asilimia 50 ndio, je watumiaji hao ni kina nani? Vipi kuhusu gharama za huduma za makampuni hayo ya simu kuwa kubwa kuliko hizo nchi zinazoongoza kwa wateja Afrika?
Watumiaji wa simu waongezeka kwa asilimia 50
Tuesday, 23 November 2010 21:33 Mwananchi
Hussein Issa Mwananchi
RAIS Jakaya Kikwete amesema amefarajika baada ya kuambiwa kuwa wanaotumia wa simu za mkononi wameongezeka nchini kwa asilimia 50.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kikwete alisema idadi ya watumiaji wa simu za mkononi wameongezeka kwa asilimia 50 na kwamba watumiaji wanasababisha maendeleo makubwa nchini.
"Maendeleo katika nchi yoyote ile yanaletwa kwa njia ya mawasiliano ya simu na kama nchi haina huduma hiyo, uwezekano wa kupata maendeleo hayo ni mgumu,"alisema.
Akizungumza katika hafla ya kubadilisha mmiliki wa simu ya Zain na kuitwa AIRTEL jijini Dar es salaam, Kikwete alisema nchi ya Tanzania ni ya nne Afrika kwa matumizi ya simu baada ya Nigeria, Afrika ya Kusini na Kenya.
Kwa mujibu wa Rais, umuhimu wa simu pia unaonekana katika sehemu ambazo hamna huduma za kibenki, kwani watumiaji wanaweza kutumia huduma ya M-Pesa ,tiGopesa, Zap and Z-pesa.
"Mtanikubalia kuwa miongoni mwa sekta ambazo zinakuza uchumi nchini ni mawasiliano kwa njia ya simu, kwa muda wa miaka mitano kuanzia mwaka 2005 hadi 2009, sekta hii imekuza uchumi kwa asilimia 20.1,"alisema.Alisema kwa watumiaji wanakabiliwa na matatizo ya gharama kubwa za simu za mkononi hasa kwa watumiaji wa vijijini hususan maeneo ya vijijini ambao pia wana uwezo mdogo wa kutumia.