Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,005
- 9,872
Imesalia miezi minne kabla ya uchaguzi wa urais nchini Burundi, uchaguzi ambao rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amebainisha mara kadhaa kwamba hatawania.
Hayo yanajiri wakati Bunge la nchi hiyo limeidhinisha sheria inatakayompa rais Nkurunziza kitita cha faranga Burundi bilioni moja sawa na Dola laki 5 za Marekani atakapostaafu.
Hata hivyo upinzani umelalama na kusema fedha hizo ni nyingie mno.
Pia Bunge la Burundi limepitisha muswada wa sheria unaompa rais Pierre Nkurunziza cheo cha "Kiongozi Mkuu".
Sheria hiyo iliyotetewa bungeni na Waziri wa Sheria Aime Laurentine Kanyana, inaagiza pia Rais atakapostaafu kuchukuliwa kwa hadhi ya makamu wa rais kwa kipindi cha miaka 7.
Muswada huo wa sheria pia utamuwezesha kulipwa mshahara katika kipindi chote cha maisha yake, kupata marupurupu yote anayopewa makamu wa rais aliyeko mamlakani na atapewa nyumba ya kifahari, anayopewa kila rais wa Burundi aliyechaguliwa kidemokrasia.