Rais wa Sudan Akoswa koswa na Kiatu Rais wa Sudan, Omar Al-Bashir

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,080
3975538.jpg

Rais wa Sudan, Omar Al-Bashir Tuesday, January 26, 2010 5:41 AM
Baada ya George Bush na waziri mkuu wa China kukoswa koswa na viatu, zamu ya kurushiwa kiatu imemuangikia rais wa Sudan, Omar Al-Bashir ambaye alikoswa koswa na kiatu kilichoruswa na mwananchi wake mwenyewe mbele ya wageni wake waalikwa. Mwanaume mmoja raia wa Sudan ametiwa mbaroni baada ya kumkosa kosa na kiatu rais wa Sudan, Omar Al-Bashir.

Mwanaume huyo ambaye jina lake halikutajwa alitiwa mbaroni dakika chache baada ya kumrushia kiatu rais Omar Al-Bashir ambaye aliandaa hafla ya kujadili uchumi wa Sudan na kuwaalika wageni mbali mbali.

Mashuhuda wa tukio hilo ambao hawakutaka kutaja majina yao, walisema kuwa mwanaume ambaye anakadiriwa kuwa na umri wa miaka 50, alisombwa msobe msobe na walinzi wa rais Al-Bashir baada ya kiatu alichomrushia kumkosa.

Mwanaume huyo hakuelezea sababu ya kumrushia kiatu rais huyo ambaye ameitawala Sudan tangia mwaka 1989 alipoipindua serikali iliyokuwepo madarakani wakati huo.

Kwa mara ya kwanza katika historia, Sudan itafanya uchaguzi wake mkuu wa kwanza mwezi wa nne mwaka huu na rais Al-Bashir ni miongoni mwa wagombea akiwania kurudi tena madarakani.

Rais Al-Bashir yuko kwenye listi ya watu wanaotafutwa na mahakama ya kimataifa ya makosa ya jinai ambapo anatuhumiwa kufanya uhalifu wa kivita kwenye maeneo ya Darfur.

Rais al-Bashir sio kiongozi wa kwanza wa kisiasa kurushiwa kiatu, mwezi disemba mwaka 2008 mtangazaji wa televisheni ya Iraq, Muntazer al-Zaidi alimrushia kiatu rais wa zamani wa Marekani George W. Bush na kupelekea atupwe jela miezi tisa.

Waziri mkuu wa China, Wen Jiabao naye alirushiwa kiatu wakati wa mkutano wake na wanafunzi wa chuo kikuu nchini Uingereza.

Kurushiwa kiatu au kuonyeshwa soli ya kiatu ni tukio la kuonyeshwa dharau kwa mujibu wa tamaduni za kiarabu.





http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3975538&&Cat=2
 
Back
Top Bottom