Rais wa nchi yupo kwa ajili ya Watanzania. Anaposema ataongea na Wazee wa Dar es Salaam huu ni ubaguzi usio na tija

elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
8,975
2,000
Siasa za makaburu hazina nafasi Tanzania, Rais wa nchi yupo kwa ajili ya watanzania wote na anaposema ataongea na wazee wa Dar es Salaam kisha Mkuu wa Mkoa anawatambulisha wazee wa CCM kwa Rais huu ni ubaguzi usio na tija kwa taifa.

Tumekuwa tukishuhudia wazee wa CCM wakipewa upendeleo wa kadi za matibabu huku wengine wasio wa CCM wakiachwa.

Tanzania ni yetu wote na itasonga mbele haraka endapo CCM itaachana na tabia mbaya ya ubaguzi ambao hata makaburu waliuona hauna tija kwenye dunia ya wastaarabu.
 

denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
5,654
2,000
Jamaa naona wana copy & paste kila alichofanya Nyerere, hao wazee wa CCM hawawezi kamwe kuwa wazee wa DSM, wajue hizi ni zama za vyama vingi sio enzi ya TANU.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom