Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,694
- 40,720
HabariLeo; Wednesday,November 07, 2007 @00:01
TUNAUNGA mkono agizo lililotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Albert Mnary, ya kutaka maelezo kutoka kwa wenyeviti wa wilaya na Halmashauri ya Manispaa juu ya upotevu wa fedha unaofikia Sh milioni 360 zilizotolewa na Serikali Kuu kwa ujenzi wa madarasa chini ya Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM).
Tunasema hivyo kwa sababu kiwango hicho cha fedha si kidogo, na kama zingetumika ipasavyo zingesaidia kupunguza kwa kiasi fulani tatizo la upungufu wa madarasa.
Kinachosikitisha ni kwamba fedha hizo haziko benki na wala madarasa yaliyosudiwa kujengwa hayapo. Dalili zilizopo zinaonyesha kwamba fedha hizo zimekombwa benki na kutumika kwa malengo tofauti na ya binafsi.
Mnary amenukuliwa akisema uchunguzi wa awali unaonyesha kwamba kuna baadhi ya watumishi wa halmashauri hizo ambao wanamiliki kampuni hewa, wanazozilipa fedha za walipa kodi kwa kazi ambayo haikufanyika.
Matarajio yetu ni kwamba agizo lake litatekelezwa katika kipindi alichokiweka na sheria itachukua mkondo wake kwa watu binafsi na kampuni ambazo zitabainika kuhusika na mtandao huo wa ujenzi wa madarasa hewa.
Kwetu sisi tukio la upotevu wa fedha za MMEM Bukoba linatonesha donda la matukio mengine kadhaa ya aina hiyo, yaliyotokea siku za nyuma katika sehemu nyingine nchini na kusababisha hasara inayokisiwa kuwa ya mabilioni.
Kama hiyo haitoshi, Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES) nao unagubikwa na tuhuma kadhaa kama hizo ambazo mara kadhaa zinawahusisha maofisa wa halmashauri, wakuu wa shule, madiwani na kampuni binafsi.
Wakati wachache hao wakitunisha mifuko na matumbo yao kutokana na wizi wa fedha za umma, kwa upande mwingine wa sarafu waathirika ni taifa zima kutokana na kushindwa kufikia lengo la kuboresha elimu ya vijana wetu ambao ni taifa la kesho.
Sisi tunaamini tunastahili kuungana mikono kupambana dhidi ya ufujaji huu wa rasilimali chache za umma wa Watanzania wengi masikini ambao watoto wao watajikuta wakikosa hata elimu ya msingi kama hatutachukua hatua za haraka. (call about understatement)Bukoba wametuonyesha njia. Tuwaige mfano kwingineko kwa kufichua ubadhirifu wa fedha za MMEM na MMES.