Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi awasili Tanzania, aweka jiwe la msingi hospitali ya rufaa ya kanda Burigi, Chato

Hii sasa anasa. Hospital ya Kanda Ziwa ipo Chato ?Hapa hawajaangalia proximity kabisa. Ila factor ilikuwa kijijini kwa Rais. Gbadolite part 2 in the making.
Kwa haya yanayoendelea wasiwasi wangu ni kiongozi ajaye, huenda tukashuhudia maajabu pale atakapo tumia fedha zote za bajeti za muda wake wa utawala kujenga kijiji , wilaya na mkoa anaotoka na asiguse kabisa sehemu nyingine za nchi.

Bila kupepesa macho mtawala ajaye ndie atakayeibomoa kabisa nchi,maana baada ya huyo ajae kura zitapigwa kwa kufuata mgombea ni wa wapi.
 
Kwa haya yanayoendelea wasiwasi wangu ni kiongozi ajaye, huenda tukashuhudia maajabu pale atakapo tumia fedha zote za bajeti za muda wake wa utawala kujenga kijiji , wilaya na mkoa anaotoka na asiguse kabisa sehemu nyingine za nchi .Bila kupepesa macho mtawala ajaye ndie atakayeibomoa kabisa nchi,maana baada ya huyo ajae kura zitapigwa kwa kufuata mgombea ni wa wapi.
Yaani tuombe Mungu ajae awe mzaliwa wa Kinondoni. Walau palishajengwa.
 
kumbe yupo likizo?
inamaana hao anaowapokea ni wageni binafsi?
Mungu aliipenda sana nchi hii ndio maana akamleta kwanza nyerere angalau aifungue Tanzania maana kuna wengine wangetangulia tu,Nchi isingekua na utofauti na Congo DRC. Sehemu nyingi za nchi zingebaki kua remote areas. Hii ni just 6yrs tukifika kumi nusu ya pato la nchi litakua limekwenda kujuenga wilaya moja tu. Yajayo yanafurahisha.
 
Nyie watu vp, mnalalamika sana hivi kwani hamjui chato ndo uwanja wa ndege wa kimataifa unapojengwa?

Na sasa uwanja huo wa ndege bado kidogo ukamilike, hivyo basi ndege zote za kimataifa lazma zianzie chato na zishukie chato.
Hapo hiyo ni ndege imetoka taifa lingine lazma ingeshukia chato kiwanja cha ndege za kimataifa. Hivyo basi mkuu akaona arahisishe mambo kila kitu kimalizikie Chato.

So mh. hana makosa.
 
Hivi Rais anatembelewaje nyumbni keske ziara ya kikazi?? si angeahirisha mapumziko akampokea mgeni wake Ikulu theni mgeni akiondoka anarudi kwenye mapumziko yake?? huyu jamaa mi huwa simuelewi kabisa hatukuyaona huko nyuma.

Rais wa Musunbiji na Mwenyekiti wa Sadc anahusikaje kuweka jiwe la msingi hospitali ambato haikujengwa kwa msaada wa sadc au Msumbiji??
Ana madharau sana huyu
 
Ni makosa makubwa kuendeleza kanda moja na nyingine ikasahaulika, ki Taifa, ni kosa kubwa, lakini je, ni kweli kanda ya ziwa ilikuwa imesahaulika sana?

Inasadikika kuwa, Watu kutoka kanda hiyo, ilikuwa ni vigumu kufaulu kutoka Standard 7 na kuingia secondary, hii ni Kwa sababu ya uwoga wa watawala eti kwamba, hao jamaa Kwa kuwa ni wengi mno! Wataleta shida! Na za chini chini ni kwamba, ilikuwa wasipewe Uongozi wa juu kitaifa, Kwa sababu zao wanazozijua wenyewe!

Ajabu ilikuwa, mtu huyohuyo aliyekuwa akifeli huko kwao, akija kurudia kanda ya Kati, anakuwa mwanafunzi daraja A"
Je hayo Ni ya kweli ATI?

Watu mnaotoka huko ni ya kweli hayo
 
Yaani tuombe Mungu ajae awe mzaliwa wa Kinondoni. Walau palishajengwa.
Kinondoni bado kabisa hiyo, inahitaji kuwa na metro system, Trams,Tandale , manzese yote ibomolewe zijengwe 5 stars apartments kisha wakazi walipe rent ndogo .zinahitajika Arena za basketball, Tennis na michezo mingine..Kinondoni bado sana hiyo kiongozi ajaye akitoka kinondoni ataibadili kuwa dubai kivitendo sio kisiasa kama walivyokuwa wakibwabwaja kina Ummy Mwalimu
 
Ana madharau sana huyu
Hata mimi naona ivo alianza na Uhuru Kenyatta na Raila Odinga sasa kaja na Msumbiji inaelekea anataka Ikulu ihamie Chato.

Nina uhakika kabla hajamaliza mda wake makao makuu wa mkoa wa Geita yatahamia Chato, Geita itabaki kuwa Wilaya
 
Kinondoni bado kabisa hiyo, inahitaji kuwa na metro system, Trams,Tandale , manzese yote ibomolewe zijengwe 5 stars apartments kisha wakazi walipe rent ndogo .zinahitajika Arena za basketball, Tennis na michezo mingine..Kinondoni bado sana hiyo kiongozi ajaye akitoka kinondoni ataibadili kuwa dubai kivitendo sio kisiasa kama walivyokuwa wakibwabwaja kina Ummy Mwalimu
Bora. Ni Dar mji wa biashara. Mapato si haba. Yataongezeka.
 
Hata mimi naona ivo alianza na Uhuru Kenyatta na Raila Odinga sasa kaja na Msumbiji inaelekea anataka Ikulu ihamie Chato.

nauhakika kabla hajamaliza mda wake makao makuu wa mkoa wa Geita yatahamia Chato, Geita itabaki kuwa Wilaya
Ataanzisha mkoa wa Burigi. Chato makao makuu ya mkoa. Hiyo hospital kuitwa Burigi kuna sababu.
 
Back
Top Bottom