Rais unakumbuka ahadi yako kuhusu experience kazini?

Sigara Kali

JF-Expert Member
May 28, 2017
3,623
8,441
Salaam wanaJF
Kichwa cha habari chahusika
Nakumbuka wakati flani wa kampeni za uchaguzi mkuu 2015 ndugu Pombe Magufuli akiwa mgombea wa CCM katika kampeni zake alizungumzia suala la ajira Kwa vijana na akazungumzia suala la kuawataka vijana/wanaoomba kazi Kuwa na experience
Akasema suala hili si sawa kama kijana kamaliza chuo mpeni kazi hiyo experience ataipatia kazini
Lakini naona imekua tofauti baada ya kuingia madarakani ,taasisi nyingi Sana z serikali zinapotangaza nafasi za kazi sharti moja wapo Kwa Yule mwombaji awe na experience tena ya miaka kuanzia 3 na kuendelea.Sasa vijana waliomaliza chuo na hawana experience hizo ajira hawazipati
Au ndo mnataka wazee waendelee kukalia ofisi ? Inakera Sana kila ikitangazwa ajira utasikia experience atleast 5 years ,shit
Timiza ahadi yako ili vijana wapate hizo nafasi,suala la experience linawanyima riziki
 
Hawezi kuwa anaikumbuka hiyo ahadi.

Kuna ahadi nyingi tu hazikumbuki..

Laptops kwa wanafunzi, mil 50 kila kijiji, kuna sehemu kibao aliahidi madaraja mpaka kesho hakuna kitu.

Hiyo ndio CCM.
 
Ukimkumbusha hayo hakawii kusema watanzania wanapenda udaku
 
  • Thanks
Reactions: SDG
_20170607_171005.JPG

Tangazo la ajira NHIF la hivi karibuni
 
Hawezi kukumbuka,wakati wa kampeni akiwa Tabora alisema wanafunzi wote watakao dahiliwa kuingia vyuo vikiu watapewa mkopo hila kilichotokea ni wanafunzi 25k kati ya 80k ndio waliopewa mkopo.
Huyu mzee sio wakumuamini kabisa
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Hujamsikia Alipokanusha Kwenye Uteuzi Wa Anna Mghwira Wakati Akiwa Zanzibar Alisema Mpinzani Hawezi Kuingia Serikali Ya Viwanda
Haaa Sasa Hivi Kageuka
Aje Akumbuke Hilo Haiwezekani Experience Lazima
 
UKWELI NI KWAMBA POST ZOTE AMBAZO NI SINIOR POST ZINAHITAJI MTU MWENYE UZOEFU,KWA SABABU ZIFUATAZO
MOSI,KUWAPA MOTISHA WALE AMBAO WAMEJITOA KUTUMIKIA MSHAHARA WA SERIKALI WA POST ZA CHINI AMBAYE ATAPANDA MPAKA ATAFIKIA BAR HUSIKA NA AKAWA MAY BE MSAIDIZI WA MKURUGENZI THEN AKAAMUA KUOMBA IKIWA ANASIFA. ATAFANYA USAILI THEN KUAJILIWA KWA POST HUSIKA.
PILI,KUMPA MTU NAFASI AMBAYE UNAMJUA MADAHIFU NA UWEZO WAKE
TATU,KUPUNGUZA UWEZEKANO WA MKURUGENZI KUDANGANYWA KWA KIGEZO HAJUI AU HANA UZOEFU NA KAZI HUSIKA
NNE,KURAHISISHA UWAJIBIKAJI, NA KUPUNGUZA KUKAIMISHA WATU MAJUKUMU AMBAYO SI YAO NA PASIPO ULAZIMA
TANO,UTUNZAJI WA SIRI
SITA,,,,,,,,,,,,NK

NINAVYOJUA POST AMBAZO HAZIIITAJI UZOEFU SERIKALINI NI ZA KUANZIA YAANI BAR ENTRY MFANO AFISA MSAIDIZI AU AFISA DARAJA LA PILI AMBZAO PIA KIMSINGI HAMA HAMA YAKE MPAKA (KM UMEAJILIWA)MWAJIRI AKUAMISHIE OFISI NYINGINE SIO KUAMUA TU LEO ULIKUWA KILIMO KESHO MALIASILI KWA KUWA WAMETOA TANGAZO LA AJILI NA UNAVIGEZO ILA KWA POST ZA SINIOR OFFICERS NDIPO SHERIA/KANUNI/MIONGOZO(NIMESAHAU VIFUNGU) HAIJABANA KUHAMA HAMA MAWIZARA AU OFISI ILA IMEWEKA KIGEZO CHA UZOEFU
View attachment 520813
Tangazo la ajira NHIF la hivi karibuni
 
Back
Top Bottom