mkuu hebu tuwekee kwa kifupi ni kipi kilichosemwa.sina access na hicho kipindi kabisaMkulu alikuwa anahojiwa na MSNBC lakini kipindi kimeisha labda marudio baadae
Nadhani atatumia lugha ya kiingereza...Umesikia wanasema 'He is a very special man'
Mimi naogopa kusikiliza kama ni kwa lugha ya Malkia maana lugha gongana kwa mkulu
Mara 1000 ningeona rais anafanya jambo la maana kwa kuitisha mkutano wa kitaifa unaojumuisha watu mbalimbali wa matabaka mbalimbali na kujadili namna ya kuondoa umaskini. Ifike mahali sasa kama taifa tuwaambie viongozi wetu waache kutuabisha na kutafuta majawabu kwa wanyonyaji.
Watanzania ndio wanaokumbana na adha ya umaskini, lakini kwa hakika ni watanzania hawa hawa maskini ndio wenye majawabu juu ya namna ya kutokomeza umaskini. Tatizo tulilo nalo ni kasumba mbaya kwa viongozi wetu kujadili with the wrong people.
Hii campaign ya nutrition imeletwa na Marekani. It is not coming from us, na kwa mtu mwenye akili timamu Marekani wamebuni hii campaign kama njia mojawapo ya kupambana na influence ya China Africa. Wanajua watu wengi bado hawana chakula cha kutosha, na mchina yeye haongei mambo ya chakula, sasa wanacheza na akili za viongozi wetu. Na campaign inaongozwa na shirika lao USAID. kila anapokwenda Kikwete anakumbana na mkurugenzi wa USAID! Inakuwaje? Mbona hao USAID hawawagandi wakenya? Au Tanzania wana shida ya chakula kuliko Kenya?
hongera sana kikwete
wewe ni malalamikaji tu,hebu jiulize wewe umefanya nini kuondoa umaskini wa watanzania zaid ya kubeza wanayofanya wengine.