Rais Mohamed Abdullahi Farmajo wa Somalia ametangaza janga la njaa lililoikumba nchi hiyo ya Pembe ya Afrika kuwa ni maafa ya taifa.
Katika taarifa iliyotolewa jana na Ikulu ya Somalia, Rais Farmajo amesema, kuna wajibu wa kuchukuliwa hatua za dharura za kibinadamu katika maeneo yote yaliyoathiriwa na ukame.
Aidha Rais wa Somalia ameitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua za haraka za kuzisaidia familia na watu walioathiriwa na ukame ili kuepusha kutokea janga jingine la kibinadamu.
Rais Mohamed Abdullahi Farmajo wa Somalia
Mashirika ya misaada ya kibinadamu yamesema kuwa, ukame umepelekea watu wapatao milioni tatu kukumbwa na mgogoro katika maeneo mbalimbali ya Somalia.
Nchi hiyo hivi sasa imekaribia kuingia kwenye janga kubwa zaidi la ukame katika kipindi cha miaka 25 iliyopita.
Siku ya Jumatatu, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitahadharisha kuhusu kutokea maafa na ukame mwingine mkubwa kama ule wa mwaka 2011 uliopelekea watu 260,000 kupoteza maisha yao.
Shirika hilo limesema, zaidi ya watu milioni 6.2 wanahitajia msaada wa haraka ambapo watu milioni tatu kati yao wanaishi katika mazingira ya njaa hivi sasa.
Mwanamke na mtoto wakipita mbele ya mifugo iliyopoteza maisha kwa ukame nchini Somalia
Kwa mujibu wa WHO, zaidi ya watoto 363,000 wanateseka kwa kiwango kikubwa cha lishe duni na karibu 70,000 wana lishe duni ya wastani na wote wanahitajia misaada ya haraka ya kuokoa maisha yao.
Zaidi ya hayo, watu wa maeneo mengine ya Somalia wanateseka na magonjwa mbalimbali kama vile kipindupindu na kuharisha. Watu wapatao milioni 5.5 wa Somalia wana hatari ya kukumbwa na magonjwa yatokanayo na maji yasiyo salama.