Rais wa Tanzania anakuwa na msafara wa watu wachache sana anaposafiri nje ya Nchi

Lizaboni

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
33,894
20,372
Wadau, Wakati akijibu hoja za baadhi ya wabunge na taarifa ya kambi ya Upinzani, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, amesema kuwa Msafara wa Rais anaposafiri nje ya nchi unakuwa na watu wachache sana ukilinganisha nchi nyingine. Amesema kuwa Rais wa Nigeria ndiye anayesafiri na maafisa wengi sana kwani husafiri na zaidi ya maafisa 600. Aidha, amesema kuwa Rais wa Uganda anasafiri na watu 180, wa Afrika ya Kusini anasafiri na watu 92 na Rais wa Kenya anasafiri na watu 102.

Akitoa mchanganuo wa watu hao, amesema kuwa maafisa wanaosafiri kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ni wanne, maafisa 14 kutoka Idara ya Usalama wa Taifa na wengine hutokana na maeneo ambayo ziara hiyo inalenga.
 
Membe muongo , anasema kuna boko haramu, hivi Ulaya na Marekani kuna boko haram? Eti ndio maana walinzi wengi eehhhh
 
Hivi hujui kuwa Boko Haram wapo kila kona? Halafu ulivyo --------, kwani Rais Kikwete anasafiri Ulaya tu?
 
Kwahiyo ndio maana anasafiri kila siku kwavile anakuwa na msafara ya watu wachache? mfano ile safari yake ya kwenda kubembea huko jamaica alienda na watu wangapi?
 
Wadau, Wakati akijibu hoja za baadhi ya wabunge na taarifa ya kambi ya Upinzani, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, amesema kuwa Msafara wa Rais anaposafiri nje ya nchi unakuwa na watu wachache sana ukilinganisha nchi nyingine. Amesema kuwa Rais wa Nigeria ndiye anayesafiri na maafisa wengi sana kwani husafiri na zaidi ya maafisa 600. Aidha, amesema kuwa Rais wa Uganda anasafiri na watu 180, wa Afrika ya Kusini anasafiri na watu 92 na Rais wa Kenya anasafiri na watu 102.

Akitoa mchanganuo wa watu hao, amesema kuwa maafisa wanaosafiri kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ni wanne, maafisa 14 kutoka Idara ya Usalama wa Taifa na wengine hutokana na maeneo ambayo ziara hiyo inalenga.
Issue hapa ni kuwa ni nani kati ya JK na Rais Jonathan wa Nigeria ambaye misafara yake inakuwa mzigo zaidi kwa walipa kodi wa nchi yake.

Tuchukulie mathalani Rais Jonathan anafanya ziara za nje 5 tu kwa mwaka na misafara yake ya watu 600 kwa kila ziara na JK anasafiri mara 50 kwa mwaka na ujumbe wa watu 100 kwa kila ziara.

Unadhani kwa mazingira hayo ni nani kati ya JK na Rais Jonathan atakuwa anawakamua zaidi walipa kodi wa nchi yake kutokana na gharama za safari zake za nchi za nje?
 
Sasa mnataka Raisi wetu asafiri na watu wengi, hamjui kama mambo anayoenda kuyafanya ni ya siri
 
Hatutaki kujua anasafiri na watu wangapi tunalotaka kujua ni tija ya hizo safari. Inasadikika amezurura dunia hii kumzidi Vasco Da Gama.
 
Back
Top Bottom