Rais wa Argentina amsihi Messi asijiuzulu

Babu wa Kambo

JF-Expert Member
May 2, 2016
559
808
Rais wa Argentina Mauricio Macri amemwita nyota wa soka wa nchi hiyo Lionel Messi kwa lengo la kumuomba atengue maamuzi yake ya kujiuzulu kucheza soka la kimataifa.

Messi alifikia maamuzi hayo baada ya timu yake kushindwa kwa mara ya pili mfululizo katika fainali za Copa America huku akiwa miongoni mwa wachezaji waliokosa mikwaju ya penalti.

160627100204_messi_640x360_reuters_nocredit.jpg

''Amemwita na kumueleza namna anavyoona fahari kwa kiwango kizuri kilichoonyeshwa na timu yake katika michuano hiyo huku akimtaka asisikilize maneno ya watu'' alisema msemaji wa rais Macri.

Ndani ya miaka mitatu Messi ametinga katika fainali tatu tofauti moja ikiwa ni ya kombe la dunia nchini Brazili mwaka 2014 ambapo walipoteza dhidi ya Ujerumani,na nyingine mbili za Copa America moja ikiwa mwaka 2015 na 2016 zote timu yake ikipoteza dhidi ya Chile.

CHANZO: BBC Swahili
 
hahahaaa wako serious bhana, sasa bongo mpira (michezo) tunaitaka ila sasa siasa bhana, TBC wameshindwa kuonyesha hata mechi moja hata mechi zetu wenyewe tumeshindwa kuzithamini bado tunataka tuitwe wa kimataifa..... michezo mashuleni tumeondosha bado tunataka ku-create ajira hahaha aza Bongo Mivie?? Haya twende tu....
 
Wa Argentina wengi bado wanamhitaji katika timu yao ya Taifa mana anaushawishi pia.
 
Umuhimu wa mess ni mkubwa sana kwa timu yake ya Taifa. Hivyo baasi asikate tamaa kikubwa akaze sana pia kuwepo kwake kunawatia moyo wachezaji wenzake
 
Nadhani kutokana na umuhimu wake katika Timu ya Taifa wanahofia pia kuondoka kwake ataondoka na wengi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom