Rais wa Brazil amjia juu rais wa ufaransa kuelekea vikao vya G-8

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
Rais wa Brazili amemkemea vikali Rais wa Ufaransa ambaye aliandika kwenye tweet yake kuwa vikao vya G7 vinavyokaa wiki hii kuwe na ajenda ya moto unaounguza mistu ya amazoni.

Rais wa Ufaransa ambaye atakuwa mwenyeji wa mkutano huo anajaribu kuzishawishi nchi za G7 ziingize ajenda hiyo ya moto kwani mistu inaungua ambapo yeye anasema chanzo ni rais wa Brazili kuruhusu kukata miti. Rais wa Brazil amemjia juu kwa kusema kuingiza agenda hii kwenye mkutano wa nchi hizi kubwa duniani ni kuendeleza ukoloni. Amesema Brazil ni sovereignty state haipaswi kuingiliwa mambo yake.

My take: Tusiruhusu Mabeberu kutuamulia mambo yetu ya kufanya ambayo lengo lao ni kutukwamisha. Nchi zote duniani zinazoendelea zisikubali kuburuzwa.
 
Haya mabeberu yameshazoea kunywa damu za watu basi hiyo tabia hawawezi sahau.
 
ni G7 sio G8. na huyo rais wa brasil maji yanakaribia kumfika shingoni huko kwao, yeye ndiye aliyepunguza bajeti ya uhifadhi wa misitu ya amazon, wajuvi wakamwambia unakosea mkuu, yeye akajifanya mjuaji.
 
ID za kanda ya ziwa ni laana kwa mustakabali wetu.
Rais wa Brazili amemkemea vikali Rais wa Ufaransa ambaye aliandika kwenye tweet yake kuwa vikao vya G8 vinavyokaa wiki hii kuwe na ajenda ya moto unaounguza mistu ya amazoni.

Rais wa Ufaransa ambaye atakuwa mwenyeji wa mkutano huo anajaribu kuzishawishi nchi za G8 ziingize ajenda hiyo ya moto kwani mistu inaungua ambapo yeye anasema chanzo ni rais wa Brazili kuruhusu kukata miti. Rais wa Brazil amemjia juu kwa kusema kuingiza agenda hii kwenye mkutano wa nchi hizi kubwa duniani ni kuendeleza ukoloni. Amesema Brazil ni sovereignty state haipaswi kuingiliwa mambo yake.

My take: Tusiruhusu Mabeberu kutuamulia mambo yetu ya kufanya ambayo lengo lao ni kutukwamisha. Nchi zote duniani zinazoendelea zisikubali kuburuzwa.
 
Katika hili la mazingira tunaowaita mabeberu wapo sahihi kabisa kuingilia ili kuzuia uharibifu

Msitu wa Amazon ukilindwa kutokana na uharibifu wa mazingira Ufaransa haifaidiki kitu, ila ukiharibiwa ni majanga kwa ekolojia ya ulimwengu mzima

Katika moja ya hotuba zake marehemu Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kua wazungu wanahaha kuyarudisha mazingira yao katika hali ya asili kama yalivyokua enzi na enzi za mababu zao lakini wameshindwa. Pamoja na elimu na utaalam wao wote wanaishia kuweka mazingira artificial

Akasema maranyingi anapokutana nao walikuwa wanamwambia watanzania na walimwengu wote wasijaribu kufanya kosa kama walilofanya wao.

Akaongeza kusema katika hilo wazungu walikua wanatoa ushauri kwa dhati kabisa bila hila, na wanakua tayari kusaidia kwa rasilimali fedha na utaalamu ili mazingira yahifadhiwe

Uharibifu unaofanyika misitu ya Amazon na Congo unatia uchungu sana
 
Back
Top Bottom