Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba hatoziwekea vikwazo vya kibiashara nchi za Tanzania, Uganda na Kenya

Lee Swagger

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
1,064
1,807
TRUMP AIBANA KOO RWANDA - TANZANIA, UGANDA, KENYA ZAPONEA CHUPUCHUPU: Rais wa Marekani Donald Trump amesema kwamba hatoziwekea vikwazo vya kibiashara nchi za Tanzania, Uganda, Kenya kama alivyofanya kwa Rwanda endapo nchi hizo zitaendelea na uamuzi wao wa kutopiga marufuku bidhaa za mitumba kutoka marekani.

Uamuzi huo wa Trump wa kuiwekea Rwanda ushuru wa nguo zake katika soko la Marekani umetokana na Rwanda kuweka vikwazo kwa nguo na viatu vya mitumba vinavyotoka Marekani.
Chini ya mkataba wa ushirikiano wa kibiashara baina ya Afrika na Marekani (AGOA) baadhi ya nchi za Afrika Rwanda ikiwemo ziliondolewa ushuru wa baadhi ya bidhaa zake zinazouzwa Marekani.

"Hata hivyo Marekani inaendelea kutoa faida za AGOA kwa mataifa ya Tanzania na Uganda kwa sababu nchi hizo zimechukua hatua ya kuondoa kodi ya nguo na viatu vya mitumba na kuamua kutopiga marufuku bidhaa hizo," alisema mwakilishi wa ofisi ya biashara ya Marekani.

"Ninaipongeza Tanzania na Uganda kwa kuchukua hatua za kupatia suluhu hofu za Marekani," alisema afisa wa masuala ya biashara katika ofisi ya rais nchini Marekani C. J. Mahoney katika taarifa yake.

Rais Trump amesema kuwa kupiga marufuku mitumba Rwanda imevunja makubaliano ya kibiashara na Marekani chini ya AGOA.
FB_IMG_1522488845549.jpg
FB_IMG_1522488850931.jpg
 
Mitumba imetutoa sana miaka ile,Naingia zangu kwa sheni nakula kangundu langu baloo kama 3 naingia nazo mnadani pande za matui,chakwale,mvumi mpaka kiteto..Damn
 
Kwa hali tuliyonayo bado tunahitaji sana mitumba itutoe la sivyo tukubali kujifunika mashuka ya mmasai na vitenge manaake sidhani kama tina kiwanda chochoye cha matisheti na vimodo
 
Back
Top Bottom