Rais wa Burundi kufanya ziara ya siku 3 nchini

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,482
9,242
Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye, anatarajiwa kuwasili nchini kwa ziara ya Kitaifa ya siku tatu kuanzia tarehe 22 hadi 24 Oktoba, 2021.

Akiongea na Waandishi wa Habari ofisini kwake jijini Dodoma, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Liberata Mulamula amesema Mhe. Rais Ndayishimiye atawasili katika uwanja wa ndege wa Dodoma tarehe 22 Oktoba na kuelekea Ikulu ya Chamwino ambako atapokelewa rasmi na mwenyeji wake, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan.

Mhe. Waziri Mulamula amesema baada ya kuwasili Ikulu ya Chamwino, Rais Ndayishimiye atakagua gwaride la heshima na kupigiwa mizinga 21 kwa heshima yake na baadae viongozi hao watakuwa na mazungumzo ya faragha na kufuatiwa na mazungumzo rasmi.

Balozi Mulamula amesema akiwa jijini Dodoma tarehe 22 Oktoba mchana, Mhe. Rais Ndayishimiye atatembelea na kuweka jiwe la msingi katika kiwanda cha kuzalisha mbolea ya asili yenye mchanganyiko wa madini ya phosphate na samadi kinachojengwa katika eneo la viwanda la Nala, kiwanda ambacho kinajengwa na Wawekezaji wa kampuni ya Itracom Fertilizers Limited (ITRACOM) kutoka nchini Burundi na baadaye jioni atahudhuria dhifa ya kitaifa itakayofanyika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Balozi Mulamula ameongeza kuwa tarehe 23 Oktoba 2021 Mhe. Rais Ndayishimiye ataelekea Zanzibar ambako atapokelewa na Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi na kuwa na mazungumzo na mwenyeji wake huyo na baadaye ataelelekea Mkoani Dar es Salaam ambapo ataungana na mwenyeji wake Mhe. Rais Samia.

Amesema akiwa jijini Dar es Salaam Rais Ndayishimiye anatarajiwa kutembelea Bandari ya Dar es Salaam na kukagua ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) unaoendelea nchini kutokea stesheni ya Dar es salaam hadi stesheni ya Kwala - Ruvu pamoja na kutembelea bandari kavu ya Kwala inayojengwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania katika eneo hilo la Kwala mkoani Pwani ili kujionea maendeleo ya ujenzi wa bandari kavu hiyo.
 
alipikuwa kigoma alimuita sana baba, mzee na kila sifa alimwagia mwendazake.


natarajia mama ataitamka mara nyingi kuliko Burundi
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom