Rais wa Nchi si sawa na baba wa Familia!

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,113
33,623
Kuna dhana inajegwa kwa kasi sana kwamba Rais wa nchi yetu ni sawa na baba wa familia kwa ivo ni lazima aungwe mkono na ni kosa kukosolewa. Dhana hii ambayo inajengwa sana na wana CCM ilishawahi kujengwa huko zamani ikihusishwa na "ubaba" wa CCM kwa watanzania hadi ule wimbo wa "CCM ndiye baba..." ukatungwa.

Baba wa familia ni tukio lisilopangwa wala hakuna mtu anayeomba kuwa na baba wa aina fulani. Mtu akiwa na baba wa hovyo anamvumilia si kwa sababu anamkubali bali kwa kuwa haiwezekani kubadili baba. Lakini rais wa nchi ni mwanasiasa ambaye huchaguliwa (hata kama kuna hitilafu kwenye kuchaguliwa kwake) ili afanye kazi mahsusi kwa ajili ya wananchi waliomchagua.

Wakati baba wa familia hakuna Katiba inayomuongoza, rais wa nchi kuna Katiba inayomuongoza na yeye huwa hayuko juu ya katiba hiyo na ni LAZIMA aifuate. Baba ni mambo ya kibailojia ambayo hakuna mtu anayeweza kuchagua azaliwe na baba wa ina gani. Lakini Rais wa nchi ni kiongozi wa kisiasa tu na watu wana hiyari ya kumkubali ama kumkataa!
 
Malaika huwa lazma aungwe mkono hata kma hana sifa za kua malaika,
Malaika yeye siku zote huwa yuko sahihi kwenye kila jambo hata kma baya lazma mshangilie
 
Back
Top Bottom