Rais wa Malawi Awananga Waandishi wa Habari wa Tanzania

Ukweli unauma!! Ni kweli vyombo vyetu vya habari havina wabunifu wa kujadili hoja, nilitegemea waandishi wetu wangekuwa wanatoa somo zaidi katika inshu nyingi kuelimisha jamii badala yake karibia waandishi wote wanaegemea kwenye kuripoti habari kutoka kwa wanasiasa zaidi. Vyombo vya habari vijifunze namna ya kujenga hoja zikakubalika kwenye jamii badala ya kukimbilia/kutegemea wanasiasa na watu wengine waropoke ndiyo wapate habari za kuandika.

....Kama MwanaHalisi wanavyo ripoti. Huku si kuwananga, bali ni KUSEMA UKWELI. Hata Ben Mkapa aklwa rais, alishawahi sema haya! Vibonzo vya kenya wakati fulani walishawahi sema haya pia. Kusema kweli, nilisoma yale walosema Membe, Sitta na Lowasa, SIKUONA mahali waliposema kuwa VITA INAKUJA! Kwa hiyo sensational reporting, ambayo inalenga kuuza habari, inaharibu HADHI ya habari hapa Tanzania.
 
Huyu mama ni Rais wa nchi mbili hawezi kuropoka hivi hivi
 
Huyu mama asituzingue kabisaaaaaa! aliyeanza kusema hatuachii hata sentimeta moja ya Nyasa ni nani? Kauli zao ndio zilizotuzindua! Alafu unaposema hamuachii hata sentimeta moja ya Nyasa unamaanisha nini kama si vita?

Yaani uchukue sehemu ya Tanzania hata kama kwa maneno tusijiandae kwa lolote! Mazungumzo yataendelea na wazee wa kazi JWTZ wataendelea na mazoezi endelevu pale Kyela! Tena yale matizi yetu yaleee ya kuvunja matofali kwa vichwa!
 
Na hao wanasiasa anaowataja kuwa walinukuliwa na wanahabari wa Tanzania, ni WAPINZANI. Ikumbukwe kuwa JK alimwambia Joyce kuwa wapinzani ndio wanaoshabikia vita ! Sasa sijui Membe na EL ni wapinzani wa JK !!?
 
Tatizo kubwa kwa wenye byombo vya habari hawaajiri waandishi ili kukwepa kuwapa mishahara ya maana na stahili. Matokeo yake wanawatumia kama vibaru na makanjanja. Sasa unategemea kibarua ambaye hana ties na kampuni akufanyie kazi vizuri? Wenye vyombo vya habari, mtihani kwenu na do justice to waandishi. Bila wao hakuna habari ya kufanya kampuni yako iendelee mbele. Ngoja siku wagome kama editors hawatakosa kazi na kampuni kwishey kama Kafumu leo.
 
Na hao wanasiasa anaowataja kuwa walinukuliwa na wanahabari wa Tanzania, ni WAPINZANI. Ikumbukwe kuwa JK alimwambia Joyce kuwa wapinzani ndio wanaoshabikia vita ! Sasa sijui Membe na EL ni wapinzani wa JK !!?

Ha ha ha ha mkuuu. Udhaifu wa kufikiri huo!!! Tukisema dhaifu mnatuambia tuondoe hoja na kuomba miongozo.
 
Ha ha ha ha mkuuu. Udhaifu wa kufikiri huo!!! Tukisema dhaifu mnatuambia tuondoe hoja na kuomba miongozo.
Mkuu, ukweli ndio huo. Jaribu kutafuta katika media jinsi rais wako alivyomwambia Joi. Maybe hujanielewa!
 
Rais wa Malawi hajitambui!!! Yeye ndio mwenye mamlaka ya kuamuru kama Malawi iinge kwenye vita au lah, sasa anamaanisha kuwa maamuzi yake yangekuwa influenced na waandishi!!! Hiki kichekesho kingine, hahahahahahahahahahaha hivi watu wa namna hii wanaraise vipi mpaka kuwa Rais?!!!
 
Ha ha ha ha mkuuu. Udhaifu wa kufikiri huo!!! Tukisema dhaifu mnatuambia tuondoe hoja na kuomba miongozo.
Mku nimekuelewa haswa hiyo post yako hapa chini. Na nimekubaliana na wewe kuhusu media.

Na hao wanasiasa anaowataja kuwa walinukuliwa na wanahabari wa Tanzania, ni WAPINZANI. Ikumbukwe kuwa JK alimwambia Joyce kuwa wapinzani ndio wanaoshabikia vita ! Sasa sijui Membe na EL ni wapinzani wa JK !!?
Naunga mkono hija yako, tena na miguu kabisa. Zis iz Tansania.

Mkuu, ukweli ndio huo. Jaribu kutafuta katika media jinsi rais wako alivyomwambia Joi. Maybe hujanielewa!
Nilijibu kwa lugha ya fumbo mkuu. Nimekupat barabara.
 
Kwani waandishi wa tanzania walikosea wapi? Mbona wamekuwa wakiandika kile kinachotamkwa na wanasiasa tena bila kuongeza hata neno. Kwa mfano mzee Lowassa alisema tuwakung'ute tu hawa wanataka kutuzingua tena na majeshi yetu yapo tayari kiakili na kila kitu sasa hapo waliongeza neno gani wakati wote tulisikia? Na ninaomba niwadokeze wale wasio waeledi wa siasa ni kwamba alichofanya Lowassa ndicho hasa Malawi walikuwa wanakisubiria kukisikia kwa muda mrefu sana! Ni kauli hiyo tu ndiyo imewarudisha kwenye utii uliokuwa umetoweka, sasa wacha mazungumzo yaanzae hata kama yakichukua karne sio tatizo ilimradi tunaendelea kuvua samaki na kuogelea kwenye ziwa letu.
 
aache kelele zake,ye akae mkao wa kutandikwa tu akileta jeuri yake

Big up Sana kwa waandishi wa Jabari na Jamii forum kwa kutuhabarisha, Huyu mama akileta kiherehere chake tena ni kumtandika tu halafu habari baadae, ili siku nyingine awe na adabu ala! Anachezea nchi ya mwalimu, alituachia mipaka tutailinda, labda hichi kizazi cha dot com ndicho kite kimpe lake nyasa wakati tupo makaburini, hatakipindi hiicho makaburini yatafumuka.
 
My Take: Waandishi wa habari wa Tanzania wanaandika yale yanayosemwa na wanasiasa kuhusu suala la mpaka.

ukiachilia mbali mapungufu ya upande wa pili(malawi),lakini ni kweli usiopingika kuwa waandishi wetu wa habari waliripoti tofauti(vibaya) hili suala la mgogoro wa Tz na Malawi.Niliwasikiliza hao viongozi watatu(sitta,membe na lowasa) kwa nyakati tofauti ila hakuna hata sehemu wamesema kuwa tutapigana vita na malawi.
Ukweli ni kuwa waandishi wetu wengi wana-exagrate sana habari..hasa za kisiasa.sijui kwa nini?mfano gazeti linaweka kichwa cha habari;"watu 27 waficha pesa uswisi"lakini ukisoma ndani ya gazeti hupati hata jina moja,why this?hii kwangu mimi ni kama habari ya kijiweni.
Nadhani waandishi wetu wajifunze kuwa wachambuzi zaidi kuliko kuripoti habari zinazoonekana nyepesi nyepesi(sijui nitumie lugha/neno gani ili nieleweke lakini waandishi wetu wanahitaji mabadiliko)
 
....Kama MwanaHalisi wanavyo ripoti. Huku si kuwananga, bali ni KUSEMA UKWELI. Hata Ben Mkapa aklwa rais, alishawahi sema haya! Vibonzo vya kenya wakati fulani walishawahi sema haya pia. Kusema kweli, nilisoma yale walosema Membe, Sitta na Lowasa, SIKUONA mahali waliposema kuwa VITA INAKUJA! Kwa hiyo sensational reporting, ambayo inalenga kuuza habari, inaharibu HADHI ya habari hapa Tanzania.
Yeah, kweli kabisa mkuu! Nilitegemea waandishi magwiji ya habari yangekaa chini na kuuelimisha umma umuhimu wa kuingia vitani na hasara za kuingia vitani. Walitakiwa watoe mifano ya nchi mbali mbali zilizowahi kupitia hatua kama hiyo, je zilifaidika au ni kusumbua wananchi wake? Tatizo ni kama mnavyojua, waandishi wengi wamewekwa mfukoni. Na pengine hawa wanasiasa wangekuwa wanajifunza kitu kutokana na ugwiji wa kuandika habari. Naimani kubwa kama tasnia ya habari itaamua kuuelimisha umma kuhusu jambo fulani, sidhani kama kutakuwa na kiongozi atakayekuwa juu ya sheria.
 
huyu mama yuko right.waandishi wa habari wa bongo wapuuzi sana...wanasubiri ondo za jf na wanasiasa wapuuzi waseme ndio waandike..ni upuuzi tu..akuna habari za kitafit bali wamekali majungu tu
 
Huyo mhalalisha ushoga mbona vyombo vya kwao pia vilikuwa vikiegemea upande mmoja tu kwamba ziwa lote 100% ni lao je huo si uchochezi?

Mkuu au hujagundua kwamba Banda ndiye role model wa jf? Lolote atakalosema mchokozi huyu lipigiwa debe kuwa ndo marking scheme!
 
Alisikia vijana wana hamu ya kumvua gagulo imebidi awe mpole! Si ni huyuhuyu alisema atakufa kwa kulinda mipaka ya Malawi? Sasa imekuwaje tena? Tumb..f kabisa!
 
Waingerezj wanasema 'the hood comes first'.. Ndicho alichofanya huyu mama. Sasa jamaa yetu yeye kaanza kuwalaumu watu wake mwenyewe na kuwaita 'ma-opozishen' na kujitutumua kuwa yeye ndo mwenye filimbi ya kuruhusu ngoma ipigwe ama ispigwe na hajapuliza..,sasa hiyo ina-HU?
 
Back
Top Bottom