Rais wa Liberia amsimamisha kazi mwanae

Historia ya uongozi ya Liberia ni historia ya uongozi wa kiukoo zaidi na hiki kwa anayejua si cha kushangaa..nasikitika tu kwa baadhi ya watu kuingiza ushabiki kwenye hili kwa kufananisha na Tanzania.

Haitowezekana kwa tanzania ya leo mtu aweke watoto wake ngazi za juu Benki kuu, SHirika la Mafuta, na Usalama wa taifa. Hii ni moja wapo wa lasting legacy ya Nyerere, hakutaka kakikundi fulani, na watu wa aina fulani wahodhi madaraka makubwa sehemu nyeti za uongozi na kwa msimamo huo nepotism ikawa imepigwa risasi ya kichwa. inawezekana bwana Nepotism anarecover haswa ngazi za chini za kiserikali , lakini bado hatuwezi kujilinganisha na vinchi kama hivi hata kama tuna chuki binafsi na Jk au CCM, tanzania hatuna hizi low standards za kazi za kitaifa.

Halafu tunashangilia kumsimamisha kazi kwa kutotangaza nafikiri tungejifunza zaidi kama angemsimamisha kazi kwa kutangaza mali za uongo. hii ingeleta maana zaidi kuliko hiki kiini macho.

mleta mada hii ni displaced topic hatuna cha kujifunza hapo
 
Hapo hakuna cha kujifunza. Naona kama kumsimamisha kazi mwanae ni danganya toto. Kama ameweza kuwateua wanae wote maana yake ni kwamba anatawala kidugu-nepotism. Tusidanganywe na neno kusimamisha kazi. Kimsingi, Afrika bado tuko mbali. Kwenye nchi za wenzetu huwezi kuwateua wanao hivyo na bado ukaendelea kuwa madarakani. Laiti kama wale watoto wangekuwa wamegombea na kushindwa kwa merits zao hakuna ambaye angeona makengeza kama haya. Sirleaf alimsaidia Taylor kuiharibu ile nchi ambayo naye anamalizia. Hana tofauti na Jakaya katika kutumia madaraka kunufaisha familia na marafiki zake.

Na mimi nililtaka kusema hilo kua sidhani kama ni wazo zuri kwa Rais kuteua watoto/ndugu zake kwenye nafasi muhimu serikalini hasa kwenye usalama wa taifa na wizara nyeti..bt africa ndio tulivyo Gadaffi alifanyaga hivyo na wengineo wengi wamefanya hivyo pia
 
Afrika sijui tuna nini, huyu mama naye kaishaingia kwenye kurithishana?
Yule wa Gambia ndiyo kituko cha hali ya juu.

kuna hii equtorial guinea, Togo, etc hizi nchi wananchi wake wanavuta tu pumzi na matumaini ya kujiendeleza kijamii, kisiasa na kiuchumi ni finyu sana kwenye tawala za kijinga kama hizi.
 
Ndo ivo Mkuu ''Dont break the Law just bend it'' na ndo alichofanya hyo mama na viongozi wengi Africa wanafanya ivo.

Hakuna lolote alichokifanya,mpaka watoto wake 3 wawe katika nafasi nyeti hivyo serikalini kwani watu wengine hawapo?
Tabia hii ya kulundika watoto wa vigogo srekalini ni tabia ya viongozi wengi wakiafrica,waache hiyo tabia,siku moja tutawachoka,waulize watoto wa GADAFI KILICHO WAPATA
 
jk unajifunza nini kwa mwanamama huyu?

Jk hana cha kujifunza, wewe fikiri watoto 3 wa Rais kawateua nafasi nyeti. Anawawajibishaje? Wote wana matatizo. JK yeye anawapa pesa na malori kwa mlango wa Nyuma, mwenzio mlango wa mbele wazi wazi.

 
hapo sioni kama ni kweli kafanya hivyo kujikosha tu wala hakuna la maana kwa nini ateue mtoto (familia ) iwe kwenye uongozi wake??
 
kuna hii equtorial guinea, Togo, etc hizi nchi wananchi wake wanavuta tu pumzi na matumaini ya kujiendeleza kijamii, kisiasa na kiuchumi ni finyu sana kwenye tawala za kijinga kama hizi.

Kuna signature ya Mkuu mmoja hapa inasema ''miafrika ndivyo tulivyo''. Ni aibu. Na huyu mama si ndo kapata na Nobel Prize? Au ndo ''Tembo kalitia maji'' baada ya kupata misifa kemkem. Inatia hasira!
 
jk unajifunza nini kwa mwanamama huyu?
huyo mama anacheza sarakasi,yaani kaona watu wameanza kumsakama yeye kwa kuwapa vyeo vya bure wanawe ,sasa kaona anapigiwa kelele kaona ngoja acheze mazingaombwe kwa kutangaza kumsimamisha mwanawe,yote hiyo ni funika kombe,kwanza kwa nini awateuwanawe kwenye nyadhifa nyeti,hapo hamuoni mgongano wa kimaslahi.viongozi wa kiafrika wamezidi ubinafsi,wote ni walewale ,hupenda kujinufaisha wao tu na familia zao.sifa kuu za kila raisi katika bara hili ni kujinufaisha kwanza yeye,familia yake na jamaaa zake
 
Back
Top Bottom