mechard Rwizile
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 1,571
- 873
Kimsingi hapa hakuna maswali ma3, tatizo lako ni lowassa, kifupi alimuunga mkono km alivyowahi kuumunga mkono slaa na wengine, naleewa una insinuate lowassa ni fisadi, km hujalogwa as per jpm na au una IQ yakutosha utaelewa mna mahakama ya mafisadi, mpelekeni huko kwanza b4 blaming Lissu
Mimi nilimpigia Mhe. Lowasa kura yangu kwa hiyo simtuhumu kama fisadi kama unavyodhani. Lakini ukweli ni kwamba tulishindwa. Mheshimiwa Tundu Lisu ninamuona kama tunu ya taifa na wala simungunyi maneno. Ukweli ni kwamba, mimi na wewe peke yetu sio watakao muuingiza Ikulu peke yetu; kama ambavyo watu millioni sita tulishindwa na wapiga kura millioni nane kumuingiza Mhe. Lowasa, Ikulu. Tunahitaji watu wengine watuunge mkono, hakika tunahitaji zaidi ya nusu ya watu wote watakaopiga kura. Kama tunamtaka Mhe. Tundu Lisu tunahitaji ushawishi na mikakati ya kisanyasi kabisa labda kuliko wakati mwingine wowote katika historia ya nchi hii.
Mihemko au ushabiki uliopitiliza hauna nafasi katika zama hizi. Kwanini nimekuuliza maswali hayo matatu, bado naamini ni maswali muhimu sana kwa mtu anayetaka, Mhe. Tundu Lisu aingie Ikulu, kwa maana bado kuna watu hawana uhakika kama alihongwa ndio akamuunga mkono Mhe. Lowasa au ni akili yake tu ndiyo iliyomtuma au hakumuunga mkono isipokuwa alikiunga mkono chama chetu kama mimi nilivyofanya. Hili linapashwa kujibiwa pasipo shaka.
Swali la pili na la tatu, ipo dhana kuwa Mhe. Lowasa ndiye aliyeleta wingi wa kura kwa chadema na kuwa yeye asingekuwepo tusinge kuwa na kura milioni sita na wabunge wengi wa kuchaguliwa. Hoja hii ikijibiwa kuwa ni ndiyo, itapelekea kudharau karata yetu ya UKAWA ambayo ninaamini ilivinufaisha vyama vyote vya upinzani na Mheshimiwa Lowasa hakushiriki kuibuni.
Kujiandaa kujibu maswali haya na kuweka mikakati sitahiki, Chadema kama chama na Mhe. Tundu Lisu kama mteule wetu tutajiweka katika hali nzuri. Ninakuomba utambue kuwa hata sanduku la kura ni mahakama ya aina yake.