Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi, aleta neema Tanzania Kiuchumi, Elimu, Afya na Utalii, Kiwanda cha nyama Kujengwa

Magazetini

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
588
1,698
Rais wa Misri, Ndugu Abdel Fattah el-Sisi anawasili nchini Tanzania kwa ziara ya siku 2. Analakiwa na Mwenyeji wake, Dkt. John Pombe Magufuli uwanja wa ndege wa JNIA.

Rais wa Misri yupo Ikulu, Dar es Salaam akiwa na mwenyeji wake, Rais Magufuli kwenye ziara yake ya siku mbili nchini.

-Fuatana nasi kujua kitachojiri Ikulu.

Rais wa Misri, Abdel Fattah el-Sisi ameshatua na kinachoendelea kwa sasa ni nyimbo za mataifa yote mawili ambapo marais wote wawili wamesimama kwenye eneo lilitotengwa kwa ajili yao.

Rais wa Misri ameelekea kupumzika kabla ya kuanza ratiba yake ya ziara ya siku mbili nchini ambayo atahitimisha kesho. Akimaliza ratiba yake Tanzania, ataelekea nchini Rwanda kuendelea na ziara yake.




=>Mh rais na wageni tumezungumza maneno mengi, nchi ya Misri ina historia kubwa.

=>Hata mapiramidi, historia ya Misri bado inatambulika na dunia nzima.

=>Hata vitabu vya dini vimeandika, hata mtume Yesu Kristo alipotaka kuuawa alikimbilia Misri.

Najua Mh rais ananisikia

=>Lakini nchi ya Misri ina idadi kubwa ya watu zaidi ya milioni 93, ukubwa wa eneo tunawazidi kidogo.

=>Pia ina eneo kubwa lenye jangwa.

=>Pamoja na kwamba hatukuungana kati ya nchi na nchi, lakini tumeunganishwa na maji. Unaweza kunywa maji hapa na mtu mwingine akayanywa Misri.

=>Maji yanayokusanywa katika ziwa victoria ambapo 55% yapo Tanzania, 5% Kenya na 44% yapo Uganda.

=>Tumekubaliana ku-revive joint commsion kupitia mawaziri.
=>Tumekubaliana kushirikiana katika biashara

=>Tumekubaliana pia kuendeleza sekta ya kilimo ikiwemo irrigation

=>Tumekubaliana kuboresha huduma za afya katika hospitali ya Muhimbili, na Mnazi Mmoja Zanzibar. Muhimbili iweze kufanya upasuaji wa figo na maswala mengine kabla ya 2020.

=>Kutusadia namna ya kupanua na kupata idadi kubwa watalii, sisi tunapata watalii 2M, Misri wanapata 10M kwa mwaka. Watashiriikiana na air Tanzania ili kukuza sekta ya utalii.

=>Kuimarisha masuala ya ulinzi.

=>Kushirikiana katika masuala ya elimu. Sisi tutoa walimu wa Kiswahili. Wao watatuletea wataalam wa IT, Sayansi na Kiarabu.

=>Tumezungumza jinsi ya kuutumia mto Nile kwa maendeleo ya nchi hizi mbili japo hatujafikia muafaka.

=>Rais amenialika kuwatembelea na kama tunavyojua Misri ni Marafiki zetu

=>Nimempa nafasi rais wa Zanzibar kuelezea changamto zilizopo. Akanidokeza miaka kumi iliyopita aliingia Zanzibar kiujanjanja ujanja Zanzibar kwa hiyo anajua marashi ya Zanzibar

=>Nikushukuru sana mheshimiwa rais na zaira hii imeimarisha uhusiano wa Tanzania na Misri.

=>Amekubali pia kutuma wataalamu wake kuwekeza katika phamacetical industries hapa nchini.

=>Tunamshukuru sana kwani waliosimamia daraja la Kigamboni
Na yeye ni rais na pia ni field marshal kwahiyo anapenda sana actions

=>Tumezungumzia pia ishu ya corruption kuwa na timu nzuri inayoshughulikia masuala ya corruption kwani ni kansa ya maendeleo.

=>Napenda kukushukuru sana mh rais, na Mungu abariki uliopo kati ya Misri na Tanzania.
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom