Rais wa Benki ya Dunia Mr. Kim ajiuzulu nafasi yake

Nafasi ya mkurugenzi wa Benk ya Dunia ni mali ya USA hakuna raia wa nchi nyingine anaruhusiwa kupata nafasi hiyo kama siyo raia wa USA. Hata Ulaya hawaruhusiwi, wao ya kwao ni ukurugenzi wa IMF tu.

Wakubwa walishagawana siku nyingi hayo mashirika. Sisi wamatumbi na wengine wa dunia tunaishia vyeo vya umeneja, ukurugenzi wa idara, mwakilishi wa banki nchi fulani au kanda fulani na unaibu tu.
OK, nadhani hili suala la maslahi kila nchi naona linashika kasi sana. Sasa bwana Kim inaonekana alitofautiana na USA
 
Ameamua kujiunga na shirika lingine linalohusiana na uendelezaji na uwekezaji wa miundombinu katika nchi zinazoendela. Hakosi kazi huyo.

"After leaving the bank, Kim says he will “join a firm and focus on increasing infrastructure investments in developing countries. The details of this new position will be announced shortly.” He will also serve as a senior fellow at Brown’s Watson Institute for International and Public Affairs and rejoin the board of Partners In Health..."

Source: vox.com
Sasa hapo atakuwa anatumwa na USA kuja afrika kufanya project finance na P2P ili kumpiku China. Sasa hii itakuwa vita kali za kiuchumi. Maan USA na wenzake walitumia karata ya hizo IMF na WB na inaonekana hayo mashirika wadau wameshaanza kuyastukia, na pia ya ukiritimba mwingi kiasi kwamba China yeye hajali ndiyo maana labda wameamua kutengeneza kitu kingine kuwapumbaza waafrika
 
Kwamba alichaguliwa na Obama, inatosha kuwa sababu ya kujiuzulu kwani hawezi kufanya kazi na Trump hata kama ni mtendaji mzuri!
 
Hahaha, ila sema hizo nafasi zinakuwa na siasa sana. Yaani ukitofautiana na wale ma big tu unaenda na maji. Sasa sijui Mh. Kim kaenda kinyume na nani, unaweza kuta ni Trump
Hakuna mwingine zaidi ya Trump kama kweli aliwekwa na Obama ilikuwa lazima tu aende na maji sera za Trump na Obama ni ni paka na panya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna mwingine zaidi ya Trump kama kweli aliwekwa na Obama ilikuwa lazima tu aende na maji sera za Trump na Obama ni ni paka na panya

Sent using Jamii Forums mobile app
Yeah ila kweli kabisa. Unajua Obama alijitahidi kubadili upepo, sasa ona IMF eti mkuu wake lazima atoke ufaransa sijui kwa nini
 
January 8, 2019
Washington DC USA

Rais wa World Bank, Jim Yong Kim ajiuzulu ghafla. Rais huyo raia wa Marekani amechukua hatua hiyo kutokana na tofauti zake za kisera na Rais Donald Trump wa Marekani. Kujiuzulu kwa kiongozi huyo wa Benki kunatoa fursa kwa Rais Donald Trump kutumia ushawishi wake kupatikana bosi mwingine anae endana na sera za utawala wa Rais Trump.

Jim Yong Kim ataachia wadhifa wake huo mwishoni mwa January mwaka huu kama taarifa yake iliyosambazwa na barua pepe yake kwa wafanyakazi wa benki hiyo.

Rais huyo wa Benki ya Dunia alikuwa kipenzi wa sera za Tanzania kujenga miundo mbinu kama flyover za jijini Dsm. Chini ya uongozi wake Bw. Jim Yong Kim waliamini ukijenga barabara basi kipato cha watu walio karibu na miundo mbinu hiyo kitaongezeka kwa asilimia 70. Ndoto hiyo ya World Bank iliifanya kutoa mkopo kwa nchi kama Bangladesh na Tanzania kwa ajili ya ujenzi wa barabara.

Mwaka 2017 Bw. Jim Yong Kim alitembelea Tanzania na kusifia juhudi za serikali ya awamu ya tano ktk kupanua miundo mbinu ya usafiri wa barabara za mijini hususan barabara za juu kwa juu kwa kutoa mkopo wa ujenzi wa Mfungale Flyover jijini Dar es Salaam.

Hatua hiyo ya ghafla ya Rais huyo wa Benki ya Dunia kujiuzulu inaweza kuathiri nchi zilizokuwa kipenzi cha Bw. Jim Yong Kim. Bw. Jim Yong Kim alipendekezwa na Rais Baraka Obama kuwa Rais wa Benki ya Dunia mwaka 2012.

Benki ya Dunia ni chombo chenye nguvu ulimwenguni katika kusaidia nchi zinazoendelea kupunguza umasikini, kukuza uchumi, ujenzi wa miundo mbinu, elimu na kupambana na magonjwa.
 
Why Dr. Jim Yong Kim went to World Bank
5 Sep 2018
Sep.05 -- Dr. Jim Yong Kim, World Bank president, talks about his job interview with President Obama. Kim says that during their talk, he told the president that he'd read his mother's PHD dissertation, a move Obama later called one of the best "ploys" to get a job he'd "ever seen." Dr. Kim speaks in the latest episode of "The David Rubenstein Show: Peer-to-Peer Conversations."

Source : Bloomberg Markets and Finance
 
Back
Top Bottom