Rais wa Syria akimbomoa mwandishi wa Marekani

Hili ndo tatizo, watu mnashabikia sababu tu anajibizana na USA huku watu wake wanakufa kila siku ilhali USA hajafa hata mmoja kwa hivyo vita vya Syria.

Ningemuona kiboko kama angenusuru roho za raia wake ila sasa huyu ni bogus.

Watu wakiisha atatawala majengo na mafuta? Sifa yake itakua nini, kwamba alipigana na USA akashinda ila wanachi wake wote waliisha na wengine kukimbia makazi yao. Hii ni sifa kweli
Marekani na washirika wake wanapoua raia wa Syria wanawatetea akina nani?
 
Sijui kwanini watu hawachoki kupigana vita,ni kwamba huwa wanalinda maslahi yao binafsi au wana uchungu na nchi zao kutoka moyoni kwahiyo wako tayari kupigana vita hata ikibidi muda wote wa maisha yao..??
 
Waandishi wa kitanzania na Viongozi wa kitanzania wana safari ndefu sana kufikia kiwango cha kufanya mahojiano yenye hadhi ya kimataifa. Bado sana.

Ni kweli kazi wanayo tena sio ndogo, maana hawa wenzetu unakuta ni mwanahabari eidha wa masuala ya kilimo lakini ana taaluma ya killimo, biashara na anataaluma hiyo, etc. akiamua kuwa mwanahabari anasoma mbinu za kiu-anahabari katika nyanja hiyo lakini tayari msingi anao, sasa hawa wa huku kwetu anakuwa mwanahabari wa michezo kwa sababu anapenda sana michezo etc. Lakini pia yawezeka tunao hata sisi wenye vigezo hivyo isipokuwa kwenye interview na big fishes wanabaki kubabaika na kujipendekeza tu.
 
This was very interesting, Assad is a genius, very logical answers! The interviewer was really left in disbelief!

Tatizo naloliona hapo, kama waandishi wengine tu, huwa wanaenda kumhoji mtu wakijua wao ndio wako ktk driving seat, ukimgeizia kibao tu hajielewei.
Ona sasa mmarekani hapo hajapata hata jibu moja alilolitaka.
 
Unapoa tuhuma, unatakiwa utoe ushahidi wa kuthibitisha tuhuma, hiyo ndo hoja ya Assad, kisheria yuko sahihi. Mwandishi kamjazia maelezo ya kusikia na picha za kutengeneza. Those are not evidences are just documents...! You have to know that "not every document is an evidence"
Aisee! Mwandishi ametuhumu au alikuwa anasoma report ya Amnesty international! BTW tatizo hapo sio ushahidi, ni wazi kabisa majibu ya Assad ni sawa na kusema "SITAKI KUJIBU", manake huwezi kutoa the so called" concrete evidence "pale studio!

Kumbuka ile session ni TV show sio COURT PROSECUTION kiasi cha kuhitaji examination of witness au evidence!

Unashangaa Mwandishi kutumia maelezo ya kusikia? Unafananisha Mwandishi na shahidi au vipi! Mwandishi ana privilege ya kutumia hearsay ndio maana ana haki ya kuficha his/her source!
 
Assad ana uwezo wa kupambanua mambo kwa haraka sana na kuyatolea maamuzi kwa namna anavyojibu asingekua makini ni dhahiri angejikanyaga, Mwandishi nae anaonekana kabisa yupo kwa kumbana zaidi na jamaa alimsoma mapemaa.Safi sana.
 
Western propaganda mbaya sana wanaweza kukuchafua wanaweza kukukweza... Assad akomae tu yasije tokea ka yaliyotokea Libya
 
Aisee! Mwandishi ametuhumu au alikuwa anasoma report ya Amnesty international! BTW tatizo hapo sio ushahidi, ni wazi kabisa majibu ya Assad ni sawa na kusema "SITAKI KUJIBU", manake huwezi kutoa the so called" concrete evidence "pale studio!

Kumbuka ile session ni TV show sio COURT PROSECUTION kiasi cha kuhitaji examination of witness au evidence!

Unashangaa Mwandishi kutumia maelezo ya kusikia? Unafananisha Mwandishi na shahidi au vipi! Mwandishi ana privilege ya kutumia hearsay ndio maana ana haki ya kuficha his/her source!
Sasa hizo picha kwa mfano, mbona alipoulizwa na Assad hao ni nani na unathibitisha vipi ndio hao anaodai, mwandishi kabaki mdomo wazi. Ukweli ni kwamba mwandishi alienda kwa lengo moja tu la kumbana Assad ila kachemka.
 
hapa swali la msingi ni kwa nini USA na western countries wanawasapoti magaidi kule syria? ili wamtoe assad na assad akitoka wenyewe wanapata faida gani?,
 
Sasa hizo picha kwa mfano, mbona alipoulizwa na Assad hao ni nani na unathibitisha vipi ndio hao anaodai, mwandishi kabaki mdomo wazi. Ukweli ni kwamba mwandishi alienda kwa lengo moja tu la kumbana Assad ila kachemka.
Rudia tena kuangalia ujue ni nani aliomba ushahidi wa picha!

Assad ni forensic expert?
Wewe unaemshabikia unajuaje kama kweli picha zile sio halisi?
 
Rudia tena kuangalia ujue ni nani aliomba ushahidi wa picha!

Assad ni forensic expert?
Wewe unaemshabikia unajuaje kama kweli picha zile sio halisi?
Kijana ebu tuliza mzuka! Wewe ulitaka Assad akubali kuwa hizo picha ni za kweli kisa kaonyeshwa na huyo mwandishi??
Wewe unajiridhisha vipi kuwa hizo picha zimefanyiwa forensics/ picha za kweli?? Huyo mwandishi kwako ni forensic expert wa picha??
Hata mimi ningekuwa Assad huwezi ukaniletwa tu picha mtu anateswa kisha uniambie ni picha ya mtu ndani ya nchi ya Syria.
 
Tatizo la wabongo wengi

Tatizo la wabongo wengi mnajua sana! Hivi mwandishi ndio anatakiwa atoe ushahidi kweli au mwandishi anatakiwa ku raise doubt kisha anayehojiwa ndio afanye clearance to such doubt!
 
Back
Top Bottom