Kunguru Mjanja
JF-Expert Member
- Aug 22, 2012
- 2,036
- 3,929
Kiongozi wa Russia Vladimir Putin, akiwa anaongea kwenye mkutano wa 'Brics group' (Brazil, Russia, India, China and South Africa) uliofanyika Xiamen, China, amesema kuendelea kutaka kuiwekea vikwazo vipya North Korea ni sawa na kazi bure, pia amesema "North Korea watakula hata nyasi, kuliko kuachana na mpango wao wa nuclear."
Licha ya Putin kuishutumu North Korea, alisema kuwa vikwazo havitasaidia.
Marekani walisema siku ya Jumatatu kwamba wataweka mezani azimio jipya la UN juu ya vikwazo vigumu zaidi dhidi ya North Korea, kufuatia jaribio lao jipya la nuclear la jumapili.
Bwana Putin pia alisema kuwa hatua za kijeshi inaweza kuleta janga la dunia nzima.
Putin amesema kuwa mazungumzo ya diplomasia ndio njia pekee.
Kiongozi wa Ujerumani Angela Merkel, alikubaliana na mpango huo wa kuongeza vikwazo zaidi kwa North Korea siku ya Jumanne na kusema kwamba vikwazo hivyo vinahitajika mara moja ili kukabiliana na North Korea kuvunja mkataba na maazimio ya wazi ya kimataifa.