Rais wa Msumbiji, Felipe Nyusi Kufanya Ziara ya siku mbili nchini

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,193
4,661
Rais Nyusi atatembelea Tanzania kwa ziara rasmi ya Kiserikali kuanziaa tarehe 11-12 Januari 2021

Mgeni huyo muhimu atawasili nchini kupitia uwanja wa ndege wa kisasa wa Chato, Mkoani Geita na kupokelewa na mwenyeji wake Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Karibu mgeni & karibu Tanzania
Kisiwa cha Amani

Chanzo: Waziri wa Mambo ya Nje, Profesa Palamagamba Kabudi

=====

Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi leo anatarajiwa kuwasili wilayani Chato, mkoa wa Geita kwa ziara ya kikazi ya siku mbili nchini.

Hii ni mara ya pili kwa Rais Nyusi kuja nchini wakati wa utawala wa Rais John Magufuli, mara ya kwanza alifika jijini Dodoma Desemba mwaka 2017.

Rais Nyusi pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), nafasi anayoishikilia baada ya kuipokea kutoka kwa Rais Magufuli Agosti Mwaka jana.

Mwaka jana wananchi wa Msumbiji walipiga kura na kumchagua Rais Nyusi kuongoza muhula wa pili. Mara ya kwanza aliongoza nchi hiyo baada ya kushinda Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwaka 2014.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kuhusiana na ujio huo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi alisema Rais Nyusi atatua katika Uwanja wa Ndege wa Geita-Chato saa 4:30 asubuhi.

"Napenda kuwafahamisha kuwa Rais Magufuli anatarajia kumpokea Mheshimiwa Filipe Nyusi, Rais wa Jamhuri ya Msumbiji hapa Chato, mkoani Geita kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kuanzia kesho (leo)," alisema.

Profesa Kabudi alisema ziara hiyo ilikuwa ifanyike tangu mwaka jana lakini iliahirishwa kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Oktoba mwaka jana.

"Ziara hii ya Rais Nyusi ni ya kindugu ilipangwa kufanyika muda mrefu mwaka jana. Na kwa wakati huu Rais Magufuli yuko Chato ameona amkaribishe afike huku," alisema.

Profesa Kabudi alisema ziara hiyo ni katika kuendeleza na kuimarisha maeneo anuai ya kidoplomasia, kiuchumi, kisisa na kijamii kama ilivyoasisiwa na vyama na waasisi wa nchi hizo mbili.

"Uhusiano huo umeendelea kuwapo hata baada ya Msumbiji kupata uhuru wake. Kuanzia kiongozi wa mpito na baadaye Rais wa kwanza wa Msumbiji, Samora Machel hadi Rais Nyusi na kuanzia Mwalimu (Julius) Nyerere hadi kiongozi wa sasa hapa nchini wote wameendelea kuimarisha uhusiano ambao kwa hakika ni ndugu wa damu." "Viongozi wote wameendelea kuhamasisha uhusiano huu wa ndugu wa damu ndio maana hata wakati wa mazishi ya Rais wa Awamu ya Tatu, Hayati Benjamin Mkapa, Balozi wa Msumbiji hapa nchini alileta salamu kutoka kwa Rais Nyusi na Rais Mstaafu, Joaquim Chissano,” alisema.

Profesa Kabudi alisema uhusiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Msumbiji umeendelea kuimarika katokana na biashara inayofanyika kati ya nchi hizi mbili.

"Takwimu za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zinaonesha mauzo ya nje katika ya nchi hizi yameongezeka kutoka Sh bilioni 76.4 mwaka 2018 hadi kufikia Sh bilioni 93.5 mwaka 2019.”

"Kampuni kubwa za Kitanzania zimewekeza nchini Msumbiji ikiwa ni Bakhresa, Quality Form-Magodoro Dodoma, Mohamed Interprises na kampuni za usafirishaji wa mizigo na abiria," alisema.

Alisema licha ya changamoto ya ugonjwa wa covid-19 unaosababishwa na virusi vya corona, Tanzania na Msumbiji zimeendelea kuwezesha na kusimamia biashara kati ya nchi hizo.

Alisema wakati wa ziara hiyo Rais Nyusi atabadilishana mawazo na Rais Magufuli kuhusu biashara na kuongeza uwekezaji kati ya Tanzania na Msumbiji.

"Pia tunatarajia atakuwa na shughuli nyingine nje ya kukutana na mwenyeji wake na kuacha kumbukumbu kwa Watanzania,” alisema Profesa Kabudi.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel aliwataka wananchi mkoani humo kujitokeza kwa wingi kumpokea Rais Nyusi.
 
Rais Nyusi atatembelea Tanzania kwa ziara rasmi ya Kiserikali kuanziaa tarehe 11-12 Januari 2021

Mgeni huyo muhimu atawasili nchini kupitia uwanja wa ndege wa kisasa wa Chato, Mkoani Geita na kupokelewa na mwenyeji wake Rais Dkt John Pombe Magufuli.

Karibu mgeni & karibu Tanzania
Kisiwa cha Amani

Chanzo: Waziri wa Mambo ya Nje, Profesa Palamagamba Kabudi
Serikali imeachana na Dodoma!
 
Magufuli hajamaliza kutambika huko chato arudi ikulu ya Rais chamwino kupokea wageni wa kitaifa?
 
Sasa hivi makao makuu ya nchi yasiyo rasmi ni Chato Mzee, kwani wewe hujui?

Hao wageni wote wanafikia Chato na watalala kwenye Hoteli zake Jiwe!

Hakika huyu Jiwe ametugeuza watanzania wote kuwa ni wapumbavu na malofa tisioelewa chochote!
Kwa anayoyafanya jiwe. Ametufanya sisi watanzania ni kama watoto wake. Yaani anajiona kama yeye ana hati miliki ya nchi hii.
 
Back
Top Bottom