Rais wa Tanzania anatakiwa kuwa huyu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais wa Tanzania anatakiwa kuwa huyu

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Igabiro, Sep 3, 2010.

 1. Igabiro

  Igabiro JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2010
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 242
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mtanzania yeyote Mzalendo wa kweli, mwenye akili timamu, asiye na mtindio wa ubongo, wala mtumwa wa hila chafu, wala udumavu wa kiakili, tena asiye na utando wa buibui wala tongotongo za ufisadi machoni, wala asiye mzembe wa kufikiri, anaalikwa asome kwa uangalifu na azingatie makala hii na awashirikishe ndugu, jamaa na marafiki zake popote pale walipo..

  Dr Slaa yes we can! Huyu ni mtanzania wa pili baada ya Nyerere kuchukia ufisadi kwa vitendo. Ni mtanzania wa pili kuchukia umaskini wa watanzania kwa vitendo. Ni Dr. Slaa aliyesimama na kutaja majina ya wala rushwa na mafisadi. Akataka wale wanaopinga wampeleke mahakamani. Hakuna aliyethubutu kujitokeza kumpeleka mahakamani.

  Ni Dr. Slaa aliyesimama bungeni kuomba posho za wabunge kupungzwa kuzielekeza zaidi kwa watanzania maskini. Ni Dr Slaa aliyesimama bila woga kunyosha vidole kwa matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa amekuwa mtanzania baada ya Nyerere kutoa hoja za nguvu zinazomlenga kumkomboa mtanzania maskini. Maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi? Ajira milioni moja ziko wapi? Hebu mwenye mbavu za kujibu swali hili ajibu bila unafiki!

  Ni Dr Slaa anayeweza kudhibiti matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa anayeweza kuwapa elimu ya bure watoto wetu pale mlimani. Achana na longolongo za CCM kuwatoza ushuru watoto. Waulizeni majukwaani wao Nyerere aliwatoza ada? Kama si kutaka watanzania waendelee kuwa mambumbumbu ni nini? kama si kutaka watanzania tuendeleee kuwa watumwa ni nini?

  Ni Dr. Slaa anayeongelea treni ya umeme kwenda Kigoma, Dodoma, Tabora, na Mwanza. Waulize mpango wao ccm kama si kuwapa wahindi wanaoleta mabehewa ambayo mababu zetu walitumia wakati wa ukoloni. Sasa wahindi wanabaki kutudanganya na bajaji wakati vyuma chakavu vya reli sasa vinatumika kujenga vyoo. Hawa hawatutakii mema. Hawana tofauti na akina Carl Peters.

  Ni Dr Slaa anayeongelea mfumko wa bei -nani hajajua dola leo hii ni sawa na tsh 1500. Uchumi unadidimia kwa kasi. Ahadi nyingine za uongo lukuki zinatolewa tena, wakati zile tulizoahidiwa mwaka 2005, hata moja haijatekelezwa. Watanzania walio wengi na hasa wa vijijini, wamelala usingizi. Wanafumbuliwa macho, lakini wamesinzia bado! Wanatabasamu, wanachekelea na kuridhika na vitisheti vya kijani na vikofia za njano. Wamekwishazoea shida kiasi kwamba wanadhani ni sehemu ya maisha yao. Ee mwenyezi Mungu, tunusuru na hili balaa..

  Ni Dr.Slaa anaweza kuzuia wizi wa matrilion ya pesa kutoka migodi yetu ya Buzwagi, Geita, Bulyankulu, Buhemba, Nyamongo, Tulawaka, Nzega na Tanzanite. CCM wameshindwa kwa sababu ni washirka wakubwa na wameruhusu wizi huo. Ni Dr Slaa anaeweza kuwalipa wafanyakazi zaidi ya shilingi 350.000 achana na CCM ambayo imeshindwa kusimamia maliasili ambazo zingeliwapa wafanyakazi kima cha chini kinachokidhi mahitaji yao.

  Ni Dr.Slaa anayeweza kusimamia mashirika ya umma kuleta tija achana na CCM wanaofyonza michango yetu kule, kwani haya mashirika yameshindwa nini kuwajengea nyumba wanachama wake? Mbona kwingine yameweza? Ni Dr.Slaa anayeweza kuongoza nchi bila woga, kwa utawala wa kweli wa sheria bila kuwaonea watu wala bila kulipiza visasi.

  Ni Dr. Slaa ambaye amepanga kubadili katiba ili Rais afuate matakwa ya walio mwajiri ambao ni wananchi. Waulize CCM hata kama mtu kaiba anapewa mda arudishe pesa. Hivi inaingia akilini kweli? Utawala wa sheria uko wapi? Naomba niwape heko ITV kwa kuturejeshe kwenye hotuba za mwalimu. Katika hotuba yake moja alisema waziri mmoja kule uingereza aliandikwa kidogo tu gazetini juu ya kashfa, yule waziri alijiuzulu na waziri mkuu hata hakumjibu bali aliteua mtu mwingine.

  CCM hawawezi hayo? Eti wanataka ushahidi. Nani kawambia rushwa tule wawili harafu tutoe vielelezo? Tunaiona rushwa kwa matokeo yake. Matengenezo ya barabara ya bilion 200, baada ya siku mbili imeharibika. Kwanini usimfukuze waziri na katibu wake wa wizara kwanza? CCM hawawezi! eti wanataka vielelezo!

  Ni Dr Slaa anayeweza kufanya hayo. Si tumeona mnazi mmoja alivyowataja mafisadi wote! hapo akiwa ni mbunge tu! Je akiwa rais si watakimbia nchi? Jamani nawambia tumpe miaka mitano tu awakurupushe muone moto utakavyowaka.. Tutapata dawa, tutapata shule za bure, tutapata madawati. Jamani hivi kweli karne ya leo watoto wanasoma wamekaa chini? we must be serious! Hivi kweli dunia ya leo watu wanavuliwa nguo njiani kwenda Mwanza, Shinyanaga, Tabora, Kigoma, Mbeya, Lindi na Mtwara kwa sababu ya usafiri wa malori?

  Nani asiye jua madaktari wetu wengi bingwa wapo botswana kwa sababu ya maisha duni Tanzania na hivi kwenda kutafuta maisha bora wakati hapa kwetu wananchi maskini wanakufa bila madawa? Nani asiyejua matatizo ya umeme, maji, makazi, maradhi, yanavyotutesa? Nani asiyejua wakulima wetu wasivyokuwa na masoko ya mazao yao? Nani asiejua asilimia 85 ya watanzania wanatumia vibatari au makoroboi kama mwanga? nani asiejua tunavyonyonywa na hawa wakoloni waliokuja kuchukua kila kitu??

  Jamani wafanyakazi, wakulima, na wanafunzi, kwa nini mnalala usingizi? Kwa nini mnapiga miayo ya njaa wakati maghala yetu yamejaa nafaka? Ni akili gani hii? Nchi yetu inazo raslimali za kututosha, lakini wanaozifaidi ni vibaka wachache. Mtalala hadi lini?

  Ni Dr Slaa mzalendo wa kweli, na sio kwa ajili ya sifa, anaweza kutuvusha tulipo. Nchi hii ni maskini na umaskini wenyewe ni wa kujitakia. Tanzania ni tajiri tuna kila kitu - mito, maziwa, national parks, migodi, mazao ya misitu, na kila aina ya utajiri. Lakini tuko maskini wa kutupwa! Naona huruma na umaskini wa kifikra wa watanzania.

  Hivi kuna mtu hajui mapolisi wanalala kwenye vibanda vya mabati? Hivi kuna ambao hawajui mapolisi watendaji wanalipwa laki moja? Wamekosa nini hawa? Ni ajabu! pamoja na laki yao moja utakuta bado wanatumika kuwanyanyasa watetezi wao. Hata maaskari amkeni hiyo laki moja yenu haina tija hadi mrubuniwe kuwanyanyasa wapinzani ambao kimsingi wanawatetea ninyi! Hivi maaskari mnayo macho ya kuona? Jamani tuache woga inawezekana! Mbona Kenya wameweza? Mbona malawi wameweza?Mbona zimbabwe wameweza? Mbona Ghana wameweza? Kufanya mabadiliko sahihi, inawezakana na nafasi ni hii tuitumie.

  Tumtume Dr Slaa atukurupushie wezi wote na atuwekee katiba sawa. Huo ndio msingi wa yote. Ni Dr. Slaa asiyeogopa kuwepo na mgombea binafsi. CCM hili hawaliwezi. Wamelipinga hadi mahakamani. Wanataka wao tu ndio waendelee kututawala na kutunyonya.

  Jamani 2010 hakuna kudanganyika! enough is enough. Acheni kudanganyika. Wakati ndio huu. Watanzania msipoamua sasa, mtamlaumu nani tena? Nawatamani watu wa kule Mara -hakuna kura inaibiwa. Zote zinasimamiwa. Tukibadilika inawezekana, tena ni rahisi. Peleke ujumbe huu kwa marafiki, ndugu, jamaa, babu na bibi yako kule kijiji ambako wanadhani bado Nyerere ndiye rais wa nchi hii. Peleka ujumbe huu haraka kwa simu kama ipo, au kwa njia ya posta, mradi tu wale jamaa waliochoka kuishi wasiikwapue barua wakidhani ni hela..
   
 2. Bado Niponipo

  Bado Niponipo JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2010
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 680
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  ANGALIA NITAKAVYO GONGEWA THENKSI HAPO CHINI....LOL!

  I would ask watanzania wenzangu to think about what am going
  to talk about with reasoning. It is not easy for a president kutekeleza

  Vitu vyote ambavyo aliahidi in just the first term. now imagine how far we could go in 10yrs?Put in mind that most presidents don't do whatever they set out to do in their terms, so if we keep changing presidents every
  after 5yrs ,surely TUTAFIKA POPOTE?

  We definitely still need PEACE. And who is better at peace keeping than JAKAYA KIKWETE .We have all seen how he proved to us as concerning regional peace when he settled issues among the Kenyans during their rough political
  times, now think about peace keeping at local level !

  All these false accusation concerning corruption involving him, do u think we would even get to hear about EPA if it was not for him to grant freedom of speech to the press. Otherwise u would never have heard about all
  the corruption issues, NOW think about it, do u think u will still have the
  freedom to know what really goes on in your country if it was otherwise?

  Formatting the system: let me use the simplest example, if u had a lot of data on your laptop and one day u decide to format it u obviously loose what is in it.dat way watanzania tuwe makini with the decisions we make because
  tume toka mbali to risk it all na I know u have no guarantee that if u lost it
  u would get better.

  At least now I can say I am from Tanzania in a chat room and my next reply wouldn't be (what's that? Or where is that)all thanks to our MAN JK for doing his best in advertising the country. This has
  being made in many ways .most African countries are known through wrong and
  negative ways like Kenya for its political instability nature, Uganda for its
  un democratically nature and life loss but TANZANIA: for:

  1. Hosting the World Economic forum in Dar es salaam from 5th-7th may2010

  2. Hosting the SULIVAN SUMMIT meeting in Arusha

  3. Hosting a friendly match between Brazilian national team and the Taifa stars on 7th june 2010 in dare s salaam at Benjamin Mkapa National Stadium

  4. Invited George W. Bush to Tanzania on 5th Feb.2008

  5. Being the first African President to officially meet the President of the USA. BARACK OBAMA

  6. For chairing African Union

  7. Inviting the president of the Republic of China Hu Jintao to Tanzania

  8. And etc

  NOW ASK YOURSELF WOULD ANYONE ELSE BE ABLE TO DO ALL THESE THINGS IN JUST THE FIRST FIVE YEARS?AND I GUARANTEE U WITH THIS I CAN SEE TANZANIA VERY FAR IN 10YRS AND MORE TO COME.

  BABKUBWA.NING
   
 3. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2010
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Karibu JF

 4. Bado Niponipo

  Bado Niponipo JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2010
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 680
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Aliambiwa 75% wa wadanganyika ni wafuata upepo.

  Anapima upepo.

  Mbayuwayu + ya kwako= akili mukichwa
   
 5. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #5
  Sep 3, 2010
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Yaani kuna mtu anaweza kujivunia haya? Ona hakuna chochote kilichomlenga mwananchi wa kawaida na maisha yake ya umasikini yanayohitaji huduma safi za maji, huduma nzuri za afya, huduma nzuri za mawasiliano ya barabara, shule nzuri zenye walimu nk
   
 6. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #6
  Sep 3, 2010
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160

  Umemaliza, kwa ufupi prezidaa ni muuza sura tu!!
   
 7. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #7
  Sep 3, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Bado nipo naona utaendelea kuwepo,wewe kama wewe umefaidikaje na mambo uliyoyataja?
   
 8. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #8
  Sep 3, 2010
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Una maana rais anayeweza kumlkaribisha rais wa nchi nyingine kuitembelea nchi yake ni kikwete peke yake? Wewe ulifaidi nini walipokuja hao watu?
   
 9. R

  Reyes Senior Member

  #9
  Sep 3, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  SOMA KWA UMAKINI  Mtanzania yeyote Mzalendo wa kweli, mwenye akili timamu, asiye na mtindio wa ubongo, wala mtumwa wa hila chafu, wala udumavu wa kiakili, tena asiye na utando wa buibui wala tongotongo za ufisadi machoni, wala asiye mzembe wa kufikiri, anaalikwa asome kwa uangalifu na azingatie makala hii na awashirikishe ndugu, jamaa na marafiki zake popote pale walipo..

  Dr Slaa yes we can! Huyu ni mtanzania wa pili baada ya Nyerere kuchukia ufisadi kwa vitendo. Ni mtanzania wa pili kuchukia umaskini wa watanzania kwa vitendo. Ni Dr. Slaa aliyesimama na kutaja majina ya wala rushwa na mafisadi. Akataka wale wanaopinga wampeleke mahakamani. Hakuna aliyethubutu kujitokeza kumpeleka mahakamani.

  Ni Dr. Slaa aliyesimama bungeni kuomba posho za wabunge kupungzwa kuzielekeza zaidi kwa watanzania maskini. Ni Dr Slaa aliyesimama bila woga kunyosha vidole kwa matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa amekuwa mtanzania baada ya Nyerere kutoa hoja za nguvu zinazomlenga kumkomboa mtanzania maskini. Maisha bora kwa kila mtanzania yako wapi? Ajira milioni moja ziko wapi? Hebu mwenye mbavu za kujibu swali hili ajibu bila unafiki!

  Ni Dr Slaa anayeweza kudhibiti matumizi mabaya ya ofisi za umma. Ni Dr Slaa anayeweza kuwapa elimu ya bure watoto wetu pale mlimani. Achana na longolongo za CCM kuwatoza ushuru watoto. Waulizeni majukwaani wao Nyerere aliwatoza ada? Kama si kutaka watanzania waendelee kuwa mambumbumbu ni nini? kama si kutaka watanzania tuendeleee kuwa watumwa ni nini?

  Ni Dr. Slaa anayeongelea treni ya umeme kwenda Kigoma, Dodoma , Tabora, na Mwanza. Waulize mpango wao ccm kama si kuwapa wahindi wanaoleta mabehewa ambayo mababu zetu walitumia wakati wa ukoloni. Sasa wahindi wanabaki kutudanganya na bajaji wakati vyuma chakavu vya reli sasa vinatumika kujenga vyoo. Hawa hawatutakii mema. Hawana tofauti na akina Carl Peters.

  Ni Dr Slaa anayeongelea mfumko wa bei -nani hajajua dola leo hii ni sawa na tsh 1500. Uchumi unadidimia kwa kasi. Ahadi nyingine za uongo lukuki zinatolewa tena, wakati zile tulizoahidiwa mwaka 2005, hata moja haijatekelezwa. Watanzania walio wengi na hasa wa vijijini, wamelala usingizi. Wanafumbuliwa macho, lakini wamesinzia bado! Wanatabasamu, wanachekelea na kuridhika na vitisheti vya kijani na vikofia za njano. Wamekwishazoea shida kiasi kwamba wanadhani ni sehemu ya maisha yao . Ee mwenyezi Mungu, tunusuru na hili balaa..

  Ni Dr.Slaa anaweza kuzuia wizi wa matrilion ya pesa kutoka migodi yetu ya Buzwagi, Geita, Bulyankulu, Buhemba, Nyamongo, Tulawaka, Nzega na Tanzanite. CCM wameshindwa kwa sababu ni washirka wakubwa na wameruhusu wizi huo. Ni Dr Slaa anaeweza kuwalipa wafanyakazi zaidi ya shilingi 350.000 achana na CCM ambayo imeshindwa kusimamia maliasili ambazo zingeliwapa wafanyakazi kima cha chini kinachokidhi mahitaji yao .

  Ni Dr.Slaa anayeweza kusimamia mashirika ya umma kuleta tija achana na CCM wanaofyonza michango yetu kule, kwani haya mashirika yameshindwa nini kuwajengea nyumba wanachama wake? Mbona kwingine yameweza? Ni Dr.Slaa anayeweza kuongoza nchi bila woga, kwa utawala wa kweli wa sheria bila kuwaonea watu wala bila kulipiza visasi.

  Ni Dr. Slaa ambaye amepanga kubadili katiba ili Rais afuate matakwa ya walio mwajiri ambao ni wananchi. Waulize CCM hata kama mtu kaiba anapewa mda arudishe pesa. Hivi inaingia akilini kweli? Utawala wa sheria uko wapi? Naomba niwape heko ITV kwa kuturejeshe kwenye hotuba za mwalimu. Katika hotuba yake moja alisema waziri mmoja kule uingereza aliandikwa kidogo tu gazetini juu ya kashfa, yule waziri alijiuzulu na waziri mkuu hata hakumjibu bali aliteua mtu mwingine.

  CCM hawawezi hayo? Eti wanataka ushahidi. Nani kawambia rushwa tule wawili harafu tutoe vielelezo? Tunaiona rushwa kwa matokeo yake. Matengenezo ya barabara ya bilion 200, baada ya siku mbili imeharibika. Kwanini usimfukuze waziri na katibu wake wa wizara kwanza? CCM hawawezi! eti wanataka vielelezo!

  Ni Dr Slaa anayeweza kufanya hayo. Si tumeona mnazi mmoja alivyowataja mafisadi wote! hapo akiwa ni mbunge tu! Je akiwa rais si watakimbia nchi? Jamani nawambia tumpe miaka mitano tu awakurupushe muone moto utakavyowaka.. Tutapata dawa, tutapata shule za bure, tutapata madawati. Jamani hivi kweli karne ya leo watoto wanasoma wamekaa chini? we must be serious! Hivi kweli dunia ya leo watu wanavuliwa nguo njiani kwenda Mwanza, Shinyanaga, Tabora, Kigoma, Mbeya, Lindi na Mtwara kwa sababu ya usafiri wa malori?

  Nani asiye jua madaktari wetu wengi bingwa wapo botswana kwa sababu ya maisha duni Tanzania na hivi kwenda kutafuta maisha bora wakati hapa kwetu wananchi maskini wanakufa bila madawa? Nani asiyejua matatizo ya umeme, maji, makazi, maradhi, yanavyotutesa? Nani asiyejua wakulima wetu wasivyokuwa na masoko ya mazao yao ? Nani asiejua asilimia 85 ya watanzania wanatumia vibatari au makoroboi kama mwanga? nani asiejua tunavyonyonywa na hawa wakoloni waliokuja kuchukua kila kitu??

  Jamani wafanyakazi, wakulima, na wanafunzi, kwa nini mnalala usingizi? Kwa nini mnapiga miayo ya njaa wakati maghala yetu yamejaa nafaka? Ni akili gani hii? Nchi yetu inazo raslimali za kututosha, lakini wanaozifaidi ni vibaka wachache. Mtalala hadi lini?

  Ni Dr Slaa mzalendo wa kweli, na sio kwa ajili ya sifa, anaweza kutuvusha tulipo. Nchi hii ni maskini na umaskini wenyewe ni wa kujitakia. Tanzania ni tajiri tuna kila kitu - mito , maziwa, national parks, migodi, mazao ya misitu, na kila aina ya utajiri. Lakini tuko maskini wa kutupwa! Naona huruma na umaskini wa kifikra wa watanzania.

  Hivi kuna mtu hajui mapolisi wanalala kwenye vibanda vya mabati? Hivi kuna ambao hawajui mapolisi watendaji wanalipwa laki moja? Wamekosa nini hawa? Ni ajabu! pamoja na laki yao moja utakuta bado wanatumika kuwanyanyasa watetezi wao. Hata maaskari amkeni hiyo laki moja yenu haina tija hadi mrubuniwe kuwanyanyasa wapinzani ambao kimsingi wanawatetea ninyi! Hivi maaskari mnayo macho ya kuona? Jamani tuache woga inawezekana! Mbona Kenya wameweza? Mbona malawi wameweza?Mbona zimbabwe wameweza? Mbona Ghana wameweza? Kufanya mabadiliko sahihi, inawezakana na nafasi ni hii tuitumie.

  Tumtume Dr Slaa atukurupushie wezi wote na atuwekee katiba sawa. Huo ndio msingi wa yote. Ni Dr. Slaa asiyeogopa kuwepo na mgombea binafsi. CCM hili hawaliwezi. Wamelipinga hadi mahakamani. Wanataka wao tu ndio waendelee kututawala na kutunyonya.

  Jamani 2010 hakuna kudanganyika! enough is enough. Acheni kudanganyika. Wakati ndio huu. Watanzania msipoamua sasa, mtamlaumu nani tena? Nawatamani watu wa kule Mara -hakuna kura inaibiwa. Zote zinasimamiwa. Tukibadilika inawezekana, tena ni rahisi. Peleke ujumbe huu kwa marafiki, ndugu, jamaa, babu na bibi yako kule kijiji ambako wanadhani bado Nyerere ndiye rais wa nchi hii. Peleka ujumbe huu haraka kwa simu kama ipo, au kwa njia ya posta, mradi tu wale jamaa waliochoka kuishi wasiikwapue barua wakidhani ni hela
   
 10. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #10
  Sep 3, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Sawa mkuu!
   
 11. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #11
  Sep 3, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Thanks
   
 12. Xuma

  Xuma JF-Expert Member

  #12
  Sep 3, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 631
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  I'd say watu ka wewe hamhitajiki nchini kwetu.
   
 13. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #13
  Sep 4, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145

  Reyes,

  Kumbe nawe u mzalendo? Kweli, kama wangekuwapo watu kama wewe 20 tu, basi Tanzania hii ingekuwa mbele sana katika kupambana na ufisadi.

  Tatizo ni kwamba, CCM haikupambana na maadui wa asili - ujinga, umaskini na maradhi - kwa kuwa walitambua kwamba kufanya hivyo WANGEKOSA SABABU ya kuwaibia Watanzania. Sijui ni lini uzalendo ndani ya CCM (au TANU) ulikoma, na kubadilika kuwa ufisadi, wakafanya MAAMUZI YA PAMOJA (collective responsibility) kwamba, kila uchaguzi, watumie NGUVU YA DOLA kuwaingiza mkenge wananchi.

  Lakini leo wananchi WAMEAMKA, hawana woga, wanasema waziwazi. Leo (Ijumaa) asubuhi nimewaona kwa macho yangu - wala sikusimuliwa - akinamama wakulima, tena maskini kabisa, wale ambao wanaishi kwenye maisha ya "mkono uende kinywani", hawana senti hata moja ya kuweka akiba, kila wanachozalisha kinaenda kwenye familia, kinachobaki kuzungusha mtaji, wakitamka waziwazi kwamba HAKUNA KUIPIGIA KURA CCM!

  Hawa si matajiri, hapa Moshi Mjini, wamesema kura kwao ni kwa CHADEMA. Sikuamini macho yangu, sikuamini masikio yangu, ilibidi nisogee karibu niwaone na kuwasikiliza kwa makini.

  Hawa - maskini - wanawakilisha sauti za wanawake wengi hapa nchini, ambao hakika wamechoshwa na hadaa na ghiliba za CCM. Wameamua.

  Mimi - ninayeishi jijini Dar - nilikwishaamua kabla yao, mapema, lakini sikujua kwamba wao, kwa wingi wao, walikwishaamua nao pia, bila hata ya kushawishiwa na mtu kama mimi. Wana macho, akili timamu, hawajajazwa pumba za kifisadi - kama wengine humu JF wanaowasaliti kila uchao, kama Yuda Iskarioti alivyomsaliti Yesu Kristo!

  Sasa ni zamu ya Watanzania KUIREJESHA Tanzania mikononi mwao. Sasa ni zamu ya HUKUMU TAKATIFU!

  Watanzania wameamua. CCM lazima iondoke.

  Na Wataondoka. Kura ni haki yao, kura ni siri yao, watapiga tu, hata kama CCM wataiba kura, lakini hawawezi kuiba kura nchi nzima!

  Watake wasitake, CCM wataondoka, kama walivyoondoka maswahiba zao wa zamani - KANU!

  Saa ya ushindi ni SASA!

  -> Mwana wa Haki

  2010 HATUDANGANYI-KI!
   
 14. m

  muafaka Senior Member

  #14
  Sep 4, 2010
  Joined: Oct 30, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  umetoa hoja nzuri sana na nadhani watu wengi wanauona mchango wa Dr. Slaa hasa Bungeni unapoharibu ni kujenga hoja ya kulazimisha hoja nadhani members wengi wa JF ni wapevu wa kufikiri hukuwa na haja ya kuweka kipengere hicho.

  Hata hivyo kuna suala moja ambalo limejengeka kwa watanzania wengi pamoja na wewe kuwa mtu akiwa very effective katika nafasi ya utendaji unamwondoa na kumpeleka katika nafasi ya uongozi kwa mtizamo kwamba anapata promotion. Lakini tunasahau kwamba kila mmoja ameumbwa na kipaji chake "a good performer can necessarily be a good manager". Kumpa nafasi ya uongozi wa juu huenda ni kuua kabisa mchango wake kwa Taifa, may be he can be a good minister, may be he can still be better off being a MP who knows.
   
 15. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #15
  Sep 4, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  thanks kwa ujumbe mzuri
   
 16. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #16
  Sep 4, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  thanks kaka kwa ujumbe mzuri
   
 17. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #17
  Sep 4, 2010
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Thanks reyes :a s 100:
   
Loading...