Pape
JF-Expert Member
- Dec 11, 2008
- 5,488
- 79
Nakumbuka miaka ya enzi za utawala wa Mwl Nyerere kabla ya kumaliza muhula wake wa utawala nilisikia fununu na malumbano meeengi juu ya nani kumrithi na nikasikia ni mzee Mwinyi! Kweli ulipofika wakati wa uchaguzi Mwinyi alishika uenyekiti na hatimaye kuwa Rais.
Baada ya hapo zikaja fununu nyingi tena kwamba nani kumrithi Mwinyi. Kukawa na majina mawili kati ya Mkapa na JK. Mkongwe wa siasa Mwl Nyerere alimshauri JK asubiri yaani amwachie nafasi Mkapa kwani JK alikuwa ni mdogo kiumri kuliko Mkapa! Mwl alimwakikishia JK kwamba yeye atafuata baada ya Mkapa. Mambo yalikuwa hivyo! Kweli sikuamini masikio yangu pale nilipokuja kusikia JK ndio katangazwa mrithi wa Mkapa na hatimaye kuwa Rais.
Baada ya hapo nilidhani labda ni kwa Marais tu kumbe hata mawaziri wakuu! Wakati JK alipochaguliwa kuwa mgombea urais nikasia tetesi kwamba Lowasa piga ua lazima awe waziri mkuu...nadhani wote mlijionea nani alikuwa waziri mkuu!!
Je ni kweli kwamba viongozi wa Tanzania wanapeana nafasi madarakani kwa kulipiana fadhira?
Je, watanzania tutaendelea kuchaguliwa viongozi wetu wakuu wa nchi mpaka lini?
Ni kweli Tanzania inafuata demokrasia ya kweli au ni propaganda na kiini macho?