Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta kuwa mgeni rasmi katika Sherehe za Uhuru

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuanza ziara rasmi ya siku mbili nchini Tanzania kuanzia kesho, Desemba 9 ambapo atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za uhuru wa Tanzania Bara zitakazofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Jumatano Desemba 8, Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Dan Kazungu amesema Rais Kenyatta atakuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za uhuru kufuatia mwaliko wa Rais Samia Suluhu Hassan alioutoa Mei 2021 alipofanya ziara nchini Kenya.

"Hii itakuwa mara ya kwanza kwa Rais Kenyatta kufanya ziara rasmi hapa Tanzania. Amekuja mara kadhaa kikazi lakini hakuwahi kufanya ziara rasmi. Kwa hiyo, ziara hiyo itaanza kesho kwa kushiriki katika sherehe za uhuru," amesema.

Siku ya pili ya ziara yake, Balozi Kazungu amesema Rais Kenyatta na Rais Samia watashuhudia utiaji saini wa mikataba minane ya makubaliano ambayo itahusisha masuala mbalimbali.

Amesema Rais Kenyatta ataambatana na ujumbe wa mawaziri watano ambao ni Waziri wa Mambo ya Nje, Waziri wa Biashara na Viwanda, Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano, Waziri wa Afya na Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Balozi Kazungu amesema wakati wa ziara ya Rais Samia nchini Kenya, viongozi hao walikubaliana kutatua changamoto mbalimbali ambazo zilikuwa zikitatiza uhusiano baina na mataifa hayo.

Amesema walianza kutatua changamoto hizo na walibaini kero 64 katika uhusiano wa Kenya na Tanzania na katika kipindi cha miezi minne, wameweza kutatua kero 46.

"Kero 18 zilizobaki ni zile za kiutawala kwenye taasisi zetu kama vile KRA na TRA (Mamlaka za Mapato za Kenya na Tanzania). Hata hivyo, kero hizo zinaendelea kutatuliwa," amesema Balozi Kazungu

Chanzo: Mwananchi
 
Sherehe hizi zinaweza kuteketeza zaidi ya Shilingi Bilioni Tano. (5,000,000,000/=) kwa kugonga mvinyo, kuku na posho, Wakati walioezuliwa nyumba na mvua kule sumbawanga wanahitaji chini ya Bilioni ili kurejea katika maisha ya kawaida na wanaambiwa serikali haina fedha.

Maisha wakati mwingine sio fair kabisa!
Na matunda ya Uhuru yanaaguliwa zaidi na watu fulani!
 
Sherehe hizi zinaweza kuteketeza zaidi ya Shilingi Bilioni Tano. (5,000,000,000/=) kwa kugonga mvinyo, kuku na posho, Wakati walioezuliwa nyumba na mvua kule sumbawanga wanahitaji chini ya Bilioni ili kurejea katika maisha ya kawaida na wanaambiwa serikali haina fedha.

Maisha wakati mwingine sio fair kabisa!
Na matunda ya Uhuru yanaaguliwa zaidi na watu fulani!
Yule mwingine alisema hatufanyi sherehe za Uhuru hela zitaenda kujenga barabara,juzi tumeonyeshwa kumbe hio barabara imejengwa kwa pesa za mabeberu wa kijapan.

CCM Ni ile Ile.
 
Inasikitisha sana kuona taarifa kama hii inatolewa na Ubalozi wa Nchi ya Kigeni badala Wizara Yetu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
 
Miaka iliyopita hii isingeeleweka kabisa! Mahusiano ya nchi hizi yamekuwa ya mashaka mashaka sana toka enzi za nyang'au. Naona SSH anaelekea uelekeo mwingine kabisa.
 
Back
Top Bottom