Rais wa Brazil kuchunguzwa kutokana na jinsi anavyopambana na corona

Sam Gidori

Verified Member
Sep 7, 2020
93
150
Mahakama Kuu nchini Brazil imeamuru Baraza la Senate kuchunguza jinsi serikali ya nchi hiyo ilivyodhibiti maambukizi ya virusi vya corona, huku ikikataza makanisa kufunguliwa na kuzidisha uwezekano wa kuongeza mvutano baina ya Rais Jair Bolsonaro na mhimili wa mahakama.
Uchunguzi huo utahusisha wanasayansi kutoka kote nchini humo kuonesha ni kwa jinsi gani Rais alivyoonesha uzembe katika utendaji wake na kauli zake.

Kabla ya amri ya Mahakama Kuu, baraza la Senate lilikwishasaini barua ya kutaka kuanzishwa kwa uchunguzi, lakini hatua yao ilikwamishwa na Rais wa Baraza hilo, Seneta Rodrigo Pacheo ambaye aliwekwa madarakani mwezi Januari kwa ushawishi wa Rais Bolsonaro. Ikiwa atakutwa na hatia, Baraza la Senate litamwomba Mwanasheria Mkuu kuanzisha uchunguzi wake.

Rais Bolsonaro anajulikana kwa misimamo yake mikali dhidi ya kujifungia ndani, na analaumiwa kwa kudharau njia za kisayansi za kupambana na maambukizi ya COVID19 katika nchi ya pili kuathiriwa zaidi na virusi hivyo ikishuhudia visa milioni 13.4 vya maambukizi na vifo 351,000. Katika siku za hivi karibuni, zaidi ya robo ya vifo vyote vinavyotokana na COVID19 duniani vimetokea nchini Brazil.

Chanzo: Huffpost
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom