Rais wa nchi anaongozwa na Katiba- Padre P. Karugendo, Tanzania Daima, 12.9 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais wa nchi anaongozwa na Katiba- Padre P. Karugendo, Tanzania Daima, 12.9

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dopas, Sep 12, 2010.

 1. D

  Dopas JF-Expert Member

  #1
  Sep 12, 2010
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  WanaJF nimeona niwaletee makala haya kutoka Tanzania Daima.

  HAYATI Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alisema kwamba hatuwezi kumpata rais malaika, maana sote ni binadamu. Anayechaguliwa kuwa rais ni Mtanzania mwenzetu, ni binadamu kama binadamu wengine, atakuwa na upungufu wa kila aina.

  Alitutaka tuzingatie na kuhoji uwezo wake wa kuongoza, ana akili timamu, ni mzalendo, amesoma na ana uelewa wa mambo ya kitaifa na kimataifa. Na kwamba kwa vile kuna Katiba hakuna wasi wasi wa kumtafuta rais miongoni mwetu.

  Alisema ni lazima rais, aifahamu katiba, na aape kuilinda na kuitetea. Asipofanya hivyo tunamjua ni msaliti. Hivyo tunapoelekea uchaguzi mkuu ni lazima tuwachambue wagombea wa urais kwa misingi hiyo.

  Vyombo vya habari vifanye uchunguzi ni nani kati ya wagombea anaifahamu katiba yetu na yuko tayari kuilinda na kuitetea. Nyongeza ha haya, si muhimu sana; ana wanawake wangapi, ana watoto wangapi, ana vimada wangapi au labda hakuoa kabisa hayana mchango wa kumpata rais bora na mwaminifu kwa nchi yake.

  Wagombea wetu wote ni watu wazima. Wengine wamefanya kazi serikalini na wengine walikuwa kwenye Bunge letu tukufu. Hivyo tunaweza kuwapima katika miaka yao hii ndani ya taifa letu, ni kiasi gani wameilinda katiba yetu na kuitetea.

  Matendo yao ya kila siku yameheshimu Katiba yetu? Kama walishindwa kuiheshimu Katiba yetu siku za nyuma, itakuwa ni ndoto kuiheshimu wakiwa madarakani.

  Mbali na Katiba, Mwalimu alitukumbusha kwamba Rais, wetu ni lazima ayafahamu matatizo ya taifa letu na yamguse. Je, wagombea wetu wa Urais wanaguswa na matatizo ya Watanzania. Na je, kwa miaka ya nyuma wamejishughulisha na matatizo ya Watanzania? Wamejaribu kutoa michango ya mawazo na nguvu zao kuyaondoa matatizo hayo?

  Mfano, tuna tatizo la maji: Mijini na vijijini. Kati ya wagombea wetu wa urais, ni yupi amejitahidi kujielekeza kwenye tatizo hili – sehemu yoyote ya Tanzania. Tuna tatizo la barabara za vijijini hata mijini, lakini tatizo kubwa ni vijijini maana wakulima wanashindwa kusafirisha mazao yao kwenda kwenye soko.

  Sasa hivi tunahimiza kilimo kwanza, ni kiasi gani juhudi zimewekwa kuboresha barabara za vijijini ili kilimo kwanza kiende sambamba na kusafirisha mazao kutoka vijijini kwenda kwenye soko.

  Kati ya wagombea wetu wa urais ni yupi analiongelea hili kwa ufasaha bila ushabiki na ujinga wa kutaka kuwafanya watu wote ni wajinga.

  Elimu bado ni tatizo. Hatuna walimu wa kutosha, hatuna madarasa ya kutosha, hatuna vitabu vya kutosha, hatuna madawati ya kutosha, hatuna vyuo vikuu vya kutosha, hatuna vyuo vya ufundi vya kutosha, hatuna fedha za kutosha kuwasomesha watoto wetu. Ni mgombea yupi anakuja na neema ya kupunguza makali haya ya elimu?

  Akina mama wanakufa wakati wa kujifungua; tatizo ni huduma za hospitali kuwa mbali, lakini pia na tatizo la usafiri. Wagombea wa urais wanaliona hili? Watanzania wana haki ya kuwauliza swali katika mdahalo. Ni vipi tatizo hili litatafutiwa ufumbuzi wa haraka.

  Malaria ni ugonjwa unaoyapoteza maisha ya Watanzania na hasa watoto walio chini ya miaka mitano. Ni mgombea yupi ataweza kuendesha kampeni ya kutokomeza mbu. Hili pia ni swali na kuwauliza wagombea wetu na vyombo vya habari vingesaidia namna ya watu kuuliza maswali haya.

  Nchi yetu ina madini, ardhi kubwa, mito na rasilimali nyingine nyingi. Ni kwa vipi tunaendelea kuwa masikini? Ni mgombea yupi ana sera nzuri ya kutuwezesha kuondokana na umasikini? Tuwapime wagombea wetu kwa kuwauliza maswali juu ya uchumi wa taifa letu.

  Kama alivyoshauri Mwalimu Nyerere, hatutegemei rais wetu kushauriwa na mke wake au mume wake juu ya kuliongoza taifa. Bila kupuuzia umuhimu wa maisha ya ndoa, hatutegemei maisha ya binafsi ya mgombea yawe ya msingi katika kuliongoza taifa letu.

  Inaweza kutokea tukaongozwa na Rais asiyekuwa na mume wala mke. Hatutegemei rais wetu kushauriwa na familia, marafiki na maswahiba wake juu ya kuliongoza taifa.

  Hawa wanaweza kutoa mchango wao kama Watanzania wengine, lakini la kufahamu na kuzingatia ni kwamba rais anaongozwa na Katiba ya nchi.

  Pamoja na kuongozwa na Katiba, mgombea ambaye ana historia ya wizi hawezi kutufaa kuliongoza taifa letu. Tunategemea vyombo vya habari kutusaidia kuyafunua mambo kama haya. Mgombea ambaye ameshiriki mauaji, magendo ya hatari kama vile kuuza dawa za kulevya hawezi kutufaa kuliongoza taifa letu.

  Mgombea ambaye ni fisadi na ametumia rasilimali za taifa kujinufaisha yeye na familia yake, jamaa zake, marafiki zake na kabila lake, hawezi kutufaa kuliendesha taifa letu.

  Dunia nzima itatushangaa, tukishindwa kuyauliza haya na kugeukia sura, kula, kulala na kwenda ****** kwa wagombea wetu wa urais, maana hayo niliyoyataja ndio wanaulizwa marais wote wanaotaka kuziongoza nchi zao.

  Viongozi wa kampeni za wagombea Urais wa vyama vyote ni watu wasomi na kusema kweli ni watu wanaoheshimika katika jamii yetu. Baadhi yao mimi binafsi ninawaheshimu sana.

  Inashangaza kuona wanavyoruhusu kampeni za kijinga na kitoto. Mbaya zaidi wakati wakiruhusu hayo yatokee, wao si wasafi sana katika ndoa zao. Wengine wana tuhuma za kubaka na kuwaingilia watu kinyume cha maumbile.

  Haya yanafahamika, lakini kwa vile si hoja iliyo mbele yetu hatupendi kuyaingilia. Pia tunaheshimu Katiba yetu inayoruhusu mtu kuwa na maisha yake binafsi.

  Hoja yangu ni kutaka kuwakumbusha watanzania kwamba tusikubali kwenda nje ya hoja yetu. Tunamtafuta rais wa kuliongoza Taifa letu la Tanzania. Rais atakayeapa kuisimamia katiba yetu na kuilinda kwa gharama yoyote ile.

  Tunamtafuta rais, wa kutuletea mabadiliko na kutupigisha hatua ya kutoka kwenye umaskini na kutuingiza kwenye maendeleo ya kweli ya dunia ya leo.
   
 2. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  kumbe kuna wengine wamewahi kuwaingilia watu kinyume cha maumbile, duh huyo hafai kuwa mitaani anatakiwa kuwa kwenye tanuru la moto wa milele.
   
 3. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,381
  Likes Received: 3,141
  Trophy Points: 280
  Hivi katiba inasemaje kuhusu mahakama ya kadhi?.....mbona kikwete anataka kuyaingiza na kuivunja katiba,tayari alishayaweka kwenye ilani yake japo sasa kaondoa kwa lengo la kupata kura za wakristo.............kwa maana hiyo jk anaweza kuilinda katiba wakati tanzania haina dini japo kila mtu anauhuru wa kuabudu?
  Basi tusimchague kwani kakiuka misingi mingi sana ya kikatiba.......mpaka alidiriki kuingilia uhuru wa mahakama kwa kuwasamehe wezi wa mali ya umma............
   
 4. George Maige Nhigula Jr.

  George Maige Nhigula Jr. Verified User

  #4
  Sep 13, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 470
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  This article has good stuffs jamani, waandishi wetu wote wangekuwa na uelewa na umakini kama mwandishi huyu basi tungekuwa mbali sana
   
 5. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kikwete anaongozwa na Sheikh Yahya Hussein.
  Hafai kuwa rais wetu
   
Loading...