Rais wa sita Mhe. Samia Suluhu atakuja na kauli mbiu yake au ataendeleza kauli mbiu ya Hayati Magufuli ya "Hapa kazi tu"?

Apr 1, 2019
96
135
Ni kawaida kila Rais mpya anapoingia madarakani kuja na kauli mbiu au falsafa yake.

Kauli mbiu hizi au falsafa ndio huonyesha dira au mwelekeo wa serikali inayokuwepo madarakani katika kuleta maendeleo kwa wananchi na taifa kwa ujumla.

Katika awamu ya kwanza chini ya utawala wa hayati Julius nyerere yeye alikuja na kauli mbiu ya ujamaa na kujitegemea. Falsafa hii ilikusudia kutokomeza unyonyaji katika nyanja zote ili kila mtu anufaike na rasrimali tulizonazo na taifa kujitegemea kiuchumi pasipo utegemezi wa misaada toka nje.

Baada ya Nyerere alikuja mzee Ally hassan Mwinyi. Katika kipindi chake alikuja na kauli mbiu ya ''Ruksa'' ambayo ililenga kutoa ruksa kwa kila mtu kufanya chochote akitakacho pasipo kuvunja sheria, kanuni na taratibu za nchi.

Baadaye akaja Hayati Benjamin Mkapa na kauli mbiu ya ukweli na uwazi. Kauli mbiu ambayo ililenga kupambana na vitendo vya ufisadi, rushwa na uzembe serikalini kwa kuimarisha ufanisi, uwazi na uwajibikaji serikalini.

Baada ya mkapa akaja mzee Jakaya. Yeye alikuja na kauli mbiu ya maisha bora kwa kila mtanzania ambayo ililenga kuinua watu kiuchumi na kuwafanya wawe na maisha mazuri(bora).

Ndipo akaja marehemu Magufuli na kauli mbiu ya ''hapa kazi tu''. Ambayo ililenga kuhimiza watu kufanya kazi kwa bidii ili kuinua uchumi wa nchi.

Sasa tunaye mama Samia suluhu ambaye ni Rais wa sita. Je atakuja na falsafa yake au ataendelea kuishi katika falsafa ya magufuli ya hapa kazi tu?

Binafsi nashauri mama Samia aje na kauli mbiu yake ambayo imefanyiwa tafiti mbali mbali kujua matatizo na changamoto tulizopitia watanzania katika miaka mitano iliyopita kwa lengo la kuzitatua au kuzipatia suluhu kama jina lake.

Nachelea kusema hivi kwa sababu kauli mbiu ya "hapa kazi tu" ni kauli mbiu ya hovyo kuwahi kutokea sababu ina hamasisha watu kufanya kazi wakati kazi zenyewe hazionekani huku fursa za kufanya kazi serikalini zikiwa zimepunguzwa au kubanwa kabisa, hivyo kauli mbiu hii imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kutengeneza jobless graduates wengi isivyo kawaida.
 
Mimi ningetamani aje na kauli mbiu ya "Mama ni nguzo ya familia"! Kupitia kauli mbiu hiyo, atuunganishe kwanza Watanzania na kuwa tena kitu kimoja kama ilivyokuwa enzi za Mwalimu!

Kiukweli kwa sasa tumegawanyika sana! Na kifo cha mtangulizi wake, ni ushahidi tosha.
 
Amesema ataendelea na Hapa Kazi tu which sio mbaya amalizie miradi waliyoiweka kwenye ilani ya chama Chao page 303
 
Mama Samia naamini Mungu amemleta kwetu kuleta umoja wa kitaifa ambao ulikuwa umeparanganyika.
1.Mama Samia futa ukanda na ukabila uliojengwa na mtangulizi wako.
2.Jenga umoja wa Kitaifa kwa kuwarudisha wote walio nje ili tuwe kitu kimoja.
3. Rudisha demokrasia iliyokuwepo kipindi cha Kikwete na sio vinginevyo (japo najua kina wajinga watakupinga ndani ya ccm)
4. Tume huru ya uchaguzi nayo ni muhimu sana sana ili maoni na uhuru wa wananchi wa kuchagua uheshimiwe.
5. Panga safu yako mpya ya baraza la mawaziri na watendaji wengine au wale kiapo upya cha utii kwako.

NB: Nikitakie kazi njema sana na Allah akutangulie, ILA tuna imani kubwa sana sana nawe.
 
Hatimaye madam president kaliweka hili sawa kwamba ni awamu ya sita kwa minajiri hiyo "hapa kazi tu" ni kauli mbiu ya awamu ya tano, je kauli mbiu ya wamu ya sita ni ipi?
 
Ya kwake itakuwa: Wajibu, Haki, Upendo na Amani kwa wote. Naomba aichukue hii.
 
Hatimaye madam president kaliweka hili sawa kwamba ni awamu ya sita kwa minajiri hiyo "hapa kazi tu" ni kauli mbiu ya awamu ya tano, je kauli mbiu ya wamu ya sita ni ipi?
Amesema "Zege Halilali" hiyo ni kauli tosha kwa serikali isiolaza damu?
 
Back
Top Bottom