Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye awasili nchini Tanzania kuanza Ziara ya siku 3

22 October 2021
Dodoma Tanzania
ITRACOM FERTILISERS LIMITED imeweka jiwe la msingi ishara kuwa shughuli za ujenzi za kiwanda zimeanza rasmi



Itracom fertilisers ni kiwanda cha ITRACOM kupitia kiwanda mama cha kutengeneza mbolea FOMI fertilisant Organo Mineral Accueil - FOMI cha nchini Burundi na kimepata kibali na kimerasimisha shughuli za ujenzi wa kiwanda kwa kufungua tawi la kiwanda chake nchini Tanzani.

Mgeni rasmi katika shughuli za kuweka jiwe la msingi,zimehudhuriwa na Mh. Rais wa jamhuri ya Burundi Evariste NDAYISHIMIYE .kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kiasi gani ? kitaajiri wafanyakazi wangapi ?ni manufaa yapi kwa nchi ya Burundi.
Source : Mashariki TV

Itracom is a subsidiary of the Burundi based FOMI.
It is anticipated that the Dodoma factory will be a saviour to Tanzanian farmers, considering the fact that the $180 million investment will not only employ 3,000 people but upon completion of the ongoing construction, it will have the capacity of producing 600,000 tonnes of natural fertiliser per year. Construction will be completed in August 2022.


More info :

Bujumbura, Burundi

FOMI is an organo-mineral fertilizer and agricultural lime manufacturing plant. It is located on the National Road N ° 5, 9km from downtown Bujumbura not far from the international airport.


Source: FOMI Burundi

First organo-mineral fertilizer manufacturing plant in Burundi and among the few that exist in the sub-region, FOMI wants to be one of the major producers of organo-mineral fertilizers. FOMI also produces agricultural lime.

FOMI is committed to protecting the environment and investing in research for development in order to provide innovative technologies.

Source : Accueil - FOMI
 
22 October 2021

KUMEKUCHA: Ujio wa Rais wa Burundi Tanzania na Fursa za Kiuchumi

Uwekezaji wa kiwanda eneo la viwanda NALA Dodoma, Bandari kavu Kwala, Pwani Tanzania. Bandari ya Dar es Salaam , usafiri wa reli na barabara, biashara ya kuvuka mipaka, nafasi za kutengeneza ajira zaidi n.k

Source: ITV Tanzania
 
Mwekezaji ni yeye....kutoka Urundi
Kwaio anakuja kukagua na kuzindua miradi ya TZ?

Nlijua wangezindua joint projects za nchi mbili, sa kiwanda cha mbolea kinamuhusu nini? au ndio kuextend ziara. Kwa wenzetu haya mambo huyaoni
Mwekezaji ni yeye kutoka Urundi Empire
 
Nimekumwambia hata Uganda M7 alimtumia ndege kumfuata Burundi. Kwa hio Ni mambo ya kawaida kabisa hayo.
Air Uganda iliyombeba to Uganda ni commercial flight kama ATC/KQ hii iliyombeba ni special aircraft ya Rais wa TZ, ambayo
hata Museveni has the same Aircraft.hapo ndio utofauti and the special way we treated him.
 
Dr. LIBERATA MULAMULA - NEEMA KUPATIKANA ZIARA YA RAIS WA BURUNDI NCHINI TANZANIA


RAIS wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku tatu hapa nchini kuanzia kesho kutwa October 22 hadi 24 ambapo pamoja na mambo mengine ataweka jiwe la msingi kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha mbolea ya asili isiyo na kemikali cha INTRACOM Fertilizer kinachojengwa na wawekezaji kutoka Burundi. Waziri wa mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akitoa taarifa jijini Dodoma juu ya ziara hiyo ameeleza kuwa Mhe. Rais Ndayishimiye ataanzia katika Mkoa wa Dodoma kisha kuelekea Zanzibar na Hatimaye Dar es Salaam kabla ya kurejea nchini kwake. Balozi Mulamula ameeleza kuwa Mhe. Rais Ndayishimiye akiwa jijini Dodoma ataweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha mbolea cha INTRACOM Fertilizer ambacho baada ya kukamilika mwezi Julai mwaka 2022 kitazalisha tani laki tano za mbolea. Akiwa visiwani Zanzibar Rais Ndayishimiye atafanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ally Mwinyi kabla ya kurejea Dar es salaam na kuutembelea mradi war reli ya Kisasa SGR sambamba na ujenzi wa bandari kavu ya Kwala iliyoko Ruvu mkoa wa Pwani Ziara ya Rais Ndayishimiye hapa nchini ni matokeo ya ushirikiano mzuri kati ya Tanzania na Burundi ambapo itakumbukwa kuwa mwezi Julai rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alifanya ziara ya siku mbili katika nchi hiyo
source : PRESENTER JIMMY

 
Burundi yaomba eneo la kulima miwa wazalishe sukari. Yashukuru juhudi za Tanzania kuchagiza jumuiya za kimataifa kuondoa vikwazo kwa nchi ya Burundi. Burundi yasifia moyo wa kuwapa makazi na uraia kwa wakimbizi waliokimbia Burundi miaka ya 1972 na 1993

Hotuba nzima ya Mh. Rais Evariste Ndayishimiye wa Burundi



Source :ISHAMI TV
 
Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evariste Ndayishimiye, amewasili nchini kwa ziara ya Kitaifa ya siku (3) kuanzia leo tarehe 22 hadi 24 Oktoba, 2021.

Mhe. Ndayishimiyeamepokelewa na mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan, Jijini Dodoma.

Atatembelea na kuweka Jiwe la Msingi katika Kiwanda cha kuzalisha Mbolea ya Asili kinachojengwa Nala, Dodoma.

Ujirani mwema
 
Back
Top Bottom