Lizaboni
JF-Expert Member
- Feb 21, 2013
- 33,894
- 20,372
Wadau, Wakati akijibu hoja za baadhi ya wabunge na taarifa ya kambi ya Upinzani, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, amesema kuwa Msafara wa Rais anaposafiri nje ya nchi unakuwa na watu wachache sana ukilinganisha nchi nyingine. Amesema kuwa Rais wa Nigeria ndiye anayesafiri na maafisa wengi sana kwani husafiri na zaidi ya maafisa 600. Aidha, amesema kuwa Rais wa Uganda anasafiri na watu 180, wa Afrika ya Kusini anasafiri na watu 92 na Rais wa Kenya anasafiri na watu 102.
Akitoa mchanganuo wa watu hao, amesema kuwa maafisa wanaosafiri kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ni wanne, maafisa 14 kutoka Idara ya Usalama wa Taifa na wengine hutokana na maeneo ambayo ziara hiyo inalenga.