Kinyungu
JF-Expert Member
- Apr 6, 2008
- 17,369
- 33,011
Nimemsikiliza rais Jakaya Kikwete (JK) jana na hotuba yake ya kujibaraguza mbele ya Watanzania. Sikutegemea jipya kwenye story zake za jana na wale Wazee wa vijiwe vya CCM ila hili la yeye kama rais wa nchi kudharau sarafu ya nchi yake mwenyewe hadharani limenisikitisha sana.
Ni ajabu sana kwa rais wa nchi kwenda mbele ya vyombo vya habari kukiwa na halaiki ya watu na kuiita bila haya wala aibu sarafu ya nchi kwa jina la kebehi kuwa eti ni "hela ya madafu" halafu anaachwa tu hakuna kitakachompata. Hii ni fedheha na dharau ya hali ya juu kwa sisi ambao hela hiyo ya 'madafu' ndio mshahara wetu na fedha yetu ya kufanya biashara kila siku.
Tunajua mmeiba sana na tena mkishaiba chap chap mnazibadilisha kuwa dollar hivyo haya "madafu" hata yawe sawa na toilet paper (karatasi za kuchambia) kwenu sio issue. Itakuwa ajabu sana kama nikimsikia tena waziri wa fedha na uchumi akisisitiza wafanyabiashara hasa Wahindi ambao wanajua sana umuhimu wa dhamani ya fedha wasiuze bidhaa zao kwa dollar maana hela wanayoambiwa watumie hata mkuu wa nchi anaiona haina maana yoyote zaidi ya kuwaweza kununulia tunda la bei duni la aina ya madafu.
Rais anatakiwa aelewe kuwa kauli zake za namna hii tena anazozitoa hadharani zina madhara ya moja kwa moja kwa uchumi wetu na achunge sana kauli zake anapozungumza masuala muhimu ya nchi hadharani. Kama ni kutudharau kesha fanya hivo sana lakini atuache basi na hii sarafu yetu ambayo kila kukicha anafanya mbinu za kuishusha dhamani. Kudharau sarafu ya nchi hadharani tena mchana kweupe na mtoa dharau akiwa ndie rais wa nchi inatakiwa liwe kosa la uhujumu uchumi na JK anapaswa kushitakiwa kwa hili.
Tumekuvumilia kwa mengi JK lakini kwa kuifananisha sarafu yetu na madafu umevuka mipaka. Bora ungeiita hivyo ukiwa chumbani kwako au ukisha acha nafasi yako ya urais. Ni kwa sababu unaongoza nchi yenye mifumo mibovu ya sheria inayokulinda laiti ingelikuwa nchi nyingine kauli yako hiyo ingetosha wewe kujiuzulu ukachunge mbuzi wako kule Msoga.
Mwana JF hebu piga picha nini kitampata rais Baraka Obama wa Marekani kama siku atakwenda hadharani kukiwa na vyomba vya habari na kutamka maneno ya dhihaka kwa dollar kama alivyofanya rais Jakaya Kikwete jana pale ukumbi wa Diamond Jubilee. Jibu nadhani unalo mwenyewe mwana Jf.
Wasalaam,
Kinyungu.