Rais wa Rwanda, Paul Kagame kufanya ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,888
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Taarifa kuhusu ziara ya Mhe. Paul Kagame, Rais wa Jamhuri ya Rwanda

Mhe. Paul Kagame, Rais wa Jamhuri ya Rwanda na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, atawasili nchini tarehe 7 Machi 2019 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Ziara hiyo inafanyika kufuatia mwaliko wa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ziara hii itatoa fursa kwa viongozi hao wawili kujadiliana masuala mbalimbali kuhusu uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizi mbili. Aidha, Viongozi hao wanatarajia kuzungumzia masuala mbalimbali ya mtangamano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mhe. Kagame, Rais wa Jamhuri ya Rwanda, atawasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa Tisa Alasiri tarehe 7 Machi 2019 na kupokelewa na mwenyeji wake, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhe. Rais Kagame anatarajia kuondoka nchini tarehe 8 Machi, 2019.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,

Dodoma.

6 Machi 2019
 
Mhe. Paul Kagame, Rais wa Jamhuri ya Rwanda na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, atawasili nchini tarehe 7 Machi 2019 kwa ziara ya kikazi ya siku mbili. Ziara hiyo inafanyika kufuatia mwaliko wa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Ziara hii itatoa fursa kwa viongozi hao wawili kujadiliana masuala mbalimbali kuhusu uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizi mbili. Aidha, Viongozi hao wanatarajia kuzungumzia masuala mbalimbali ya mtangamano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.Mhe. Kagame, Rais wa Jamhuri ya Rwanda, atawasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere saa Tisa Alasiri tarehe 7 Machi 2019 na kupokelewa na mwenyeji wake, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mhe. Rais Kagame anatarajia kuondoka nchini tarehe 8 Machi, 2019.
7.JPG
 
Attachments

  • 7.JPG
    7.JPG
    17.9 KB · Views: 61
Jana alikua S/Africa akihudhuria Young Presidents' Organisation(YPO) Summit,nadhani amekuja kumwambia mzee baba jiandaeni tunataka kuitumia central corridor ipasavyo bidhaa zote zitapita hapa kule border ya Uganda tumepiga chini.

Vp lkn barabara za kwenda Rusumo ziko fresh mzee baba?Maana yule waziri wa Mambo ya nje ya Rwanda alisema wanacheki Route ya Central Corridor kupitishia bidhaa zao.

That's my guess.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ziara hii itatoa fursa kwa viongozi hao wawili kujadiliana masuala mbalimbali kuhusu uhusiano na ushirikiano baina ya nchi hizi mbili. Aidha, Viongozi hao wanatarajia kuzungumzia masuala mbalimbali ya mtangamano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Ushirikiano na Utangamano na Mahusiano is bullshit!

KAGAME anataka Magu aongee na MU7 kuhusu waasi ambao anaamini wanasaidiwa na Uganda.

MAGU anataka Kagame ampe tena somo kwa nini blueprint yake ya kufufua ATCL imekuwa a devastating disaster, ndege zinarusha abiria watatu.

1551911774371.png
 
View attachment 1039838

Acha kudangaya watu juzi juzi nimeruka na Dreamliner ilikuwa full house unasema abiria watatu?
 
Ushirikiano na Utangamano na Mahusiano is bullshit!

KAGAME anataka Magu aongee na MU7 kuhusu waasi ambao anaamini wanasaidiwa na Uganda.

MAGU anataka Kagame ampe tena somo kwa nini blueprint yake ya kufufua ATCL imekuwa a devastating disaster, ndege zinarusha abiria watatu.

View attachment 1039838
acha ujinga na ushamba hapo ndege haijaanza kuondoka ndo kwanza abiria wanaingia
 
acha ujinga na ushamba hapo ndege haijaanza kuondoka ndo kwanza abiria wanaingia
Hapo abiria wanaingilia wapi mkuu.?
Inamaana kule nyuma hakuna mlango.?
Na wa huku mbele wamekubali masanja awazuie.?
Hao waliokaa walikuja na ndege toka ilipotoka.?

Umewahi kupanda ndege na ukaona utaratibu wa kuingia.??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom