Rais wa Brazil, Jair Bolsonaro atangaza kupata Corona

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,297
2,000
Kupitia chaneli ya Taifa, Rais Jair Bolsonaro (65) ametangaza kupata maambukizi ya #CoronaVirus baada ya kufanyiwa vipimo kwa mara ya nne siku ya Jumatatu kufuatia kuonesha dalili za ugonjwa huo

Bolsonaro amekuwa mara kwa mara akipuuza ugonjwa huo huku akiuita ni mafua madogo ya kawaida na kudai hawezi kuathirika kwa kiwango kikubwa na virusi hivyo

Aprili mwaka huu alisema "Hata nikiambukizwa virusi hivyo sitakuwa na wasiwasi kwasababu sitahisi chochote kwa maana itakuwa kama mafua madogo"

Aidha, mara kadhaa ameingia kwenya mgogoro na Magavana akiwashinikiza kulegeza masharti ya 'lockdown' na pia jana alilegeza masharti ya kuvaa barakoa kwa wananchi

Brazil ambayo ni ya pili kwa maambukizi ya #CoronaVirus, hadi leo imeripoti visa 1,628,283 huku kukiwa na jumla ya vifo 65,631 na waliopona wakifikia 1,072,229

Facebook(17).png
=========

Brazil's President Jair Bolsonaro has tested positive for coronavirus.

He took the test, his fourth, on Monday after developing symptoms, including a high temperature.

Mr Bolsonaro has repeatedly played down the risks posed by the virus, calling it "a little flu" and saying that he would not be seriously affected by it.

He has also urged regional governors to ease lockdowns, which he says hurt the economy, and on Monday he watered down regulations on wearing face masks.

Back in April, he said that even if he were to be infected with the virus, he would "not have to worry as I wouldn't feel anything, at most it would be like a little flue or a little cold".

When he made the remark, the number of Covid-19-related deaths was still under 3,000 and the number of infections was around 40,000.

But the numbers have skyrocket since then. As of Monday, the number of deaths was over 65,000 and infections were over 1.6m, second only to the United States.

Despite the rising numbers, President Bolsonaro has argued that regional lockdowns are having a more damaging effect than the virus itself, and accused the media of spreading panic and paranoia.
 

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
21,602
2,000
Bandugu huwa nawaambia hili ni tatizo la kisayansi na linahitaji suluhu la kisayansi, sio mikwara, au kuficha vichwa ardhini au kujichokea, lazima upambane, pima pima pima na uhusishe tahadhari.

Huyu rais wa Brazil amenukuliwa mara nyingi akikaidi ushauri wowote wa kisayansi na kusema corona inakuzwa na upinzani, mara akasema ni "small flu", hadi sasa hiki kirusi kinazidi kuua watu kwake huko japo kimya kimya, na kimemkuta yeye ndani ya ikulu. Pole zake.

Ikumbukwe kuna mwenzake wa Burundi keshajiendea zake mbele za haki na kuwaacha Warundi wanateseka kisa ukaidi wake.
Jameni muhimu sana tukachukua tahadhari, tusijichokee.
 

Mkikuyu- Akili timamu

JF-Expert Member
Feb 16, 2018
4,335
2,000
Corona sio tisho, iliingia hadi kwa mtoto wa magufuli na akapona.

Mjifunze kuishi na corona kama mnavyo ishi na vipindupindu.
 

joto la jiwe

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
19,057
2,000
Hapo Nairobi imeingia hadi Ikulu, lakini bado Jana ameamua kumuiga Magufuli kwa kulegeza masharti, sasa hivi hapo Kenya Magufuli anakubalika" next to God"
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
117,538
2,000
Corona haichagui Kingunge wala kapuku inacheza kote kote. Muulize Boris Johnson ilivyomfanya kazi MAKEKE yake yote yameisha baada ya covid kumchungulisha kaburi.
 

mjingamimi

JF-Expert Member
Aug 3, 2015
29,334
2,000
Wamekufa wakenya 164 kwa corona.
Ila hauwezi kusikia BBC wala DW WAKITANGAZA
Huyu bana kaacha kazi sasa anafuatilia habari za covid tu, jamani jirani badilika bora uwe unatumia hizo nguvu kulima hata sukuma wiki
 
  • Thanks
Reactions: mmh

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
21,602
2,000
Corona haichagui Kingunge wala kapuku inacheza kote kote. Muulize Boris Johnson ilivyomfanya kazi MAKEKE yake yote yameisha baada ya covid kumchungulisha kaburi.

Lakini nilimuona shujaa sana yule, yaani kuwa na kiongozi kama huyo kunahamasisha ushujaa na uzalendo.
 

Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
28,741
2,000
Aje Tanzania Apate Ujuzi Kwa Mtu Mheshimiwa Mmoja,
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania John Pombe Joseph Magufuli.

Ameitokomeza COVID 19 Sasa Hivi Tunachapa Kazi .
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom