Rais wa Kenya akifariki akiwa madarakani Katiba inasemaje? Utulivu Utakuwepo?

Kenya ndio taifa la kwanza EAC kumpoteza rais akiwa madarakani, na uongozi ulipokezwa kwa makamu wake na nchi ikaaendelea.

Katiba iko wazi kwamba akifa rais, naibu wake atachukua uongozi na kukamilisha hatamu ya awamu, ikishindikana kwa naibu, kama ikitokea naye labda aidha kafa au ana matatizo, basi spika anaukwaa ila kwa siku sitini kabla kuingia kwenye uchaguzi wa kitaifa.... 146. Vacancy in the office of President - Kenya Law Reform Commission (KLRC)

Tunaomba rais wetu Uhuru awe makini asije naye akatusababishia msiba wa kitaifa wa kujitakia kwa ukaidi, aendelee kuvaa barakoa na kuchukua tahadhari zote.
Nasikia Luo Community na BBI ndio inamuweka raisi wa Kenya madarakani.....
 
Nasikia Luo Community na BBI ndio inamuweka raisi wa Kenya madarakani.....

katiba ndio imemuweka rais madarakani, na pia uhai wake kwa maana hafanyi pumba za kijinga za kupuuza mbinu za kisayansi na kujisababishia msiba wa kujitakia.....

Hawa wote wanavaa barakoa maana wanatumia akili na mpaka leo wako hai, hawapo radhi kusababishia mataifa yao misiba ya kijinga

Museveni-with-mask-being-welcomed-by-Magufuli.jpg

2720559_jk.jpg

Signing.png

President-Kagame-chairing-a-cabinet-meeting-Friday.jpg
 
Kama ikitokea rais wa kenya afe sasa. kwanza kila mtu atakuwa anakimbizana kuhakikisha kikuyu haikamati madaraka. maana kinachoonekana ni kuwa nchi inaongozwa kama ufalme vile. Kama si kikuyu wewe huwezi kuwa rais. uchaguzi wa mwaka huu utakuwa na kimbembe sana.
 
Bado haujajibu swali. Leo hii akifa Uhuru, Ruto ataruhusiwa kuongoza nchi?
Kama hujui kusoma na kuelewa tueleze

Umeshaelezwa ya Kenyatta akifa enzi zile ambazo Africa ilikua hatujazoea democrasia...

Alafu mwaka wa 2014, Rais Uhuru Kenyatta, kabla kuenda kwa kesi ya ICC kule Hague, alijiondoa madarakani kwa wiki moja na ndani ya hio wiki moja, Naibu wake Ruto alikua ndo rais wa nchi.... Kwahivyo haya mambo so mageni kwetu... Kunawezekana kukawa na tension flani lakini mwisho wa siku katiba itafatwa.

Hapo nimehighlight utapata jibu.
 
Kama hujui kusoma na kuelewa tueleze

Hapo nimehighlight utapata jibu.

Unaeleza mambo ya kipindi ambacho hata hukuwa umezaliwa.
Wee unafikiri katiba ndiyo ulinzi? nchi zote zina katiba, ambalo ni jambo moja, lkn kuifuata ni jambo lingine. Si unaona hiyo katiba yenu inavyokanyagwa, lkn hakuna wa kumpinga rais wenu???
 
Hayo yote uliosema ndiyo yapo kwenye mioyo ya wakenya. Hata sasa Uhuru akiondoka, hafikirii kumuachia Ruto kama yalivyokuwa makubaliano ndani ya jubilee. Ona sasa Uhuru na Raila wanamzunguka Ruto. Hawataki akisogelee kiti cha ufalme.
🤣🤣🤣
Naona ameamua aanzie kwa majaji.
Kwani UK na RAO ndio watakaopiga kura? 😂
 
Alipokufa kenyatta moi hakuongozaee, nyie watu wanafiki sana..
Au unafikiria ilikua hatujui mataga mlikua mnapanga njama za kutompa mama uenyekiti wa CCM
Hakujawahi kuwa na njma zozote za kutompa Madaraka SSH, Hakujawahi kuwa na kikao chochote au kikundi chochote kilicholeta hoja ya kupinga SSH kupewa uenyekeiti.
Uteuzi wa Mpango kama VP ulifanywa na SSH mwenyewe baada ya kupendekezewa majina na si vinginevyo.
 
Kenya ndio taifa la kwanza EAC kumpoteza rais akiwa madarakani, na uongozi ulipokezwa kwa makamu wake na nchi ikaaendelea.

Katiba iko wazi kwamba akifa rais, naibu wake atachukua uongozi na kukamilisha hatamu ya awamu, ikishindikana kwa naibu, kama ikitokea naye labda aidha kafa au ana matatizo, basi spika anaukwaa ila kwa siku sitini kabla kuingia kwenye uchaguzi wa kitaifa.... 146. Vacancy in the office of President - Kenya Law Reform Commission (KLRC)

Tunaomba rais wetu Uhuru awe makini asije naye akatusababishia msiba wa kitaifa wa kujitakia kwa ukaidi, aendelee kuvaa barakoa na kuchukua tahadhari zote.
Karume aliyefariki 1972 nadhani alikuwa mkuu wa wilaya
 
Unaeleza mambo ya kipindi ambacho hata hukuwa umezaliwa.
Wee unafikiri katiba ndiyo ulinzi? nchi zote zina katiba, ambalo ni jambo moja, lkn kuifuata ni jambo lingine. Si unaona hiyo katiba yenu inavyokanyagwa, lkn hakuna wa kumpinga rais wenu???
Raisi wetu hajapingwa nini? Hebu nionyeshe ni mara ngapi Katiba/mahakama imempinga au kumkosoa rais wazi wazi huko Tanzania kama vile inavyofanyika Kenya? My friend, mambo yanayofanyika Kenya hauyawezi, yakitokea Tz mtashindwa.... Hebu imagine JPM angefuta watu kazi alafu mahakama ipinge na iwaregeshe hao mafisa kazini, mtu kama JPM angekubali kweli?
 
Kuna watu wanaitwaga mudavadi, musyoka, kijana wamalwa nk utawasikia wakati wa kampeni na vyama vya ajabu ajabu vipya
ndio demokrasia hio au sio?
ama pengine ulitaka tuwe nchi ya chama kimoja ka sisiemu?
nchi ambayo haina upinzani? kwamba hakuna wa kumpinga mkulu na atakayekuwa na mawazo tofauti na yake basi sio mzalendo?
nchi ambayo wananchi wake wanaongozwa kama mandondocha?

mkuu, naomba ujitafakari kidogo.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom