Rais wa Tanzania kwenye uzinduzi wa Airtel

Inashangaza na kusikitisha Raisi wa nchi anaposifia faida kubwa wanayopata Makampuni ya Simu Binafsi. Ningeweza kuelewa kama ingekua ni TTCL, shirika la serikali ambalo limeshindwa ubunifu na makampuni binafsi na sasa lipo kihasara hasara. Watumiaji wameongezeka kwa asilimia 50 ndio, je watumiaji hao ni kina nani? Vipi kuhusu gharama za huduma za makampuni hayo ya simu kuwa kubwa kuliko hizo nchi zinazoongoza kwa wateja Afrika?



Watumiaji wa simu waongezeka kwa asilimia 50
Tuesday, 23 November 2010 21:33 Mwananchi

Hussein Issa Mwananchi

RAIS Jakaya Kikwete amesema amefarajika baada ya kuambiwa kuwa wanaotumia wa simu za mkononi wameongezeka nchini kwa asilimia 50.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kikwete alisema idadi ya watumiaji wa simu za mkononi wameongezeka kwa asilimia 50 na kwamba watumiaji wanasababisha maendeleo makubwa nchini.

"Maendeleo katika nchi yoyote ile yanaletwa kwa njia ya mawasiliano ya simu na kama nchi haina huduma hiyo, uwezekano wa kupata maendeleo hayo ni mgumu,"alisema.

Akizungumza katika hafla ya kubadilisha mmiliki wa simu ya Zain na kuitwa AIRTEL jijini Dar es salaam, Kikwete alisema nchi ya Tanzania ni ya nne Afrika kwa matumizi ya simu baada ya Nigeria, Afrika ya Kusini na Kenya.


Kwa mujibu wa Rais, umuhimu wa simu pia unaonekana katika sehemu ambazo hamna huduma za kibenki, kwani watumiaji wanaweza kutumia huduma ya M-Pesa ,tiGopesa, Zap and Z-pesa.

"Mtanikubalia kuwa miongoni mwa sekta ambazo zinakuza uchumi nchini ni mawasiliano kwa njia ya simu, kwa muda wa miaka mitano kuanzia mwaka 2005 hadi 2009, sekta hii imekuza uchumi kwa asilimia 20.1,"alisema.Alisema kwa watumiaji wanakabiliwa na matatizo ya gharama kubwa za simu za mkononi hasa kwa watumiaji wa vijijini hususan maeneo ya vijijini ambao pia wana uwezo mdogo wa kutumia.
 
kweli huduma za simu zipo juu compare to other country ambao matumizi yao sio kama tz, na coz watanznia wengi hawajasoma basi wanaibiwa sana na mampuni haya ya simu.......I HATE VODACOM ingekuwa uwezo wangu hii kampuni ningeikorogea sumu
 
Yani humu hakuna Jema kwa JK, kila kitu mnakosoa tu kha!!! Give him a break jamani fanyeni kazi acheni kulalamika
 
Tunachokuomba Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuwaeleza wawekezaji hususani Airtel walipe kodi na uwepo wako katika uzinduzi haina maana ya kwamba umefungulia mlango wa makampuni hayo kutokulipa kodi. Ninaomba vivile uwe mkali kwa wawekezaji ambao wanakuja kwa lengo la kuwatumia watanzania kujipatia utajiri huku watanzania wenyewe wakibakia kuwa masikini. Tafadhali sana Mheshimiwa Rais usiwathamini wawekezaji kuliko wananchi wako. Kumbuka ukitufanyia hiana hata Mwenyenzi Mungu hatokusamehe?
 
Nani kasema hatufanyi kazi? Unajua kila anachofanya mwanajamii forum? Tukuulize wewe **** je lipi zuri alilofanya JK katika uzinduzi wa airtel? Rais makini hawezi kujishughulisha na mambo madogo kama hayo ana Makatibu wakuu wa wizara husika kwa nini wasifanye hilo kwa niaba yake? Labda ni kampuni yake ambayo nina uhakika kama ndivyo haimsaidia Mtanzania? Tanzania ina mambo makubwa ambayo yanahitaji attention ya Rais na si hayo ya airtel? Watu wanazungumza kwa uzoefu tulio nao kwa Rais wetu. Mwaka 2009 tulipata janga la mafuriko Kilosa Morogoro; wakati huo wa janga la kitaifa Rais wetu yupo katika hoteli za kitalii anakula Lunch na Drogba. Give a break .......... the same is happening, he has more important national issues to address which are more important to Tanzania than what he went to do with airtel. he deserve every bad comment on his unacceptable actions.
 
" Faraja ya Mwekere iwe ni ongezeko la pato la kaya kwa watanzania kwa asilimia hamsini na si yale ya matumizi ya simu". Pamoja na mawasiliano kuwa muhimu tujiulize ni kiasi gani cha fedha kinachotengenezwa kwa watu kuwasiliana kwa maana ya kodi kinachokwenda kurekebisha maisha ya mtanzania masikini? Kama angeliweza kuunganisha kukua kwa utumiaji wa simu na kuimarika kwa maisha ya mtanzania maskini ningefunga domo langu lakini sioni hilo. Hivyo basi sioni anachofarijika labda kuna anachopata yeye na si watanzania ndio maana anafarija. Lakini mimi faraja hiyo hainisaidi kabisa.
 
Nawasikitikieni sana nyie hapa!!! Zaidi ya nusu ya wawekezaji wanaotajwa kuwekeza kwenye zilizokua mashirika ya umma yaliuzwa bei chee hapo nyuma si wa nchi za nje wala nini.

Ni wa-Tanzania MAFISADI ambao ndio walionyakua mali za Watanzania kwa kujificha nyuma ya majina ya mikampuni ya njee. Nakuambia siku Wa-Tanzania waliowengi watakapoelewa hili nchi haitokalika.

Hiyo kambuni Tangu Celtel, iliomega mali zetu pale Kijitonyama bila kulipa hata senti, hadi leo hii 'AirTel' na kesho sijui itakua kitu gani, yote ni kuendelea kututoroka kabisa na kilicho halali yetu. Ole Naiko pale TIC anajua sana picha nzima.
Kawekwa na Lowassa pamoja na Rostam Aziz kwa ajili hio.
Mkuu hongera sana komenti yako itaishi na itaendelea kuishi hakika uliona mbali
 
Wadau naomba kuuliza hivi kama Raisi wa nchi anahudhuria uzinduzi wa ubadilishwaji/uhuzwaji wa kampuni ya simu, Je ni zinduzi ngapi kama hizi atahuzuria kwa kipindi chote atakachokuwa madarakani?

Hofu yangu ni kuwa NIKIASI GANI ZAIN/AIRTEL WAMECHANGIA KWENYE KAMPENI ZA UCHAGUZI CCM?

My take:
Kila kitu kinabei yake hapa TANZANIA.

Kikwete_Airtel.jpg


President Jakaya Mrisho Kikwete together Airtel Tanzania Managing Director Sam Elangalloor
Siku zote muda ni mwalimu mzuri sana! Tunafukua makaburi...
 
fagia baba naamini hatobaki mtu salama
ni wakat sasa wa kumuunga mkono jpm na kusema uhuni kwenye rasilimali zetu sasa baasi....
kwa ufukuaji makaburi wa namna hii hata mm ningekua mbunge wa chadeNCCRCUFTLP ningejiuzuru wadhifa wangu na kumuunga mkono muungwana mtukufu rais john pombe
 
fagia baba naamini hatobaki mtu salama
ni wakat sasa wa kumuunga mkono jpm na kusema uhuni kwenye rasilimali zetu sasa baasi....
kwa ufukuaji makaburi wa namna hii hata mm ningekua mbunge wa chadeNCCRCUFTLP ningejiuzuru wadhifa wangu na kumuunga mkono muungwana mtukufu rais john pombe
Hahaha
 
Back
Top Bottom