RAIS WA NCHI YA ZANZIBAR SAFI UTURUKI, Hamna kutaja TANZANIA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

RAIS WA NCHI YA ZANZIBAR SAFI UTURUKI, Hamna kutaja TANZANIA

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Pharaoh, May 3, 2011.

 1. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #1
  May 3, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Rais wa nchi ya Zanzibar mambo mazuri Uturuki, asije akaomba na silaha, kwa heshma kubwa kwa Uturuki, tunaijuwa nguvu yake kijeshi na kiuchumi, hata Israel inabembeleza ipate urafiki na Uturuki, Rais Gul na Shein wameongelea mengi na kupanga mengi, Rais wa Zanzibar amejitahidi kutotaja popote pale jina la Tanzania, hapa amekosea, Afrika mashariki anaitaja, mbona huyu JK wetu haongei popote asiitaje Z?
  fuatilieni kwenye google halafu maoni?
   
 2. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Safi sana mwanzo mzuri huo wa kujivua mnyororo wa muungano...viva Shein!
   
 3. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Let me see
   
 4. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  :happy:

  For me, in the other extreme, Shain is right maana huyu ni Raisi wa Zanzibar na sio wa Muungano

  Hajachaguliwa kupigania maslahi ya Muungano wala kusimamia "Mambo ya Muungano" bali mambo yanayohusu Zanzibar.....so mi naona ni sahihi kabisa kutokutaja kwake

  Kuhusu Kikwete kuitaja Znz ni sahihi kwa sababu ipo ndani ya eneo lake la utawala (Kumbuka yeye ni Raisi wa Jamhuri ya Muungano wakati Shain ni wa Zanzibar)
   
 5. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,804
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Sijaelewa ni kitu gani unasifia au unapongeza! Kama tutaanza kupongezana wakati tunatimiza wajibu wetu hatuwezi kufika mbali, be it Zanzibar or Tanganyika.. be it a messenger or a PS!
   
 6. N

  Nonda JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,960
  Trophy Points: 280
  “Kwa kweli hata kesho Nchi za Afrika ya Mashariki zikiamua kuungana, na Tanzania ikawa ni mshiriki, naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikisha Tanzania yenye Serikali Mbili - ya Zanzibar na ya Tanganyika - kuliko Tanzania yenye Serikali Mbili, ya Tanzania na ya Zanzibar. Wapendao Utanganyika watakuwa wazalendo zaidi, badala ya kuwa wasaliti, wakiazimia Afrika ya Mashariki iliyoungana kuwa Nchi Moja. kuliko Tanzania iliyotengana ikawa nchi mbili.” Nyerere.


  Soma ukurasa wa 10-12 Uongozi Wetu Na Hatma Ya Tanzania (by Nyerere)


  EAC ipo? Nia ya kuwa na shirikisho la Afrika Mashariki ipo? Wamesema wana-fast track, au vipi?

  Jiulize masuali, majibu tulishapewa tokea 1990s
   
 7. S

  Sio Mwanasiasa Senior Member

  #7
  May 7, 2011
  Joined: Mar 4, 2011
  Messages: 115
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  nimekusoma great thinker wa ukweli..hii mada nyepesi na umeimaliza kwa jibu lenye usahihi kabisa..labda kama mtu atataka kubisha tu
   
 8. Hute

  Hute JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,062
  Likes Received: 3,927
  Trophy Points: 280
  utumbo mtupu, tena utumbo wa nguruwe huu. au wa kuku. ule unaouzwa vilabu vya tandale kwa mfuga mbwa etc. anafurahia kujivua zenji, kwa faida gani? nyie wazenji mliolegea viuno ombeni Mungu muendelee kuwepo ndani ya Tanzania, kwasababu bile hilo, mtakula jeuri yetu.

  kwa habari ya Uturuki/Turkey, mwandishi wa mada hii ni mpungufu wa akili za shule sana. Israel hata siku moja haijajibembeleza kwa Turkey, wala haiiogopi Turkey. uwezo wa uturuki kivita ni mdogo sana ukilinganisha kuwa wanayo population ya watu kama milion sabini. wamechachafwa na wagiriki kwenye ule mgogowa wa cyprus hadi wamefyata mkia...maisha yao bado ni masikini sana hadi wanashindwa kuingia umoja wa ulaya. waturuki walio wengi wamezamia ulaya, ujerumani wamejaa kutafuta kazi, nchi nyingi za ulaya wamejaaa, nimesoma nao wengi pia...life lao bado chafu tu na sio watu wa muhimu sana kwa tz wala zanzibar kiuchumi wala silaha kwasababu hata silaha wanategemea toka sehemu zingine....ingia kwenye net uone GDP yao, halafu ndo upanue domo lako....

  kuhusu shein, sisi watanganyika, hata kama wazenji mtajitoa, hatuna hasara, zaidi sana tunayo faida kwasababu tutakuwa tumepunguziwa mzigo, yaangu gunia tulilokuwa tunalibeba kwa muda mrefu sana kwa huruma na kuwabembeleza kama mtoto anayenyonya au kama mke mrembo...kama mkitoka, hatutafurahi kwasababu tuliwapenda, lakini hata hivyo hatutapata hasara sana. pole kwa fikra mbovu.
   
Loading...