Rais wa Botswana, Mokgweetsi Masisi kufanya ziara nchini Tanzania kesho June 10, 2021

CreativityCode

Senior Member
Aug 8, 2020
119
1,000
President Mokgweetsi Masisi will undertake a Working Visit to Dar es Salaam, Tanzania tomorrow, June 10 2021 and return on Friday.

"His Excellency the President will meet with his counterpart, Her Excellency Mrs. Samia Suluhu Hassan, President of the United Republic of Tanzania, to among others discuss ways of broadening the scope of bilateral cooperation between their two countries. The Heads of State will also deliberate on the political and security situation in the SADC Region," statement from Office of the President.

======

Rais wa Jamhuri ya Botswana, Mokgweetsi Masisi anatarajia kuwa na ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Tanzania, kuanzia kesho Juni 10, 2021 kwa mwaliko wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Liberata Mulamula akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Juni 9, 2021 amesema Rais Masisi atawasili nchini kesho asubuhi na baada ya hapo atakuwa na mazungumzo ya mwenyeji wake Ikulu Jijini Dar es Salaam.

"Viongozi wetu wanatarajia kuzungumzia masuala ya ushirikiano kati ya nchi zetu mbili, uhusiano wa kidiplomasia, matumizi ya lugha ya Kiswahili nchini Botswana, bishara na uchumi pamoja na namna ya kuimarisha zaidi Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC)," amesema.

Balozi Mulamula amesema Rais Masisi ataondoka nchini Ijumaa Juni 11, 2021 baada ya kutembelea kituo kimoja wapo cha biashara hapa nchini (ambacho hakukitaja).
 

Maghayo

JF-Expert Member
Oct 5, 2014
7,021
2,000
President of Gaborone.
Hivi ni kweli huo mji mkuu wa Botswana Gaborone unatamkika Gabohone. Yani na sisi waafrika kwa Swagger tunawaiga mabeberu kwa mabeberu ufaransa na ujerumani W ni Z mfano Wenger Venger, Former Yugoslavia c ni ch mfano papic inatamkwa papich. Scandinavian ni Y mfano Jana Yana). Sweden A ni O mfano Adam Odom.
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
52,553
2,000
Hivi ni kweli huo mji mkuu wa Botswana Gaborone unatamkika Gabohone. Yani na sisi waafrika kwa Swagger tunawaiga mabeberu kwa mabeberu ufaransa na ujerumani W ni Z mfano Wenger Venger, Former Yugoslavia c ni ch mfano papic inatamkwa papich. Scandinavian ni Y mfano Jana Yana). Sweden A ni O mfano Adam Odom.
Spain Juwan ni Huwan, Julio = Hulio
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom