Rais wa Liberia amsimamisha kazi mwanae

MAKOLE

JF-Expert Member
Feb 5, 2012
618
280
Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf, amemsimamisha kazi mmoja wa watoto wake wa kiume kutoka ngazi ya unaibu gavana wa benki kuu ya nchi hiyo kwa kushindwa kuorodhesha mali zake katika tume ya kuzuia rushwa nchini humo.

Charles Sirleaf, ni miongoni mwa maafisa 46 waliosimamishwa kazi kwa kosa hilo.

Ni mmoja wa watoto wake watatu wa kiume aliowateua kushika vyeo vya juu kabisa baada ya kushinda muhula wa pili wa uchaguzi mwaka jana.

Wapinzani wa Bi Sirleaf wanamshutumu kwa kuendeleza upendeleo wa kindugu.

Rais huyo amemteua mtoto wake wa kiume Fumba kuwa mkuu idara ya usalama wa taifa, na kijana mwingine Robert kuwa mshauri mkuu na mwenyekiti wa kampuni ya mafuta inayomilikiwa na serikali-NOCAL.

Robert Sirleaf anayashitaki magazeti mawili nchini humo ya Independent na Analyst, na mwanasiasa wa upinzani Jefferson Kogie kwa kumkashifu kuwa amejinufaisha kifedha kutokana na vyeo alivyopewa.

Taarifa kutoka ofisi ya Bi Sirleaf imesema Charles Sirleaf na maafisa wengine 45 wataendelea kuwa wamesimamishwa kazi hadi hapo watakapoorodhesha mali zao kwa Tume ya Kuzuia Rushwa.

Maafisa wengine waliosimamishwa kazi ni pamoja na mkuu wa itifaki ya rais, David Anderson, Wakili mkuu na naibu waziri wa sheria Micah Wilkins Wright na naibu mkurugenzi mkuu wa utangazaji Ledgerhood Rennie.

Bi Sirleaf aliyeingia madarakani mwaka 2005 mwishoni mwa mgogoro wa vita Uliodumu miaka 14, amekuwa akiahidi mara kwa mara kupambana na rushwa na kustawisha utawala bora nchini Liberia.

Alitunukiwa tuzo ya amani ya Nobel mwaka jana, muda mfupi baada ya kuchaguliwa tena kwa muhula mwingine katika uchaguzi ulioghubikwa na tuhuma za udanganyifu katika zoezi la upigaji kura.

Rushwa bado inabakia kuwa kikwazo kikubwa nchini Liberia huku idadi kubwa ya watu wakiishi katika umasikini licha ya utajiri mkubwa wa madini nchini humo.

Mwezi Juni taasisi ya kimataifa ya Maafa-ICG, ilitoa ripoti kutahadharisha kuwa rushwa na upendeleo wa kindugu katika sekta mbalimbali vinaweza kuhatarisha demokrasia nchini humo

source: B.B.C 21 Agosti, 2012 - Saa 18:41 GMT
 
Hapo hakuna cha kujifunza. Naona kama kumsimamisha kazi mwanae ni danganya toto. Kama ameweza kuwateua wanae wote maana yake ni kwamba anatawala kidugu-nepotism. Tusidanganywe na neno kusimamisha kazi. Kimsingi, Afrika bado tuko mbali. Kwenye nchi za wenzetu huwezi kuwateua wanao hivyo na bado ukaendelea kuwa madarakani. Laiti kama wale watoto wangekuwa wamegombea na kushindwa kwa merits zao hakuna ambaye angeona makengeza kama haya. Sirleaf alimsaidia Taylor kuiharibu ile nchi ambayo naye anamalizia. Hana tofauti na Jakaya katika kutumia madaraka kunufaisha familia na marafiki zake.
 
Yaani alipowateua wanae haikuonekana habari, sasa kamsimamisha mwanae ambaye alimpa unaibu gavana wa benki kuu inaonekana big deal!!! Ukipewa ugavana wa benki kuu hata kwa miezi mitatu hata kama bila mshahara wala posho ni msaada tosha wa kukutoa kimaisha kwa sababu hiyo CV ukiiandika popote ni big deal.
 
Afrika sijui tuna nini, huyu mama naye kaishaingia kwenye kurithishana?
Yule wa Gambia ndiyo kituko cha hali ya juu.
 
Hapo hakuna cha kujifunza. Naona kama kumsimamisha kazi mwanae ni danganya toto. Kama ameweza kuwateua wanae wote maana yake ni kwamba anatawala kidugu-nepotism. Tusidanganywe na neno kusimamisha kazi. Kimsingi, Afrika bado tuko mbali. Kwenye nchi za wenzetu huwezi kuwateua wanao hivyo na bado ukaendelea kuwa madarakani. Laiti kama wale watoto wangekuwa wamegombea na kushindwa kwa merits zao hakuna ambaye angeona makengeza kama haya. Sirleaf alimsaidia Taylor kuiharibu ile nchi ambayo naye anamalizia. Hana tofauti na Jakaya katika kutumia madaraka kunufaisha familia na marafiki zake.
Huyu mama Mwiizii!. Hana cha kumfunza JK. Mama fisadi. ..... NEPOTISM au kwa kidhungu, ''UNDUGUNAIZESHENI" kama huu ni ushetani mbaya kabisa!.. Siwezi kamwe kumwita mama huyu shujaa!..
 
Miafrika ndivyo tulivyo tu (Nyangi Ngabu.....a.k.a Julius).

Mama huyu naye ni bure tu. Atateuaje watoto wake tu kwenye nafasi zote nzuri wakati kuna raia wengine? Ina maana kuwa watoto wake ndio waliokuwa bora kuliko raia wengine?
 
jk unajifunza nini kwa mwanamama huyu?

Hapo kuna somo gani wakati aliwaweka wanawe. Soma katikati ya mstari, wala hajamwajibisha mwanae sana sana amefanya siasa kuwapoteza wananchi hasira zao zisifike mbali zaidi
 
Bila shaka anajaribu kupunguza lawama ya kuwapa madaraka wanae though she has not been fair during nomination,
 
Hapo hakuna cha kujifunza. Naona kama kumsimamisha kazi mwanae ni danganya toto. Kama ameweza kuwateua wanae wote maana yake ni kwamba anatawala kidugu-nepotism. Tusidanganywe na neno kusimamisha kazi. Kimsingi, Afrika bado tuko mbali. Kwenye nchi za wenzetu huwezi kuwateua wanao hivyo na bado ukaendelea kuwa madarakani. Laiti kama wale watoto wangekuwa wamegombea na kushindwa kwa merits zao hakuna ambaye angeona makengeza kama haya. Sirleaf alimsaidia Taylor kuiharibu ile nchi ambayo naye anamalizia. Hana tofauti na Jakaya katika kutumia madaraka kunufaisha familia na marafiki zake.
Ni kweli hakuna la kujifunza hapa. Kwanza hajamfukuza kazi, amemsimamisha na inawezekana kasharudi kazini baada ya kuorodhesha Mali zake. Kuwapa wanae watatu vyeo vya
 
Hapo hakuna cha kujifunza. Naona kama kumsimamisha kazi mwanae ni danganya toto. Kama ameweza kuwateua wanae wote maana yake ni kwamba anatawala kidugu-nepotism. Tusidanganywe na neno kusimamisha kazi. Kimsingi, Afrika bado tuko mbali. Kwenye nchi za wenzetu huwezi kuwateua wanao hivyo na bado ukaendelea kuwa madarakani. Laiti kama wale watoto wangekuwa wamegombea na kushindwa kwa merits zao hakuna ambaye angeona makengeza kama haya. Sirleaf alimsaidia Taylor kuiharibu ile nchi ambayo naye anamalizia. Hana tofauti na Jakaya katika kutumia madaraka kunufaisha familia na marafiki zake.
Ni kweli hakuna la kujifunza hapa. Kwanza hajamfukuza kazi, amemsimamisha na inawezekana kasharudi kazini baada ya kuorodhesha Mali zake. Kuwapa wanae watatu vyeo vya kuteuliwa ni ufisadi tosha
 
Back
Top Bottom