Rais wa Bunge la Afrika akutwa na kesi ya kujibu tuhuma za unyanyasi wa kingono, umoja wa Afrika kuchukua hatua

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
21,713
35,518
Ndugai vipi umeipata hii?..kama ulipewa fungu aibu yako.

Hatimaye Kamati Maalumu iliyoundwa na Wabunge wa Bunge la Afrika (Pan- African Parliament – PAP) imetoa ripoti ya uchunguzi dhidi ya Rais wa Bunge hilo,Mhe. Roger Nkodo Dang.

Nkodo anatuhumiwa kwa unyanyasi wa kingono kwa watumishi wa kike walioko Makao Makuu ya PAP,matumizi mabaya ya madaraka, upendeleo dani ya bunge hilo na unyanyasaji kwa watumishi wa ofisi hiyo hali iliyosababisha kuwepo kwa mgomo wa watumishi wiki iliyopita.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Maalumu ya Uchunguzi,Jaji mstaafu wa mahakamani kuu ya kenya Mh Stewart Madzayo ametoa ripoti hiyo leo jioni katika kikao cha bunge kikiongozwa na Makamu wa nne wa rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Chief Charumbira.

Ripoti ya kamati hiyo imeonesha kuwa Rais wa PAP, Nkodo Dang amekutwa na kesi ya kujibu na hivyo wabunge wa wameazimia kuikabidhi Umoja wa Mataifa (AU) kwa ajili ya uchunguzi wa kina(forensic investigation)ambapo Rais huyo ametakiwa apishe ili uchunguzi uweze kufanyika.

Akizungumza na waandishi wa habari,baada ya kutoka kwenye kikao cha bunge ambacho waandishi wa habari hawakuruhusiwa,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Stephen Masele amesema Kamati hiyo imefanya kazi nzuri.

*“Kwanza Nimefurahi kwamba Kamati Maalumu iliyoundwa na Bunge kuchunguza tuhuma dhidi ya rais wa PAP anazotuhumiwa imefanya kazi vizuri”,*

*“Na mimi kama mkuu wa Utawala wa Bunge la Afrika na wafanyakazi wote wa PAP, nina wajibu wa kuhakikisha kwamba haki za wafanyakazi hususani wanawake ambao wanamtuhumu rais kwa kuwanyanyasa kingono zinalindwa”*,amesema Masele.

*“Utafiti wa Kamati umethibitisha kuwa alifanya hivyo na yeye mwenyewe amekiri kuwa alifanya na ameomba msamaha,Bunge limeazimia asimamishwe kupisha Umoja wa Afrika ufanye uchunguzi wa kina”*
 
Hatimaye Rais wa Bunge la Africa (Pan African Parliament-PAP) bwana Roger Dang akutwa na hatia ya unyanyasaji wa kingono kwa wafanyakazi wa Bunge hilo. Hongera mheshimiwa Stephen Masele kwa kuunda tume iliyochunguza hizi tuhuma. Umeipa Nchi yetu heshima kwenye hili Jambo. Sasa unaweza kurudi nyumbani kuitikia wito wa mheshimiwa speaker Job Ndugai.
 
Huoni lengo la ndugai limefeli ?
 
Basi sawa!
IMG-20190516-WA0014.jpeg
 
Ndugai vipi umeipata hii?..kama ulipewa fungu aibu yako.

Hatimaye Kamati Maalumu iliyoundwa na Wabunge wa Bunge la Afrika (Pan- African Parliament – PAP) imetoa ripoti ya uchunguzi dhidi ya Rais wa Bunge hilo,Mhe. Roger Nkodo Dang.

Nkodo anatuhumiwa kwa unyanyasi wa kingono kwa watumishi wa kike walioko Makao Makuu ya PAP,matumizi mabaya ya madaraka, upendeleo dani ya bunge hilo na unyanyasaji kwa watumishi wa ofisi hiyo hali iliyosababisha kuwepo kwa mgomo wa watumishi wiki iliyopita.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Maalumu ya Uchunguzi,Jaji mstaafu wa mahakamani kuu ya kenya Mh Stewart Madzayo ametoa ripoti hiyo leo jioni katika kikao cha bunge kikiongozwa na Makamu wa nne wa rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Chief Charumbira.

Ripoti ya kamati hiyo imeonesha kuwa Rais wa PAP, Nkodo Dang amekutwa na kesi ya kujibu na hivyo wabunge wa wameazimia kuikabidhi Umoja wa Mataifa (AU) kwa ajili ya uchunguzi wa kina(forensic investigation)ambapo Rais huyo ametakiwa apishe ili uchunguzi uweze kufanyika.

Akizungumza na waandishi wa habari,baada ya kutoka kwenye kikao cha bunge ambacho waandishi wa habari hawakuruhusiwa,Makamu wa Kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika,Mhe. Stephen Masele amesema Kamati hiyo imefanya kazi nzuri.

*“Kwanza Nimefurahi kwamba Kamati Maalumu iliyoundwa na Bunge kuchunguza tuhuma dhidi ya rais wa PAP anazotuhumiwa imefanya kazi vizuri”,*

*“Na mimi kama mkuu wa Utawala wa Bunge la Afrika na wafanyakazi wote wa PAP, nina wajibu wa kuhakikisha kwamba haki za wafanyakazi hususani wanawake ambao wanamtuhumu rais kwa kuwanyanyasa kingono zinalindwa”*,amesema Masele.

*“Utafiti wa Kamati umethibitisha kuwa alifanya hivyo na yeye mwenyewe amekiri kuwa alifanya na ameomba msamaha,Bunge limeazimia asimamishwe kupisha Umoja wa Afrika ufanye uchunguzi wa kina”*
Unoja wa mataifa (UN) , umoja wa Africa (AU)
 
Ni aibu kweli kwa Taifa.

Hii ni kashfa mpya ya Uongozi.

Inavyoelekea kulikuwa na mawasiliano kati ya wale madhaifu na wale waliojichimbia chini sana.

Kwa maana yule msukuma wa kahama kwenye twiter zake inaonekana alikuwa akishawishiwa kitu na wale waliojichimia chini sana mchangani ili kuzima kashfa hii.

Sasa huyu msukuma wa kahama ameshinda.

Najiuliza tu hivi ikitokea akabaininsha vitisho na ushahidi wa barua ya spika kumfuta ubunge wa Bunge la Afrika.

Si Taifa linapata aibu kubwa.
 
Back
Top Bottom