Rais wa Sudan kufunguliwa Mashtaka.

Indume Yene

Platinum Member
Mar 17, 2008
2,944
700
Rais wa serikali ya Sudan Omar Hassan Al-Bashir anategemea kufunguliwa mashitaka ya Mauaji ya Kimbari Darfur.

Mwendesha Mashtaka Mkuu (Luis Moreno-Ocampo - toka Argentina) katika Mahakama ya Kimataifa inayoshughulikia kesi hiyo anategemea ku-issue International Warrant dhidi ya kiongozi wa Sudan aidha jumatatu au jumanne. Hata hivyo habari hiyo imewaudhi sana viongozi wa Sudan na kudai kuwa warrant hiyo au utaratibu wowote wa kumfikisha kiongozi wao utasababisha ghasia zaidi katika ukanda huo. Hata hivyo inaonekana hiyo warrant itawahusu vilevile viongozi wengine zaidi wa ngazi ya juu katika serikali ya Sudani.
Tusubiri tuone nini kitatokea baada ya Search Warrant kutolewa.

Habari hii inaweza kupatikana katika vyombo vya habari mbalimbali kama vile CNN, Washingtonpost etc.


Naomba habari hii ifutwe maana nimeona nyingine the same as this. (OMBI)
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom