Rais wa Korea Kaskazini atumia Treni kwenda kukutana na Rais Trump

Nyie ndio hua mnahadithia watoto zenu eti mlienda hivo shule
FB_IMG_15510054880954572.jpg


Sent from my GT-I9300 using Tapatalk
 
kim muoga sana wa kutunguliwa huyo jamaa,lakini nadhani Train ni salama zaidi kuliko ndege,kwani train inakuwa pia imejaa walinzi,tofauti na ndege ambayo mtu mmoja tu mwenye MANPAD,akisimama kilimani anakutungua bila shida
 
Kim ndo kiboko ya mashoga wote, kuanzia Tel Aviv, London hadi Washington DC.
Huyu hana ukiboko wowote.Ni sawa na juhudi za watu wazima kujaribu kumtuliza mtoto mtukutu aliyeshika panga ili kumpokonya kistaarabu na kuepusha madhara makubwa tu.Umiliki wa silaha za nyuklia si mzuri na haufai kwa nchi yoyote kuwa nazo.Ila walao kuna nchi ambazo,matumizi ya baadhi ya silaha (na hata uanzishwaji tu wa vita) hadi kuidhinishwa,ni mlolongo mrefu na mgumu na hauumpi kiurahisi mamlaka rais wa nchi kutumia ukuu wake kimihemko tu.Kwa upande wa pili,kuna nchi ambazo mifumo yao si tu kuwa,rais anaweza kudeka hata kuua mjomba wake hadharani,lakini pia akiamka aweza kuamua kila mwanaume anyoe staili gani,na wanawake waweje-Hizi nchi,ndio zastahili kuwa za kwanza kabisa kwenye list ya kuzuiwa umiliki wa silaha kwani ndizo nchi hatari zaidi.Hashindwi kuamka asubuhi na kujiamulia lifyatuliwe tu kuelekea upande alioamkia vibaya.Atakayehoji nae ni mhanga wa kwanza kushughulikiwa hadharani kwa kunyongwa kwa silaha ya kutungulia ndege.Baada ya vinchi vya kibedui kama hivi,ndipo hatimae zifuate zingine kama USA,Urusi n.k..Hakuna mzuri katika hili,ila kuna kuzidiana ubaya kimifumo na uongozi kuhusu silaha zenyewe.
 
Huyu Jamaa sijui watatumia mbinu gani kumshawishi aache kutengeneza silaha za Nyuklia...
Trump anasema Korea Kaskazini ikiacha kutengeneza silaha za Nyuklia ina fursa kubwa ya kujenga uchumi wake na kuwa miongoni mwa Nchi tajiri..Ila navyomjua Huyu Jamaa Kim Jong Un yamemwingia sikio la kulia na kutokea la kushoto..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom