Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi awasili Tanzania, aweka jiwe la msingi hospitali ya rufaa ya kanda Burigi, Chato

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,441
7,780
Leo Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi amewasili Chato mkoani Geita kwa ziara ya siku mbili kuimarisha uhusiano ambapo atakuwa na mwenyeji wake, Rais Magufuli.

n21.jpg


4.jpg

n16.jpg


=======

Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji ameshawasili uwanja wa ndege wa Chato na kulakiwa na mwenyeji wake, Rais John Magufuli

05:34 Asb: Rais Magufuli na mgeni wake, Filipe Nyusi wamewasili kwenye hospitali ya Rufaa ya Burigi, Chato na wanatarajiwa kuweka jiwe la msingi

05: 40 Asb: Rais Nyusi amepanda mti wa kumbukumbu kwenye eneo la hospitali, mti mwingine amepanda waziri wa afya, Doroth Gwajima.

DOROTH GWAJIMA: Hospitali ya rufaa ya ngazi ya kanda sasa inazifanya hospitali za ngazi hii za serikali ya Jamhuri ya muungani wa Tanzania kuwa tatu kati ya sita, ukiunganisha na zile tatu ambazo serikali imeingia mkataba na mashirika yasiyo ya kiserikali.

Kwa upande wa hospitali zetu, ni hii yenyewe ya Chato, tunayo nyingine ya kule Mbeya ambayo ilikuwepo tangu zamani, kuna nyingine ya Mtwara kusini ambayo unaenda kuikamilisha kwenye kipindi hiki kama ilani ilivyoelekeza.

RAIS MAGUFULI: Huyu ndie bosi wetu wa SADC wa sasa kwa nchi zote 16. Awali ya yote mh. Rais na rafiki yangu nakushukuru sana kwa kuamua kuja Chato, karibu sana. Urafiki wa Tanzania na Msumbiji ni wa muda mrefu, sisi ni ndugu. Ndani ya serikali tuna makubaliano ya kufanya kazi pamoja, kushirikiana, biashara ya sasa hivi kati ya Tanzania na Msumbiji imeongezeka, mwaka jana ilifikia bilioni 93.6

Alinipigia simu akasema nataka kuja Chato, alisikia mimi niko Chato, akasema nataka tuje tuzungumze nae masuala ya amaendeleo, na mimi kwa heshma yake, nawashukuru sana wizara ya afya wakaamua hospitali hii iwekwe jiwe la msingi na Rais Filipe Nyusi.

Historia ya Chato ni ndefu, mwaka 1967 aliyekuwa Rais wa kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere, tarehe 9 Januari mwaka 67 alifika Chato, wakati huo kilikuwa bado ni kijiji cha Chato, akafungua kiwanda cha pamba cha Chato kilichojengwa kwa thamani ya milioni 2 kwa wakati huo.

Kiwanda hicho kilijengwa kwa ajili ya kutengeneza na kusafirisha marobota 20 elfu kwa mwaka. Siku ya ufunguzi, baba wa Taifa alianzisha mchango wa wananchi waliokuwepo pale katika kujenga dhana ya kujitegemea na yeye akachangia pauni 1000 katika mchango huo.

Alipotoka hapa, wiki mbili baadae, baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere akaenda Arusha, tarehe 5 mwezi wa pili akatangaza azimio la Arusha, dhana ya kujitegemea, alianzisha hapa kwa kuchangia.

RAIS FILIPE NYUSI: Nilipiga simu juzi nikamuuliza Rais Magufuli yuko wapi? Na mara nyingi huwa tunaongea asubuhi mapema, akasema niko Chato, Chato ni wapi? Akasema Chato nyumbani. Nikasema basi nije huko nyumbani kwako nikaone shule ya msingi uliyosoma wewe, akasema njoo Chato nyumbani.

Utanipikia nini? Mimi sili sembe, nakula ule ugali wa kusaga, akasema tutakusagia na nimeshafika tayari, nitakula ule ugali.

Nashukuru pia kwa kunipa nafasi pamoja na Rais kuweka jiwe la msingi, hii nadhani ni bahati sana kwetu wanamsumbiji pia kwa shauri serikali inaangalia afya ya wananchi ni serikali inayopenda wananchi, tunaweza kusema kila kitu lakini bila maisha, yote tunayosema hayataeleweka.
 
Namsikiliza hapa kwenye sherehe za ufunguzi wa Hospital ya Kanda ya Chato Waziri wa Afya, Mama Dorothy Gwajima!

Waziri anaongea haraka haraka sana kana kwamba anawahi sijui wapi!

Waziri hajapanga vizuri hotuba yake, anaongea kana kwamba anawaambia watu na sio kutoa hotuba. Mara kwa mara amekuwa anamalizia kwa kusema tumpigie makofi Mh Rais au Makofi kwake Mh Rais, sijaelewa kwanini.
 
Namsikiliza hapa kwenye sherehe za ufunguzi wa Hospital ya Kanda ya Chato Waziri wa Afya, Mama Dorothy Gwajima!

Waziri anaongea haraka haraka sana kana kwamba anawahi sijui wapi!

Waziri hajapanga vizuri hotuba yake, anaongea kana kwamba anawaambia watu na sio kutoa hotuba. Mara kwa mara amekuwa anamalizia kwa kusema tumpigie makofi Mh Rais au Makofi kwake Mh Rais, sijaelewa kwanini
Speaking style haijawahi kuwa sawa dunia nzima.
 
Back
Top Bottom