Rais wa Benki ya Dunia kuzuru Manzese | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais wa Benki ya Dunia kuzuru Manzese

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Jan 23, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,585
  Likes Received: 5,772
  Trophy Points: 280
  na Makuburi Ally

  WAKATI Rais wa Benki ya Dunia, Robert Zoellick anatarajia kuzuru Manzese jijini Dar es Salaam wiki ijayo, wajumbe wa mitaa ya Mwembeni na Midizini wamegoma kushiriki shindano la usafi kwa mitaa minane ya kata hiyo.

  Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwa sharti la kutotaja majina yao gazetini, wajumbe hao walisema hatua ya kufanya usafi ni ya zimamoto kwa sababu tukio hilo linatakiwa kufanyika mara kwa mara.

  Walisema pamoja na kutolewa kwa shindano hilo, lakini mitaa hiyo haikidhi haja ya kuwa mitaa licha ya kuwekwa kwenye ratiba ya kutembelewa na Zoellick.

  Mshindi wa kwanza wa shindano hilo anatarajiwa kuzawadiwa sh 150,000 wakati mshindi wa pili atajinyakulia vifaa vyenye thamani ya sh 100,000.

  Mitaa iliyotajwa kushiriki shindano hilo ni Uzuri Chakula bora, Mnazi Mmoja, Mvuleni, Kilimani, Muungano, Manzese Uzuri, Midizini na Mwembeni. Hata hivyo mitaa ya Mwembeni na Midizini imegoma kushiriki.

  Walisema kabla ya ujio huo, wameshauri Ofisi ya Waziri Mkuu itembelee mitaa ya Manzese na ijionee hali ilivyo kwa sasa.

  Mradi huo umefadhiliwa na Benki ya Dunia ambayo ilitoa sh milioni 600, Halmashauri ya Kinondoni ilitoa sh milioni 334 na wananchi walitakiwa kuchangia sh milioni 334.
   
 2. K

  KunjyGroup JF-Expert Member

  #2
  Jan 23, 2010
  Joined: Dec 7, 2009
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Ningekua rais wa Tz natamani sana kitu kimoja; KUFUKUZA WORLD BANK NA IMF. Polocies zao za kipumbavu, ujinga wa kunyenyekea akili za mzungu, kukosa uzalendo na ufisadi wetu ndivyo vimetufikisha hapa tulipo!
   
 3. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #3
  Jan 23, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hivi kweli hawajatembelea mpaka sasa? Hata wa Halmashauri husika? Huu ndio mwanzo wa mtu kuumbuka. Walidhani hizo pesa kutoka Benki ya Dunia ni sadaka! Sasa wajifunze maana ya ufuatiliaji.

  Amandla.......
   
 4. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2010
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,402
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  your're a victim of brainwash!!
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,520
  Likes Received: 19,943
  Trophy Points: 280
  Ndulu kajengea swimming pool
   
 6. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #6
  Jan 24, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  And you, you are a victimof programmed mind!
   
Loading...