Rais wa Botswana, Mokgweetsi Masisi kufanya ziara nchini Tanzania kesho June 10, 2021

Toka 2015 hajawahi kukanyaga Rais toka Ulaya na Marekani why?
Unahisi akikanyaga ndio ukoo wako utaondokana na umasikini?

Hivi hii tabia ya wanachadema kuhisi kwamba maendeleo yenu yataletwa na wazungu inakuwaje yani?

Wao walitembelewa na nani mpaka wakawa hapo walipo?
 
Soma tu hata kichwa cha habari mkuu, hi dunia sio lazima uwajue viongozi wa mataifa yote, ndio maana kuna kujifunza.
Ungesoma kichwa cha habari halisi alichoandika mleta mada na sio hiki kilicho haririwa na wahariri ungenielewa.

Ndio maana walionijibu mwanzo walinipa majibu mazuri.
 
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Madame Samia Suluhu Hassan
Ameshafika Dar es Salaam Akitokea Dodoma
Tayari Kabisa Hiyo Kesho Kumpokea Mgeni Wake Jijini Dar es Salaam Kwa Ziara Ya Siku Mbili.

Dodoma Tulieni,Dar es Salaam Tuna Jambo Letu Na Mgeni
 
Hivi ni kweli huo mji mkuu wa Botswana Gaborone unatamkika Gabohone. Yani na sisi waafrika kwa Swagger tunawaiga mabeberu kwa mabeberu ufaransa na ujerumani W ni Z mfano Wenger Venger, Former Yugoslavia c ni ch mfano papic inatamkwa papich. Scandinavian ni Y mfano Jana Yana). Sweden A ni O mfano Adam Odom.Sam ah an I badala ya kuandika Botswana nikaandika Gaborone zilikuwa ndoto na mchana

Hivi ni kweli huo mji mkuu wa Botswana Gaborone unatamkika Gabohone. Yani na sisi waafrika kwa Swagger tunawaiga mabeberu kwa mabeberu ufaransa na ujerumani W ni Z mfano Wenger Venger, Former Yugoslavia c ni ch mfano papic inatamkwa papich. Scandinavian ni Y mfano Jana Yana). Sweden A ni O m
Nilipitiwa na ndoto za mchana badala ya kuandika Botswana nikaandika Gaborone nakujua vizuri nilishafika hadi kunakoitwa Kanye kuna hospital I inaitwa Kanye hospital,'being run by Adventist church'(inahudumiwa na kanisa la wasabato) 'Kanye is a located in southern part of Botswana'
 
Ukiwa maskini alafu rafiki zako nao ni maskini, ni ngumu sn kutoboa
Botswana siyo nchi maskini. Per capita income yake inaizidi China kea mbali. Hii ni nchi yenye uchumi mzuri kuyazidi mataifa mengi ya Asia, America Kusini na baarhi machache ya Ulaya.

Botswana
Since independence, Botswana has had one of the fastest growth rates in per capita income in the world. Botswana has transformed itself from one of the poorest countries in the world to an upper middle-income country. GDP per capita grew from $1,344 in 1950 to $15,015 in 2016.

China
China's per capita disposable income stood at 30,733 yuan (4,461.95 US dollars) in 2019, up 5.8 per cent year on year in real terms.17 Jan 2020
 
Siku hizi nyumbani kwetu, tunapata wageni wengi.
Nasikiaga wageni ni baraka.... Karibuni sana wageni mama yupo.
 
Rais wa Jamhuri ya Botswana, Mokgweetsi Masisi

Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Botswana, Mokgweetsi Masisi anatarajia kuwa na ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania, kuanzia kesho Juni 10, 2021 kwa mwaliko wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Juni 9, 2021 amesema Rais Masisi atawasili nchini kesho asubuhi na baada ya hapo atakuwa na mazungumzo ya mwenyeji wake Ikulu Jijini Dar es Salaam.

"Viongozi wetu wanatarajia kuzungumzia masuala ya ushirikiano kati ya nchi zetu mbili, uhusiano wa kidiplomasia, matumizi ya lugha ya Kiswahili nchini Botswana, bishara na uchumi pamoja na namna ya kuimarisha zaidi Jumuiya ya maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc)," amesema.

Balozi Mulamula amesema Rais Masisi ataondoka nchini Ijumaa Juni 11, 2021 baada ya kutembelea kituo kimoja wapo cha biashara hapa nchini (ambacho hakukitaja).
 
Rais wa Jamhuri ya Botswana, Mokgweetsi Masisi

Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Botswana, Mokgweetsi Masisi anatarajia kuwa na ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania, kuanzia kesho Juni 10, 2021 kwa mwaliko wa Rais Samia Suluhu Hassan...
Hii sasa ndiyo Tanzania aliyoiasisi J K Nyerere ambayo ilikuwa ndiyo kinara wa diplomasia katika Africa. Mwendazake akichafua sana taswira ya nchi yetu. Kwa sasa wageni wanapishana
 
Botswana siyo nchi maskini. Per capita income yake inaizidi China kea mbali. Hii ni nchi yenye uchumi mzuri kuyazidi mataifa mengi ya Asia, America Kusini na baarhi machache ya Ulaya...
Tofautisha pato la taifa na nchi tajiri, hii hata dikteta alikuwa nayo sn sijui uchumi wa kati wapi kumbe hakuna kitu
 
Kwa kweli wengine tuliobahatika kutumika huko, wale wamejitahidi sana kuweza kupata maendeleo kwa kuwa na siasa liberal na kuwa na misingi mizuri ya Uchumi, financial displine, demokrasia kuanzia na Rais wao wa kwanza Sir Seretse Khama, baadae Sir Masire,Mogae, Iwn Khama na sasa Kasisi na kwa kweli pamoja na nchi yenyewe kuwa semi arid, lakini wamejaribu kuhakikisha zile natural resources chache walizonazo kama madini, mifugo na sekta ya utalii wako vizuri na kuingiza pesa nyingi za kigeni na pesa kutumika vizuri, ili kusaidia kuimprove maisha ya wananchi na kuboresha miundombinu nk. Kwa kweli wako vizuri.
Botswana siyo masikini mkuu. Wako vizuri sana
 
Unahisi akikanyaga ndio ukoo wako utaondokana na umasikini?

Hivi hii tabia ya wanachadema kuhisi kwamba maendeleo yenu yataletwa na wazungu inakuwaje yani?

Wao walitembelewa na nani mpaka wakawa hapo walipo?

..wanaweza kuwa na hoja.

..kwa mfano, ni nchi ngapi za Afrika zimewahi kutukopesha fedha za miradi ya maendeleo?

..chukulia miradi ya kimkakati ya SGR na bwawa la umeme, je fedha za miradi hiyo tumezikopa toka Wazungu, yaani Ulaya na Marekani, au tumekopa kwa Waafrika?
 
Back
Top Bottom