Rais wa Chad: 'Fisadi mwingine'

Richard

JF-Expert Member
Oct 23, 2006
14,939
20,395
Siku ya Jumamosi tarehe2 mwezi February mwaka huu majeshi ya uasi yalifika katika mji mkuu wa Chad N'Djamena wakiwa na maroli na silaha za nguvu. Wakiwa hapo palitokea vita kali kati yao na majeshi ya serikali yaliyokuwa yakisaidiwa na majeshi ya Ufaransa na baada ya hapo watu 160 walikuwa wameuawa na 1000 kujeruhiwa. Hio si idadi kamili ingawa imeripotiwa kuwepo kwa maiti zaidi za binadamu na majeruhi.

Jumanne tarehe 5 kukawa na habari kuwa waasi wamerudishwa nyuma na kuondolewa mjini N'Djamena na Rais Idris Deby Itno ametulia Ikulu na kwamba waasi wamekubali kusitisha mapigano tena baada ya mkwara wa "Jumuiya ya Kimataifa" .

Mapigano hayo yaliosababisha raia wengi kukimbilia nchi jirani ya Cameroon na wale wa kigeni kuokolewa na majeshi ya Ufaransa ambayo yana makazi mjini N'Djamena.

Majeshi ya uasi yanajumuisha makundi matatu ya Union of Democratic Forces (UFDD), wanaoongozwa na Mahamat Nouri, RFC (Rally of Forces for Change) wa Timan Erdimi, na UFDD-Fundamental waongozwao na Abdelwahid Aboud Makaye. Ingawa makundi haya yanajumuisha makabila tofauti lakini mwezi December mwaka jana waliungana kwa kauli moja kuunda umoja wenye nguvu kwa baraka za serikali ya Sudan ili kupigana na majeshi ya serikali ya Chad ambayo inafadhili shughuli za waasi wa Darfur.

Sababu kubwa ya ugomvi huu ni kitendo cha serikali ya Chad kukaribisha majeshi ya kulinda amani kutoka Ulaya yakiongozwa na Ufaransa EUFOR kwa upande wa mashariki mwa Chad na karibu na Darfur.

Waasi wamechukizwa na kitendo cha serikali ya Chad cha kuhujumu mapato yanayotokana na mauzo ya mafuta nje ya Chad kupitia bomba la mfuta linalokwenda nchini Cameroon na hivo kutoona fwedha yoyote ikinufaisha nchi na wananchi kwa ujumla.

Raisi huyu fisadi bwana Deby amekalia kuti kavu la ikulu akiwa analindwa na majeshi ya Ufaransa huku akifaidi matunda ya ufisadi tangu mwaka 1990 alipopundua serikali. Majeshi ya Ufaransa yapo nchini Chad tangu mwaka 1986.
Amepona chaguzi mbili mwaka 1996 na 2001 ambazo anatuhumiwa kuvuruga kura na amepona pia kupinduliwa mwaka 2004.

Watu milioni nane kati ya kumi nchini humo wanaishi kwa dola moja kwa siku! Na wanasiasa karibu wote ni wa kutoka katika kabila la wazaghawa la raisi Deby na ndio wametawala siasa za Chad tangu nchi hio ipate uhuru wake wa bendera.

Cha kushangaza zaidi ni kwamba viongozi wawili wa uasi bwana Timam Erdimi na bwana Abdelwahid Aboud Makaye ni binamu na waliwahi kuongoza wizara mbili za pamba na mafuta! Na pia wanandugu wengi wa bwana Deby wamo katika makundi ya uasi wakidai haki itendeke na mpaka kieleweke kuhusu mstakabali wa keki ya taifa la Chad.

Chad ina zao kuu la pamba, mafuta na ardhi nzuri upande wa maashariki mwa nchi hio tosha kabisa kuwafanza wana wa nchi hio waneemeke na utajiri huo.

Inaripotiwa kwamba Chad inachimba kiasi cha 160,000 mapipa kwa siku (kama sikosei) na kuna matenki yenye thamani ya 1.5 bilioni ya mafuta machafu (crude oil) na kwa mtazamo wa soko la dunia kwa sasa mapato ya mauzo ya mafuta hayo yanawatajirisha wana wa nchi ya Chad kwa miundo mbinu, makazi, watoto kwenda shule na kadhalika.

Lakini kwa ufisadi wa raisi Deby amekuwa akitumia mapato yatokanayo na mafuta kununua silaha za kujilinda na kuneemesha familia yake, marafiki na jamaa na sasa waasi wanakata mgao wao. Kwa hio matumizi makubwa ya kijeshi na ufisadi ndio silaha kwa wananchi maskini wasio na hatia wa Chad.

Ufisadi Ufisadi... ni nini kifanyike sijui!
 
Pamoja na kuwa Ufaransa imekuwa mstari wa mbele kumtetea Derb lakini duru zinaoneesha pia juu ya ushiriki wa China katika kuwa support hawa waasi kutipitia Sudan amabko pia China inashutumniwa katika ku supply silaha.
Chad ni mfano tuu mdogo wa jinsi jumuiya ya kimataifa esp. developed nations zinavyofaidi na migogoro ya Africa, lakini pamoja na ukweli kwamba nchi zilizoendelea zinahusika kwa kiasi kikubwa ktk ku foster vita Africa ukweli na swali la kimsingi litabaki pale pale kwanini viongozi wetu wa Kiafrica wanakublai kutumika kihivyo for the expense ya mamia ya wananchi wake wakifa?
Recently nasoma kitabu, ''comprehanding and mastering African Conflicts'' Editored by Prof. Adeju Adebayo, it worth reading it, coz inakupa mwanga mkubwa sana wa Sub Sahara conflicts na utagundua ni jinsi gani developed nations zimechangia sana na zinaendelea kuchangia migororo mbalimbali barani africa!
 
Back
Top Bottom