Rais wa Malawi auza ndege ya rais na magari 60 ya kifahari..je ni mtego kisiasa?

LUTAMBI

JF-Expert Member
Jun 1, 2012
233
102
Rais wa Malawi..Bi Joyce Banda ambaye ni mwanamke wa pili Afrika kuwa rais, ameipiga mnada ndege ya serikali iliyokuwa ikitumiwa na rais aliyemtangulia marehemu Bingu wa Mutharika.

Pia ameyapiga mnada magari 60 ya kifahari aina ya MERCEDEZ BENZ ili ipatikane pesa ya kuboresha huduma za kijamii ikiwemo madawa ya hospital, huduma ya maji, elimu, mishahara madaktari na wahudumu wengine serikalini.

Unauonaje uamuzi wake?

=========

The $15 million raised from last year's sale of a luxury Malawi presidential jet fed the poor and bought military equipment, the President said on Wednesday amid allegations it may have been embezzled.

"It was me who said let's sell the jet and the Cabinet agreed three things to benefit Malawi...to buy maize, buy military equipment such as patrol boats and pay for peacekeeping mission in the DRC," President Joyce Banda said.

Malawi has contributed soldiers to the 3,000-strong UN intervention brigade authorized to go after armed groups ravaging DR Congo.
 
Nafikiri Pinda ana majibu yote. Vipi kawanunulia mawaziri wake escudo?
 
Nafikiri Pinda ana majibu yote. Vipi kawanunulia mawaziri wake escudo?

Pinda hawezi ila nilisha msikia Lukuvi akiongea kitu kuhusu Escudo, cjui mawazo hayo yaliishia wapi. Pengine anasubiri akipewa mpini....bongo bana
 
Big up Bi Joyce, wenye macho na wapenda nchi zao watakuiga uyafanyalo. Sisi watanzania tunasikitishwa na kikwete, Ocd anatembelea shangingi la million 200, mkuu wa wilaya million 200, Mkurugezi wa halmashauri milion 200, Afisa elimu wa wilaya million 200, viongozi wote wa taasisi wilayani hivyo hivyo. Mkoani hali kadhalika hivyo hivyo, Rais mpaka katibu mkuu wa wizara hivyo hivyo! Nchi inadaiwa deni la trion 22, inaongoza kwa kukopa na kupewa misaada, Je? Tutafika ? HAPANA! Kikwete unatupeleka pabaya na Pinda wako mnafiki.
 
Mungu aione nchi yetu atujalie viongozi wenye maamuzi magumu kama huyu.
 
SI KWAMBA SERIKALI HAIJUI KUWA KUNUNUA, KULIHUDUMIA TOYOTA LAND CRUISER v8(na yote yanayofanana na hayo) NI GHARAMA KUBWA bali ni ulaji wa baadhi ya watu maana kama watu wanapata 10% kwa nini asipigie debe? jamani tujifunze kwa wenzetu wa-RWANDA na KENYA wao waziri hatembelei STATION WAGON ni VOLKSWAGEN PASSAT(saloon car). Kwa staili hii tunatengeneza taifa/kizazi wasiojua umuhimu wa kubana matumizi. La muhimu apatikane kiongozi kama Joyce Banda na kuamua. Waziri Mkuu wa Norway akisafiri kwenda popote duniani hupanda ndege za Abiria ingawa ni 1st Class hapa kwetu Prof. Mukandala wa UDSM (mfano mmojawapo) hata akienda MWANZA/BUKOBA lazima apande 1st Class tena kwa gharama za chuo/serikali? tutafika? Tena siku hizi kuna mchezo wanacheza dereva wa LAND CRUISER anatangulia na gari kama ni Mwanza toka Dar then kesho yake Mkuu anapanda ndege anamkuta dereva anamsubiri Airport. WHAT A SHAME WATANZANIA?

Hata kama Mama Rais Banda wa Malawi anatumia ni mbinu ya kisiasa ya yeye kuchaguliwa kwenye uchaguzi ujao mi binasi naona ni mbinu nzuri kuwafanya wanachi kuamini kuwa unawajali kuliko Anasa za magari ya kifahari
 
si kwamba serikali haijui kuwa kununua, kulihudumia toyota land cruiser v8(na yote yanayofanana na hayo) ni gharama kubwa bali ni ulaji wa baadhi ya watu maana kama watu wanapata 10% kwa nini asipigie debe? Jamani tujifunze kwa wenzetu wa-rwanda na kenya wao waziri hatembelei station wagon ni volkswagen passat(saloon car). Kwa staili hii tunatengeneza taifa/kizazi wasiojua umuhimu wa kubana matumizi. La muhimu apatikane kiongozi kama joyce banda na kuamua. Waziri mkuu wa norway akisafiri kwenda popote duniani hupanda ndege za abiria ingawa ni 1st class hapa kwetu prof. Mukandala wa udsm (mfano mmojawapo) hata akienda mwanza/bukoba lazima apande 1st class tena kwa gharama za chuo/serikali? Tutafika? Tena siku hizi kuna mchezo wanacheza dereva wa land cruiser anatangulia na gari kama ni mwanza toka dar then kesho yake mkuu anapanda ndege anamkuta dereva anamsubiri airport. What a shame watanzania?

Hata kama mama rais banda wa malawi anatumia ni mbinu ya kisiasa ya yeye kuchaguliwa kwenye uchaguzi ujao mi binasi naona ni mbinu nzuri kuwafanya wanachi kuamini kuwa unawajali kuliko anasa za magari ya kifahari

umenena jembe.... Nahisi umeumizwa na hali hii bongo. Big up banda
 
huyu mama safi sana...bora tungebadilishana huyu aje huku halafu YULE HANDSOME wetu wa pale MAGOGONI aende kule
 
Huyu mama anatafuta Nobel peace pri e. Laiti angejua hawa wanasiasa anatak kufanya urafiki nao wanaweza mtupa kama taka. kuchukulia nchi ka yake nakutofanya kazi na kushiriki na wengine kitamuhaibisha mwishoe.
 
hii inaonyesha jinsi gani wanawake wako strong kwenye ku make decisions...Rais mwanaume asingeweza kufanya hivyo..labda na sisi tutafute mwanamke aongoze nchi yetu..tumeshapata wanaume wengi na wote ni wezi
 
  • Tanzainian president's Plane vs Malawian President's plane
Sijui kama nakumbuka vizuri lakini Waziri wa Fedha wa wakati huo Ndg. Mramba alisema. "hata kama Watanzania watakula nyasi lazima ndege ya rais inunuliwe" swali, Watanzaninia wale nyasi ambazo hata simba akitindikiwa hula hizo nyasi-(lazima ndege ya raisi sio ya nchi) inunuliwe.

Mh.Kikwete mwanzoni alipinga sana akasema haitaki ndege hiyo lakini ukabaila ni mtamu jamani, Mungu asamehe yote hiyo ndege mpaka leo ipo na ndo inayobeba hata mkaa wa Seif huko Pemba. tetteehhhettehhee


  • Malawi: "kama wananchi wangu watakufa njaa haiwezekani lazima niuze ndege hii ya Rais(mimi mewenyewe Rais) ili ninunue chakula kuokoa hata roho moja ya Mmalawi asife kutokanan na njaa ya chakula nauza ndege hii (yangu) ya raisi ni bora nipaqnde economy class nifike sawa na wengine wa business class"
  • Waafrica hata huyu mama akikosa Mo-Ibrahimu Prize atakapostaafu basi hakuna wa kupewa tena Africa never never again.
Hii ni misingi mikubwa ya kisiasa ya jamii ambayo Mungu amekupa kuisimamia wewe Mtanzania wa elimu ya kutambua ujinga na upumbavu.
  1. Hivi ni wananchi wangapi waliokufa baada ya Waziri Basil Mramba kutangaza hivyo(ambaye hakupima hata hata kama kuna kufa baada ya miaka kadhaa hapa duniani), naomba tume ya maafa itoe majibu hapa.......
  2. Maswali mengine wanaJF naamininwnayomengi zaidi ntayouliza, plse uliza..............................
Tuwasilishe...................................
 
vp mkuuu hako ka-ndege anakauzaje? maana nimechoka kujibanabana kwenye public planes tehe teheeeeee.JAMANI NIMETANIA
Rais wa Malawi..Bi Joyce Banda ambaye ni mwanamke wa pili Afrika kuwa rais, ameipiga mnada ndege ya serikali iliyokuwa ikitumiwa na rais aliyemtangulia marehemu Bingu wa Mutharika.

Pia ameyapiga mnada magari 60 ya kifahari aina ya MERCEDEZ BENZ ili ipatikane pesa ya kuboresha huduma za kijamii ikiwemo madawa ya hospital, huduma ya maji, elimu, mishahara madaktari na wahudumu wengine serikalini.

Unauonaje uamuzi wake?
 
Back
Top Bottom