Rais umeweza kuuvunja uliokuwa mwamba wa Dar es Salaam. Mkuu wa wilaya ya Kilosa ndugu Mgoyi anakushinda?

nguruka wa kig0ma

JF-Expert Member
Jan 16, 2020
1,957
2,000
Huyu mkuu wa wilaya ya Kilosa ndg Mgoyi, ni mjivuni kwelikweli Anafanya anavyotaka wala hajali watu wa wilaya hiyo.

Anachukua ardhi za wakulima bila ridhaa yao. Watu wanalalamika yeye Hana habari nao. Mh Rais nakumbuka ulipokwenda kilosa, ulikuta ana kashfa ya kupora ekari 300 kwenye shamba la mkonge Kimamba ulilofuta hati ya muwekezaji ili wagawiwe wananchi,lakini ulimsamehe na kumataka ajisahihishe.

Bwana yule kwasasa ana mashamba ya mpunga Kilangali na Mvumi kwa maekari.

Wananchi wanakodishwa lakini yeye ana hodhi mamia ya maekari.

Yapo mengi anayafanya kinyume na maadili ya utumishi wa umma.

Yupo afisa tarafa Dumila anaitwa Nchimbi huyo ndiye mtumishi wake na siyo wa umma.
 

mbikagani

JF-Expert Member
Dec 5, 2014
3,048
2,000
Huyu na timu yake inayoongozwa na Mw/kiti wa CCM wilaya ni kero kwa wakulima Kilosa.
 

Mtego wa Noti

JF-Expert Member
Nov 27, 2010
2,491
2,000
Acheni wivu wa kijinga. Huko unakosema amehodhi kuna aliyekosa eneo la kulima? Kwa nini mtu akiamua kulima kisasa kwa mitambo ya kilimo nyie mnaanza kuona wivu. Dc ni mchapa kazi kuanzia ofisini mpaka kwenye kilimo. Tulieni afanye kazi acheni majungu
 

moudgulf

JF-Expert Member
Jan 23, 2017
96,468
2,000
Mkuu kwani Kiongozi wa uma kama amepata ardhi kihalali, akaamua kuwekeza vilivyo kwenye kilimo kosa liko wapi?

Mkoa wa Morogoro acheni majungu.

Mnayo ardhi nzuri sana lakini hamtaki kujizatiti, wageni wakipiga kazi mnaanza kulia lia kwa wivu.

Morogoro vijijini, kijiji cha Mvuha, wametoa ardhi yao kihalali kabisa ambayo haijawahi kuguswa kwa aliyekuwa Waziri Luwhaga Mpina, baada ya kumuona Mpina amejaza mashine ili alime wakaanza kuleta fitna.

Unafiki wa aina hii unarudisha nyuma maendeleo ya Morogoro.
 

nguruka wa kig0ma

JF-Expert Member
Jan 16, 2020
1,957
2,000
Acheni wivu wa kijinga. Huko unakosema amehodhi kuna aliyekosa eneo la kulima? Kwa nini mtu akiamua kulima kisasa kwa mitambo ya kilimo nyie mnaanza kuona wivu. Dc ni mchapa kazi kuanzia ofisini m0aka kwenye kilimo. Tulieni afanye kazi acheni majungu
Mjinga anweza kubadirika na kuwa mwelevu lakini siyo mpumbavu.
Wewe mpumbavu, hata tukikuweka na ngano kinuni upumbavu wako hautakutoka Bali ngano itaiva

Wewe utakuwa nchimbi afisa tarafa dumila maana ndiye kidampa wake.
Unajua mpk mitambo yake!

Issue siyo kulima Wala analimaje Bali anapataje mashamba.
Watu wanadhurumiwa ardhi na yeye.
Soma vizuri uelewe
 

Mtego wa Noti

JF-Expert Member
Nov 27, 2010
2,491
2,000
Kama i
Kuwa umezaliwa mwaka 2020 huezi jua laana ya kilosa.
Kilosa haikuwa ilivyo leo, inazidi kuporomoka,
Kama kilosa inakaliwa na watu mmejaa majungu kama wewe lazima iporomoke tu. Mtu anajiongeza anawekeza kwenye kilimo na anatoa ajira kibao wewe unaombea atumbuliwe. Kwa nini kilosa isife?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom